Shalom_Shalom,
Mabibi na Mabwana - Singles & Couples Karibuni kwa meza ya Bwana
tupate kula na kunywa pamoja. Namshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu
Kristo ambaye kwa ajili yenu amenichagua niwe mpishi wenu siku ya leo
; Nami
najitoa kwa nia ya dhati kabisa kwa ajili yenu/yetu sote kwa kusudi jema
kabisa la
Kujenga na Kupanda.
Ni mimi
Mjoli wenu katika
KRISTO_YESU Bwana wetu.
1KORINTH 7:1-11, Key Verse Yetu.
Basi kwa habari ya mambo yale
mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya
zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na
awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo
mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali
mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.... '
Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila
mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.
Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi
nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa
kuliko kuwaka tamaa ' ...!
NB: Unaweza kutusaidia maandiko mengine ku-support andiko/somo tajwa hapo juu.
Ni ukweli usiopingika kwamba huwezi kuzungumzia
Mahusiano
ukayamaliza, mahusiano ni mfano wa bahari ambayo ndani yake
kuna/imebeba mambo mengi sana na mengi mapya huzaliwa kila iitwapo leo.
Mahisiano ni hali ya kuhusiana/kubaliana/relate/share/patana/connections - na kinyume chake chaweza kuwa sahihi pia.
DONDOO_MUHIMU_UTANGULIZI.
* Kuwa na msimamo ( sio kuwachezea wasichana/umiza hisia/feelings zao/tesa mioyo yao)
* Usimwambie msichana kwamba unampenda kama hutamwambia utamuoa
* Mwanaume ndiye anayeanzisha/initiate urafiki
* Kawaida mwanaume ana huruma kwa mwanamke - hawezi kumkatalia mwanamke
* Usiwe omba omba wa upendo, na kamwe usimvulie nguo yako ya ndani ili
kumthibitishia/mwonyesha kuwa unampenda, kama zipu yako mbovu ama sketi
yako imekatika kifungo - Hima wahi kwa fundi (YESU KRISTO) aweke mambo
sawa nawe utakuwa salama.
Tunapozungumzia mahusiano lazima yawe
baina/kati ya watu wa jinsia mbili tofauti kike na kiume, ni mahusiano
ya urafiki kati ya jinsia hizi mbili ambayo yatapelekea uchumba hatimaye
yatapelekea ndoa.
Mahusiano haya yanahitaji maarifa/ufahamu na
ustadi. Mahusiano ya uchumba sio kuangaliana usoni ama kukodoleana macho
tu basi, Bali ni pamoja na kuulizana maswali magumu na kuzungumza juu
ya mambo ya msingi kwa sababu ni kitu/jambo la maisha.
WAKATI_GANI_USIO_MZURI_KUINGIA_KWENYE_UCHUMBA_MAHUSIANO!
a> Kamwe usiingie kwenye mahusiano/uchumba kama hujui
WITO_WAKO - Mungu amekuitia nini.
Mfano: kama huna muelekeo wa huduma (nazungumza na kijana aliyeokoka) -
Efeso 4:1, ...' mwenende kama inavyoustahili
wito_wenu mlioitiwa.
Kuoa/olewa na mtu asiye na muelekeo ni hatari sana. Ni lazima NIITWE/UITWE pamoja na mke wangu/wako katika huduma.
Muelekeo wa watu wawili ni muhimu - makusudi na nia ya mioyo ipatane/shikane pamoja.
Wito wa Mungu katika maisha lazima uwe nambari moja (1) katika
kuoa/olewa, wito/muelekeo/shauku ya moyo iwe ni mapenzi Mungu na sio
kutaka tu kutimiza mambo yako/nia zingine (ke/me).
Ndio maana
utakuta mke/mume kabla ya kuoa/olewa alikuwa mtumishi mzuri sana na
kujitoa sana kwa ajili ya Mungu/BWANA, lakini mara tu baada ya
kuoa/olewa huduma inakuwa si huduma tena ama inakufa/zorota au kushney
kabisa.
b> Kama umekata tamaa usiingie kwenye mahusiano.
Usifanye maamuzi kama umefishwa/vunjwa moyo - maana 95% ya maamuzi yako
yatakuwa mabovu na mwisho wa siku utaujutia uamuzi ulioufanya.
Itaendelea.
Next: SABABU 11 MBOVU ZINAZOFANYA WATU WAOANE.
Wasiliana na mwalimu wa somo hili:
0766 730 360 / 0659 700 002