Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

RIWAYA : JINAMIZI LA MABINTI



MTUNZI: ELIA MWAIPOPO
SEHEMU YA 1

KWA WASOMAJI WAPYA


Hadithi hii ni ya kubuni tu, lakini yenye kueleza uhalisi wa maisha  na mambo yafanyikayo hasa kwenye ulimwengu wa roho (spiritual realm) na ule ulimwengu wa damu na nyama (physical realm), majina yaliyotumika hayana uhusiano wowote na watu wenye majina kama hayo …

Jinamizi lisilojulikana kwa kipindi kirefu, limeendelea kuwakumba mabinti wengi vigori kwa njia za kishirikina pasipo wao kujitambua. Mabinti hao licha ya kuwa na mvuto mkubwa mbele ya vijana watanashati wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuziteka hisia zao na kujikuta wakishawishika na kujiingiza katika mahusiano ambayo yanahatarisha maisha ya vijana hao kwa muda mrefu. Usiri mkubwa unatawala katika vifo hivyo vya kusikitisha hali inayopelekea kuibuka kwa hofu kubwa katika jamii….Hadithi inaanzia kwa msichana Monica, usiku wa manane huku akiwa kitandani anashituka na kuanza kushuhudia maruweruwe mengi, kwa taharuki kubwa anaamkaa na ……ENDELEA
*******************************************************


Yapata majira ya saa nane za usiku, Monica anashituka ghafla akitokea usingizini alikokuwa amelala na kuanza kuona matukio ya ajabu machoni mwake, ghafla anahisi nywele zikimsisimka na kuanza kutetemeka, haukupita muda kijasho chembamba kinaanza kumtiririka usoni kwake hali iliyoambatana na hofu kubwa inayoyabadili kwa kiasi kikubwa mapigo ya moyo wake na kuyafanya yawe na kasi zaidi.
*********************************************
Huku haya yakiendelea Monica anahisi kupata hisia juu ya kile kilichokuwa kikiendelea lakini asijue nini cha kufanya. Anachungulia dirishani huko nako anapokewa na kiza totoro kilichosheheni weusi mithili ya mkaa. Taharuki inazidi kuukumba moyo wa Monica pale anapohisi joto na baridi vikiongezeka mwilini mwake kwa pamoja.
******************************************************
Zinapita dakika kumi na tano huku akiwa ameduwaa anajaribu kujitafutia msaada kwa kupiga yowe kubwa ambalo linakuwa halina maana yoyote kwani halikuwa likisikika na mtu yeyote aliyekuwa karibu na chumba chake. Kufumba na kufumbua macho Monica anajikuta yuko ndani ya kifuu mithili ya kile cha nazi kwa udogo na na taratibu anapaa kuelekea asikokujua huku joka kubwa likiwa limezunguka kingo za kifuu hicho ambacho kwa wakati huo kilikuwa kikipaa taratibu.
*************************************************************************

Wakati hayo yakitokea joka lilikuwa likitema moto wa cheche za kijani kuelekea machoni na kuzitisha mboni za Monica binti ambaye alikuwa akisifika kwa uzuri na sifa kem kem. Ndiyo ulikuwa ni msafara mkubwa uliokuwa ukiongozwa na Madubwana ambayo ni maarufu kama Majitu yaliyokuwa na sura za kutisha ambapo yalikuwa na macho matatu na pembe tatu..Juu ya mboni zao Madubwana hayo inasemekana kulikuwa na machipukizi ya viganja mithili ya vile vya binadamu na inasadikika kuwa hali hii ilitokana na mahusiano yao ya hapo zamani yaliyokuwepo baina ya Madubwana hayo na binadamu wa kawaida ambapo inasemekana uhusiano wao uliharibiwa na Madubwana pale yalipoanza kuwakamata na kuwala binadamu.
***************************************************
Wakati Monica akifikiria namna ya kujinasua akajikuta akipokea amri yenye vitisho ambayo ilimuamuru kutokugeuka wala kupiga kelele “Usigeuke wala kupiga kelele, achama mdomo wako ili tuingie na tujihifadhi kwa miaka ijayo” kisha amri hiyo ikafuatiwa na kicheko cha dharau “aaaaaaahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa” kicheko ambacho kilimfanya Monica azidi kujihisi kuwa uhai wake ulikuwa ukikaribia kufikia tamati. Muda ukapita zaidi na Monica kwa wakati fahamu zilikuwa zimemtoka na hakujua nini kilikuwa kikiendelea kwa wakati wote wa safari hiyo ndefu iliyogharimu siku saba .
******************************************************************
Ilikuwa ni safari ya kuelekea angani liliko anga la kaskazini ambako inasemekana na kuaminika na wengi kuwa huko ndiko viumbe wengi na wa kila aina wenye kustaajabisha walikimbilia huko baada ya mifarakano mikubwa kutokea duniani yakiwemo Madubwana na viongozi wao. Awali, kabla ya Majitu kuja duniani na kumnyakua Monica palikuwa pametokea balaa kubwa sana la njaa hali iliyopelekea Madubwana mengi kupoteza maisha. Inasemekana takribani miaka saba Majitu yalikosa kabisa chakula na maji, mwanzoni katika kutatua tatizo hilo majitu yalianza kukamatana yenyewe na kulana kama chakula na wakati mwingine yalilazimika kukamata madubwana mazee ambayo yalikuwa dhaifu na kuanza kuyala kama chakula. Hali hii ilisababisha majitu kupungua kwa kasi kubwa sana.
************************************************************************

Inaaminika baada ya madubwana mazee kuisha Madubwana yalianza kupunguza sehemu za viungo vyao na kuvifanya kama chakula chao. Mikia yao ambayo ilikuwa imenona mafuta na pembe zilizokuwa kavu mithili kuni zilizokaukia juani kwa kipindi kirefu nazo ziligeuka na kuwa msaada mkubwa sana kwa madubwana hayo. Habaari za taabu na kutaabika kwa majitu hayo zilimfikia kiongozi wao ambaye kwa wakati huo wala hakuwa na habari juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwani yasemekana ilipokuwa ikikaribia majira ya kipindi cha joto Kiongozi huyo maarufu kwa jina la Iisambo alishuka duniani na kuyaendeleza maisha yake yaliyoshabihiana kwa karibu kabisa na majini walioko duniani. Tofauti yao ilikuwa wakati majini walioko duniani walikuwa wakiishi kwa kunyonya damu binadamu na viumbe wengine, Irisambo aliishi kwa kutegemea nyama za binadamu na viumbe waliokuwa wakiishi katika dunia ya tatu.
Kwa kuwa hali ilikuwa ni tete katika anga hilo la kaskazini Irisambo siku moja aliitisha kikao kilichodumu kwa takribani masaa kumi na mbili akitafakari kwa kina kiini cha matatizo yake na suluhisho la matatizo yaliyokuwa yakiwakabiri madubwana hayo. Katika kutafuta suluhisho hilo akaja na mbinu ambazo kwa fikra za kijitu Irisambo aliona ni njia mbadala wa kutatua tatizo hilo………..ITAENDELEA
**********************************************************************
**********************************************************************
SHARE &COMMENT


ITAENDELEA JUMATANO 24/07/2013  

UZINDUZI WA ALBAM YA ''AMANI YA BWANA'' YA RUNGU LA YESU KWA UDHAMINI MKUBWA WA KAMPUNI YA HALISTA ENTERPRISES.


UZINDUZI HUU UNAKUJIA KWA UDHAMINI MKUUUBWAAA KABISA WA KAMPUNI YA HALISTA ENTERPRISES WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI WA MAFUTA HALISI YA KUPIKIA YA ALIZETI KUTOKA SINGIDA.
NUNUA MAFUTA HALISI YASIYOCHAKACHULIWA.

MAFUTA HAYA YATAKUWEPO SIKU YA UZINDUZI NA YATAUZWA KWA BEI NZURI KABISA ( REASONABLE PRICE ), USIKOSE KUJA NA PESA UJIPATIE MAFUTA HALISI YA ALIZETI katika ujazo wa Lita 1 Na Lita 5.

Mkurugenzi wa kampuni ya Halista Enterprises atakuwepo na atazungumza!

Ukitaka kujua bei za Mafuta tembelea http://halisitz.blogspot.com/ AU Tupigie 0659 700 002


ANANIA MWASOMOLA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA AJA NA KWAITO STYLE.


Anania Mwasomola azungumza na Blog hii. Mwandishi na mmiliki wa Blog hii alikuwa na machache ya kumuuliza kuhusu huduma yake ya uimbaji.

Blogger: Kijana mbona uko kimya sana, vipi uko wapi?
Anania:  Niko Mbeya, nina mikutano kadhaa ya Injili. Nataraji kuja Dar mwanzoni mwa mwezi wa nane 2013.

Blogger: Wapenzi na washabiki wako watarajie nini baada ya ukimya huu?
Anania:  Washabiki wangu watarajie mambo mazuri. Nakuja tena kwenye kazi ya Mungu na albamu ya pili.
              Ni kitambo sija toa nyimbo mpya tangu nilipo achia albamu ya WEWE NI BABA ambapo hadi sasa video yake imekamilika na mwezi wa nane itakuwa sokoni. Wakati huo huo albmu yangu mpya ambayo jina nimelihifadhi nitaliweka wazi nikikamilisha kazi ila kwa wale wapenzi wa nyimbo za taratibu,wajiandae kupokea, Mungu kanipa nyimbo ya taratibu moja naamini itawagusa wengi sana kwa neema ya Mungu.

Blogger: Umesema kwenye albam mpya kuna wimbo mmoja wa taratibu, zilizobaki zipo kwa style ipi?
Anania:  Nimetumia kwaito style kwenye nyimbo zangu naamini zitawabariki sana, nawapenda wapenzi wangu kama wanavyonipenda.

Blogger: Kwa nini umeamua kuja na kwaito.
Anania:  Ooh kwaito naipenda sana kwani haiko kikwaya zaidi kitu ambacho inawafanya watu wamataifa (wasiomjua Mungu) waweze kusikiliza na ni rahisi kuwapata na wakaja kwa Yesu.
Kiukweli waimbaji wa gospel tunapenda kuigana kitaifa sio kimataifa so mimi nakaa kimataifa zaidi.

Anania Mwasomola aliendelea kufunguka zaidi kwa kuwatolea mifano baadhi ya waimbaji anaowakubali.

Mfano ni dada Christina Shusho, wabongo wengi hawa mwelewi anaimba nini, lakini ukienda mataifa ya nje Shusho anajulikana kuliko unao wajua hapa bongo, hii nimeona kwa nchi nilizo tembelea hapa africa.Wanampenda sana Shusho naamini nitafikia viwango vyake na kuzidi.

Pia John Lisu wabongo hawa mwelewi kabisa ila kiukweli ndo mwimbaji wangu sana na mwansasu wana uwezo wa kuimba live muda wowote.

Mwisho. Naomba wapenzi na mashabiki wangu wakae tayari kupokea kitu kipya kutoka kwenye albamu mpya (AUDIO)

Blogger: Mungu akuzidishe kama mchanga wa baharini.

TUMA MAONI YAKO.

ZIJUE TABIA NNE ZA IMANI


Kama kawaida ya blog hii, jumapili hii ilikuwa ndani ya kanisa la Ebenezer IPHC Tabata Segerea ambapo mtumishi wa Mungu Rev. Meinralr Anthony Mtitu aliuwasha moto na watu wengi waliponywa kwa namna ya ajabu na pekee sana! Ibada ilipoisha watu hawakutaka kuondoka.

Rev. Meinrald Anthony Mtitu katika fundisho lake alifundisha na kuhubiri zaidi juu ya mambo manne kuhusu tabia za Imani.







MAMBO MANNE KUHUSU IMANI:
Mwanzo 6:9--  
Kielelezo ni Nuhu.

1* Imani inamtumaini Mungu hata pale ambapo hapaleti maana yeyote, pale ambapo mazingira yanakataa lakini imani bado inatumaini wakati mtu mwingine akiangalia anaona huku ni kuchanganyikiwa.

Imani inatumaini mahali ambapo katika akili (reasoning) huoni maana - mahali ambapo hesabu zinakataa, formula zinakataa, principle zinagoma, Lakini imani bado inatumaini.
Pale ambapo mazingira yanakataa, ushahidi (facts) unakataa, lakini imani inasema ndio - na hii ndio tabia ya imani.

Kwa imani Nuhu akajenga safina.
Ikumbukwe kuwaNuhu hakuwahi kuona safina hapo kabla, lakini Mungu anamuambia utajenga safina. Pia Nuhu hajawahi kusomea kazi ya kutengeneza safina wala hakuwa engineer.

Hivyo imani inaamini wakati kila kitu hakileti maana. Bali italeta maana utakapotii na kuchukua hatua.

2* Imani haisubiri kuona, kugusa, kuhisi, kunusa au kusikia.
Nuhu alikuwa hajawahi kuona mvua lakini aliamini, maana tangu kuumbwa ulimwengu mvua ya kwanza kunyesha ilikuwa ni wakati wa gharika.
Nuhu alimuamini Mungu kwa kutarajia kuona kile Mungu alichokusudia kufanya.
Nuhu hakujua gharika itakuwaje, lakini alimwamini Mungu.

3* Imani inasubiri haikati tamaa.
Imani ni uwezo wa kusubiri ahadi ya Mungu juu ya neno fulani alilosema bila kukata tamaa.
Ibrahimu anaitwa baba wa imani kwa sababu alisubiri zaidi ya miaka 20 kupata mtoto.
Nuhu alisubiri miaka 120 ndipo mvua ikanyesha.

4* Imani inatii kile Mungu alichosema au kuagiza bila kujali kitakuwa kigumu kiasi gani, au kitakuwa na changamoto kiasi gani. Ndio maana inajengwa kwenye msingi wa neno la Mungu. Neno hili laweza kuwa la jumla (Logos) au maalumu ( Rhema ).

MUNGU AKUBARIKI.

Ukiwa na maoni niandikie upande wa kulia wa blog hii kuna mahali pameandikwa ''WASILIANA NAMI HAPA'' Au mahali pameandikwa ''Client Testimony''


Mawasiliano mengine:
0659 700 002
mdeejunior@gmail.com





Juu