Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

TANGAZO LA UFADHILI KWA WASANII CHIPUKIZI WA FILAMU NA MUZIKI

1.     Wewe  ni  msanii  chipukizi  wa  filamu au  maigizo ?
2.     Wewe  ni  mwandishi  chipukizi  wa  filamu  ?
3.     Wewe  ni  mtayarishaji  chipukizi  wa  filamu ?
4.     Wewe  ni  muimbaji / mwanamuziki  chipukizi 
 Unataka  kukamilisha  ndoto  zako  lakini  haujui  pa  kuanzia ?  Kama  jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako.
Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  inapenda  kuwatangazia  wananchi  wote  kuwa  sasa,  tumeanza  kutoa  ufadhili  na  udhamini  kwa   wasanii  chipukizi  wa  filamu, waandishi  chipukizi  wa  filamu, watayarishaji ( Producers )  chipukizi  wa   filamu   pamoja  na  waimbaji(wanamuziki ) chipukizi   wenye  sifa  zifuatazo :
1.      Awe  na  kipaji  cha  kuigiza  AU
2.     Awe  na  kipaji  cha  uandishi  wa  filamu   AU
3.     Awe  na  nia  thabiti  ya  kuwa  mtayarishaji  wa  filamu  AU
4.     Awe  na  kipaji  cha  uimbaji.
5.     Awe  raia  wa  Tanzania  na  mkaazi  wa  jijini  Dar  Es  salaam.
6.     Awe  na  umri  wa  kuanzia  miaka  14   hadi   55.
     
     UTARATIBU   WA  KUTUMA  MAOMBI  
Tuma  maombi  yako  kupitia  barua  pepe  yetu  ambayo  ni  : rafikielimutanzania@gmail.com   . Maombi  yaelekezwe  kwa
Mkurugenzi  Mtendaji,RafikiElimu  Foundation, S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.
   AU 
Unaweza  kuleta  maombi  yako  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu. Ofisi  zetu  zipo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU. 
Kufika  katika  ofisi zetu,  panda  daladala  za  UBUNGO- CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  30  SEPTEMBA  2013.
Kwa  maelezo  zaidi   wasiliana  nasi  kwa  simu  0782405936  au  0756606085   

NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU ISHIRINI 20,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.


Juu