Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU_KITABU CHA RUTHU_ ''SEHEMU YA PILI''.

Baada ya utangulizi na kuona nini maana ya ushirika ikwa sambamba na Maandiko Matakatifu; leo napenda kukupa mwendelezo wa somo hili zuri sana.
Leo tunaingia sehemu ya pili.

NB: UNAOMBWA KUTOA MAONI YAKO KUHUSU SOMO HILI PIA JE MUNGU AMEKUHUDUMIA KWA KIASI GANI KUPITIA SOMO HILI?


















USHUHUDA WA WATU WALIOKUWA NA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU.

Daniel 6:10.
Hata Daniel, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake; ( na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalem ) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
* Daniel alikuwa na maisha ya Ushirika na Roho Mtakatifu, si kwa sababu tu ya matatizo yaliyomkabili.

Zaburi 55: 16,17.
Nami nitamwita Mungu, Na Bwana ataniokoa; Jioni, asubuhi na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
* Ushirika na Roho Mtakatifu unatufanya kuwa waombaji, pia hutufanya tumtegemee Mungu 
   zaidi katika maisha yetu ya kila siku sanjari na kila pito tunaloweza kulipitia katika maisha yetu.

Marko 1:35.
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.

* Yesu alikuwa na ushirika na Roho Mtakatifu
* Ushirika _ Ni urafiki
* Ushirika na Mungu ni moyo wa Mungu kuwa ndani yangu / yako; au moyo wa Mungu kuwa moyo wangu/
   wako.

1Kor. 6:17.
Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
* Ushirika ni umoja katika roho / moyo.

Ruthu 1:1-5.
Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili; Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. Akafa Elimeleki mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Wakakaa huko yapata miaka kumi. Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.

* Siku zote Mungu anatufundisha ili tupate faida, tupate kufanikiwa.
* Ziko nyakati za njaa. Je! Unafanya nini yanapotokea hayo?


Je! unafanya nini wakati unapokuwa chini / kupungua nguvu za kiroho?
Yesu alifanya nini alipoguswa na yule mwanamke mwenye kutokwa na damu? (maana alihisi kupungukiwa nguvu).

* Wakati wa kushuka / kupunguka nguvu ndio wakati muafaka wa kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu
* Elimeleki aliikimbia njaa - AKAFA. Hatutakiwi kukimbia.


UNAFANYA NINI NJAA INAPOINGIA? (sehemu ya tatu)   Itaendelea, Usikose!


Sikiliza wimbo huu wa Christina Shusho, Ushirika na Roho. Barikiwa!




MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA MZIMA BILA DOSARI APATWA NA TATIZO LA KICHWA KUJAA MAJI; MAMA MZAZI WA MTOTO AHITAJI MSAADA WA MAOMBI BAADA YA KUHANGAIKA KILA MAHALI HADI KWA WAGANGA WA KIENYEJI BILA MAFANIKIO.




MITHALI 24:11.

Siku ya Jumapili ya tarehe 24. March 2012, Blog hii ilikuwa maeneo ya Kongowe, Kibaha Mkoani Pwani. Nilikutana na dada mmoja ambaye aliniambia kuwa mtoto wake alimzaa akiwa salama kabisa, lakini siku moja alishangaa kuona akimkalisha mtoto chini hawezi kukaa, akimsimamisha anasimamia vidole, akashtuka. Ndipo alipoamua kumpeleka hospitali, akaambiwa mtoto ana matatizo ya kichwa kujaa maji. JINA LA MTOTO NI: EVA.

Dada huyu amehangaika sana na mtoto tangu January mwaka jana hadi leo, amezunguka kila mahali kutafuta msaada wa kunusuru maisha ya mtoto wake. Lakini sasa ameamua kumrudia Mungu na anaomba msaada wa maombi kwa ajili ya mtoto wake.
Amefungua mlango kwa mtumishi yeyote kwenda nyumbani kwake kumtembela na kufanya huduma ya maombi pamoja.

WITO:

IKIWA WEWE NI MWANAMAOMBI/MTUMISHI NA UNA HUDUMA YA USHAURI NA KUFUNGUA WALIO KATIKA VIFUNGO, NAOMBA UWASILIANE NAMI KWA NAMBA ZIFUATAZO ILI IKIWEZEKANA TUONGOZANE TUKAFANYE HUDUMA HIYO PAMOJA, NA MUNGU ATATUKUZWA.... NA WEWE UTABARIKIWA ZAIDI.



0659 700 002 / 0756 145 417.

PICHA ZINGINE.





Juu