Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

ZIJUE TABIA NNE ZA IMANI


Kama kawaida ya blog hii, jumapili hii ilikuwa ndani ya kanisa la Ebenezer IPHC Tabata Segerea ambapo mtumishi wa Mungu Rev. Meinralr Anthony Mtitu aliuwasha moto na watu wengi waliponywa kwa namna ya ajabu na pekee sana! Ibada ilipoisha watu hawakutaka kuondoka.

Rev. Meinrald Anthony Mtitu katika fundisho lake alifundisha na kuhubiri zaidi juu ya mambo manne kuhusu tabia za Imani.







MAMBO MANNE KUHUSU IMANI:
Mwanzo 6:9--  
Kielelezo ni Nuhu.

1* Imani inamtumaini Mungu hata pale ambapo hapaleti maana yeyote, pale ambapo mazingira yanakataa lakini imani bado inatumaini wakati mtu mwingine akiangalia anaona huku ni kuchanganyikiwa.

Imani inatumaini mahali ambapo katika akili (reasoning) huoni maana - mahali ambapo hesabu zinakataa, formula zinakataa, principle zinagoma, Lakini imani bado inatumaini.
Pale ambapo mazingira yanakataa, ushahidi (facts) unakataa, lakini imani inasema ndio - na hii ndio tabia ya imani.

Kwa imani Nuhu akajenga safina.
Ikumbukwe kuwaNuhu hakuwahi kuona safina hapo kabla, lakini Mungu anamuambia utajenga safina. Pia Nuhu hajawahi kusomea kazi ya kutengeneza safina wala hakuwa engineer.

Hivyo imani inaamini wakati kila kitu hakileti maana. Bali italeta maana utakapotii na kuchukua hatua.

2* Imani haisubiri kuona, kugusa, kuhisi, kunusa au kusikia.
Nuhu alikuwa hajawahi kuona mvua lakini aliamini, maana tangu kuumbwa ulimwengu mvua ya kwanza kunyesha ilikuwa ni wakati wa gharika.
Nuhu alimuamini Mungu kwa kutarajia kuona kile Mungu alichokusudia kufanya.
Nuhu hakujua gharika itakuwaje, lakini alimwamini Mungu.

3* Imani inasubiri haikati tamaa.
Imani ni uwezo wa kusubiri ahadi ya Mungu juu ya neno fulani alilosema bila kukata tamaa.
Ibrahimu anaitwa baba wa imani kwa sababu alisubiri zaidi ya miaka 20 kupata mtoto.
Nuhu alisubiri miaka 120 ndipo mvua ikanyesha.

4* Imani inatii kile Mungu alichosema au kuagiza bila kujali kitakuwa kigumu kiasi gani, au kitakuwa na changamoto kiasi gani. Ndio maana inajengwa kwenye msingi wa neno la Mungu. Neno hili laweza kuwa la jumla (Logos) au maalumu ( Rhema ).

MUNGU AKUBARIKI.

Ukiwa na maoni niandikie upande wa kulia wa blog hii kuna mahali pameandikwa ''WASILIANA NAMI HAPA'' Au mahali pameandikwa ''Client Testimony''


Mawasiliano mengine:
0659 700 002
mdeejunior@gmail.com




KUNA WATU WANAOKUJA DUNIANI KIMYA KIMYA NA KUONDOKA KIMYA KIMYA

Harris Kapiga_The Critical Thinker.
Msikilize hapa, akiwa ndani ya Nchi Ya Ahadi, Sinza!

7 Ways to Stop the Adultery Epidemic

It happened again. For the third time in six months, the pastor of a large church in my hometown of Orlando, Fla., has resigned from his pulpit because of adultery. I’m sad. I’m sick. I’m sorry for the pastors, and sorrier for the congregations that are having to deal with the fallout caused by bad choices.

I’m also cringing because an increasingly hostile public sees these train wrecks as evidence that Christians are hypocrites who preach one thing and live another. We stand for biblical marriage between one man and one woman, but in many cases those marriages are failing. No wonder the gay community hates our flimsy platitudes.

Why are we witnessing this epidemic of moral failure? Many factors could be cited (easy access to pornography, sex-saturated entertainment, the devil and his demons, etc.)—but I don’t think we need a list of excuses today. I’m tired of excuses. The devil does not make us do this. It is totally possible for Christian men and women to live in holiness today. The power of His grace is not affected by social trends or hell’s attacks.

Maybe we’ve made this too complicated. Let’s go back to some basic ways we can stay pure:

1. Practice regular “fire drills.” Paul told Timothy to “flee” from youthful lusts (2 Tim. 2:22). But you can’t flee a burning building if you don’t know where the exits are. If you don’t map out your plan of escape, you won’t run when you are confronted with a lustful glance, an X-rated website or a brazen proposition. When faced with temptation, don’t play with it, talk to it, stroke it, analyze it or revisit it in an hour. Just bolt for the door!

2. Don’t live in isolation. Many people are vulnerable to moral compromise because they spend so much time alone. God designed us to live in community. If King David had not left his brothers on the battlefield and returned home, he would not have seen Bathsheba skinny-dipping on the roof. You are less likely to succumb to temptation if you are surrounded by family or Christian friends.

3. Stay faithful in spiritual disciplines. Nothing makes the heart colder than a lack of quiet time with God. Charles Spurgeon said, “Prayer will make you leave off sinning, or sinning will make you leave off praying.” If you have spent time with Jesus in the morning, you are not going to invite Delilah to cut your hair off that evening. If you are too busy with your work to pray and read the Bible, you are already headed for a spiritual train wreck.

4. Be ruthless with temptation. Today’s wimpish Christian culture encourages us to be soft toward sin. Yet the apostle Paul used athletic imagery when he taught about the strenuous effort of resisting sin. He wrote, “I discipline my body and make it my slave, so that, after I have preached to others, I myself will not be disqualified” (1 Cor. 9:27, NASB). If you can’t resist looking at a pornographic website, you are a spiritual baby. If you can’t run when Potiphar’s wife turns on her charm, you need to get your jellyfish spine in shape. Grow up and quit making excuses for your weak morals.

5. Confess your sins regularly. Last weekend during a men’s conference in Philadelphia, one brave brother shared openly how he had been molested as a child—and how the trauma of abuse led him into a pattern of fornication. After he shared his weakness, dozens of men felt the freedom to come to the altar and confess their sexual sins. Transparency is the path to sexual purity. You cannot expect to be pure if your inner life is a cesspool of ugly secrets. Tell somebody. Get the monkey off your back.

6. Keep the home fires burning. I’ve met many Christian men who struggle with all kinds of sexual temptation. But after talking with them, I learn that they have no regular intimacy with their wives. The apostle Paul taught that husbands and wives have an equal responsibility to fulfill each other sexually (1 Cor. 7:3). If the fires have gone out in your marriage, find a counselor or enroll in a marriage course in your church. God can rekindle romance and repair your communication breakdown before your chilly marriage freezes beyond repair.

7. Get regular spiritual checkups. Adults are supposed to see a doctor annually to prevent heart ailments, cancer and other problems. Yet many of us never open our lives to input from pastors or mentors. (And many pastors have no one to examine them!) Learn to ask for prayer and counsel. Share your struggles and weaknesses. If you detect a weak spot in your armor, don’t wait until the devil blows you out of the water to ask someone for help.

SOURCE: Ministry Today.

TUNAJIFUNZA NINI KWA MWEREZI WA LEBANONI ?

By Rev. Meinrald Anthony Mtitu.















Bonyeza hapa ununue mafuta halisi ya alizeti yasiyochakachuliwa kutoka Singida ili ku-support Blog hii.

Psalms 92:12-15
Key verse 12b.  Atakuwa kama mwerezi wa Lebanoni

Kabla ya kutambua ni nini hasa ambacho Mungu anapenda tujifunze kwa mwerezi, ni lazima kwanza tutambue sifa za mwerezi halafu ndipo tunaweza kuyaingiza maisha yetu humo kama kanisa la Tanzania (mwili wa Kristo) na mtu mmoja mmoja!



SIFA ZA MWEREZI WA LEBANONI
1. Unavutia
2. Mrefu sana, unakadiriwa kuwa na urefu kati ya mita 40-45
3. Matawi yake yamesheheni majani
4. Una mzunguko (circumference) wa mita 11-12
5. Unaishi miaka mingi (approx. 1000-2000 yrs)
6. Unaweza kustahimili misimu yote ( all seasons ) na majani yake hayapukutiki.
7. Una mizizi mirefu sana kwenda chini hivyo haung'oleki kirahisi.
8. Hauozi: kwa sababu hakuna mdudu yeyote anayeweza kuula, una harufu ya asili ambayo
    hufukuzawadudu wa aina zote.

Mwerezi ni picha ya Uimara na Uthabiti.

TUNAJIFUNZA NINI KWA MWEREZI

1. Mungu anatutaka tukue kwenda chini.
    Kabla ya kwenda juu sana lazima uende chini kwanza (Ukuaji)

Aina za Ukuaji
a, Ukuaji wa kwenda chini
b, Ukuaji wa kwenda juu.

Ukuaji wa kwenda chini.
Ili tuwe hivyo ni lazima tuwe na mizizi kwa sababu ndio inayosafirisha nishati(minerals) pia hutafuta Uhai. Katika hili ndiko tunajenga mambo ya msingi yafuatayo:

Ukuaji wa kiroho
> Ukuaji wa uhusiano wetu na Mungu yaani kutafuta source yetu na Mungu.
> Uhusiano wetu na Mungu ndio unaoleta maendeleo ya ukuaji wetu
> Mizizi ya kiroho.

Kukua kwenda juu.
Haya ni maisha yasiyofichika ambayo watu wengine watayaona ( Ushuhuda )


2. Mungu anataka tukue kwa nje/kupanuka (outward growth)
    Ni maisha ya kuongezeka katika kuwa baraka kwa watu wengine.

3. Mungu anataka tuwe na ukuaji endelevu (onward growth)
    Hubaki kuwa wa ukijani misimu yote (remain evergreen in all seasons)
    Hauchoki/haukomi kukua

Tusikome kukua katika Mungu.

Asante kwa kuwa pamoja nami, AMEN!





NGUVU YA SADAKA.

By. Pastor Magreth Marton @ Ebenezer IPH_Church.

Sikiliza neno fupi juu ya nguvu ya sadaka, sadaka iletayo majibu.

 +255 659 700 002
+255 756 145 417



BADILISHA MAISHA NA LADHA YA NDOA YAKO LEO


STORY FUPI INAYOWEZA KUBADILISHA MTAZAMO WA NDOA YAKO 

“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.


Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Judy. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Judy. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!

Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Judy aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.

Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Judy.

Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

Nilimsimulia Judy kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Judy alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Judy tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Judy kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.

Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.

Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapanda ngazi. Judy alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Judy, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Judy, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’

Ikawa kama Judy alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.

Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema.

Ni Wewe_Ebenezer praise team!
Bonyeza kitufe cha play  kusikiliza wimbo huu.


Toa maoni yako, story hii imekusaidia?

Source: Mary Muna.


KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 



Understanding The Purpose And Power Of Woman_ By. Dr. Myles Munroe

   Dr. Myles Munroe is an internationally known author, lecturer, teacher, life coach and government consultant and leadership mentor. He has spent the last thirty years traveling the world training leaders in business, education, government and religion. He delivers his message on personal and professional development to more than 500,000 people each year and millions through his Media program.








Women of every culture and society are facing the dilemma of identity. Traditional views of what it means to be a woman and changing cultural and marital roles are causing women conflict in their relationships with men. Women are under tremendous stress as they struggle to discover who they are and what role they are to play today in the family, the community and the world.

Are women and men equal?

How is a woman unique from a man?

What does the Bible really teach about women?

Is the woman to blame for the fall of mankind?

What are the purpose and design of the woman?

Are women meant to be leaders?

What is a woman's basic communication style?

What are a woman's emotional and sexual needs?

What is a woman's potential?

To live successfully in the world, women need a new awareness of who they are, and new skills to meet today's challenges.


SOURCE: Myles Munroe On Relationship.

Contact me on.
+255 659 700 002

Dream Big As You Grow Big.
mdee junior

Fundisho La Msingi I NENO LA MUNGU NI NINI NA SIO NINI...

   http://mdeejunior.blogspot.com     Kutokufahamu maana halisi ya Neno la Mungu kumeleta tatizo kubwa kwa Wakristo wengi kama sio wote kuishi kwa mazoea na kumuwekea Mungu mipaka ya kiutendaji! Naomba tuingie kwenye somo. 
   Bwana Yesu husika na kila mmoja anayeenda kujifunza hiki ambacho unamletea siku ya leo, fungua fahamu na moyo wa kupokea; kwa Jina lako Yesu, Amen!





Neno la Mungu sio nini:


> Neno la Mungu sio Historia ya Mungu.

> Neno la Mungu si-habari kuhusu Mungu.
> Neno la Mungu si-mapokeo ya kidini.

Neno la Mungu ni nini:


Neno la Mungu ni NIA / AZIMIO ndani ya moyo wa Mungu na ni kama mawazo. Lakini Mungu anapoitamka / anapoisema nia yake - Hilo ni Neno la Mungu. Neno la Mungu ni NIA iliyosemwa na Mungu.


Mithali 23:7a

Maana aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo.

* Awazavyo mtu ndivyo alivyo.
* Ukifanikiwa kuyakamata mawazo ya mtu fulani, utakuwa umemkamata mtu huyo.
* Nafsi ya mtu ni jumla ya mawazo awazayo.

Mungu na wazo lake ni mtu mmoja, yaani vile Mungu awazavyo ndivyo alivyo. Mungu ana uwezo.

Zaburi 33:6, 11
Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
Shauri la BWANA lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
* Hili neno liko juu ya historia na habari ya Mungu.

Yohana 1:1 
''Naye Neno alikuwa Mungu''

> Muundo mzima wa mawazo ya mtu, ndivyo mtu huyo alivyo; na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu.

> Moyo wa Mungu ndio Mungu mwenyewe.

Marko 7:1-9
' Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake, wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa. Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao...'

> Tunaona wazi kabisa, hapa wanafunzi walikuwa wakibomoa historia na mapokeo ya kidini.
Mfano: Nyoka wa shaba pale jangwani > Nia ya Mungu ilikuwa ni kutoa unabii juu ya Yesu Kristo. Yesu Kristo akapambana na Mafarisayo na Wayahudi ili kuwatoa katika historia ya Musa na kuwaingiza katika NIA ya Mungu.

Maombolezo 3:33. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.
> Uzima uko ndani ya Neno la Mungu.

Luka 12:13-15
Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. Akamwambia, mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu? Akawaambia, angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

> Yesu anajua ukweli wote, hakuna uzima katika wingi wa vitu.
> Uzima - ni furaha, amani, na upendo ndani ya mioyo yetu.
Uzima unapatikana wapi kama sio katika wingi wa vitu? Yohana 1:1,4- uzima unapatikana ndani ya neno la Mungu.

Zaburi 23:1.
Bwana ndiye Mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

Hapa Daudi alikuwa anamaanisha hivi:
* Ndani ya Mungu nimejaa kila kitu.
* Nimejaa furaha, shangwe, uzima, amani, - mtu awaye yote asinisumbue.
* Shetani anawadanganya watu kwa sababu wamekata tamaa katika umaskini.
> Ili kuwa na furaha na ujasiri kama wa Daudi ni lazima KUJAA.
> Mtu aliyejaa huwezi kumwonea huruma; mfano. Yesu hawakumuonea huruma, maana ALIJAA.
> Ili Mungu aweze kukutana na mahitaji yetu ni lazima tuwe na charge / TUJAE.

Yakobo 1:2-4
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbali mbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

> Hii ni hatua ya KUJAA.
> Saburi hutufanya kuwa watimilifu na utimilifu huo kuwa mkamilifu.
> Ni lazima kukaza moyo. Pasipo kukaza moyo huwezi kuyaona hayo.

Habakuki 3:17-19
Maana mtini hautachanua maua, wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, na mashamba hayatatoa chakula; zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe; Walakini nitamfurahia Bwana, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. Yehova, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.

Naomba maoni yako humu.

Dream Big As You Grow Big

By. mdee junior.

Contact:

+255 659 700 002
+255 756 145 417

mdeejunior@gmail.com (email)

@mdee_junior (twitter)
mdee.junior (skype)







Juu