Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

UNGA BORA WA LISHE - Kutoka FamareX Products & Co..


FAMAREX - The Home Of Natural Products.

Mara nyingi umekutana na unga wa lishe wa aina tofauti tofauti na watengenezaji/waandaaji tofauti tofauti na mchanganyiko tofauti tofauti wa nafaka.

Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawana/wamekosa Elimu sahihi kuhusu Lishe sahihi yenye mchanganyiko wa nafaka sahihi kwa uwiano/ration sahihi.

Lishe yeyote isipozingatia uwiano sahihi wa mchanganyiko wa nafaka na aina ya nafaka inayotumika - Ni ukweli kwamba italeta madhara makubwa kiafya; kwa watoto hata watu wazima.
FamareX Products Imekuja na majibu sahihi yatakayosababisha/leta KICHEKO KWA FAMILIA yako na/au mtu mmoja mmoja.

Unga Bora wa Lishe uliotengenezwa/andaliwa na FamareX Products umezingatia mambo yote muhimu - Aina ya nafaka, Idadi/kiwango cha nafaka na uwiano kati ya nafaka moja hata nyingine.

ANGALIZO/USHAURI WA KITAALAM: 
1. Ukienda kununua unga wa lishe alafu ukakuta umechanganywa na karanga, USINUNUE.
2. Kama utanunua unga wa lishe kwa ajili ya matumizi ya mtoto wa umri chini ya miaka miwili alafu ukakuta Lishe hiyo ina mchanganyiko wa nafaka zaidi ya mbili, USINUNUE.
SABABU ZA KIAFYA:
  • Karanga ni nzuri endapo mtumiaji atafuata utaratibu unaotakiwa kiafya. Karanga iliyosagwa inatakiwa itumike ndani ya siku saba; zaidi ya hapo inakuwa na madhara mwilini/kiafya.
  • Karanga ikikaa zaidi ya siku 7 (saba) ina kawaida ya kuweka/ota fungus; hivyo hushambulia/huleta/sababisha madhara kwenye figo. Ili utumie karanga kwenye Lishe yako hakikisha unasaga kiasi pembeni itakayotosheleza muda wa siku saba, hivyo wakati wa kupika uji wako ndipo utakuwa unaongezea karanga uliyoiandaa.
  • Lishe yenye nafaka zaidi ya mbili si nzuri kwa afya ya mtoto chini ya miaka miwili kwa sababu mfumo wake wa mmeng'enyo/digestion system haina uwezo wa kumeng'enya nafaka nyingi kitu ambacho kitamsababishia mtoto asipate choo vizuri na utaupa kazi kubwa mfumo wa umeng'enyaji chakula.

JIPATIE SASA KWA AFYA YAKO NA FAMILIA YAKO.
Unga huu wa Lishe unapatikana kwenye ujazo wa nusu kilo ( 500g ) na kilo moja ( 1Kg ).
Kwa mauzo ya Jumla na Reja Reja.
Pia Tunapokea Oda mahali popote ( DAR na MIKOANI ).

WASILIANA NASI:
Simu: 0659 700 002 / 0766 730 360
Barua Pepe: famarexproducts@gmail.com


Ipe Familia Yako Kicheko kwa kuipatia Lishe Bora.

Mkurugenzi,
FamareX Products & Co.
P.O.Box 7331, D'salaam, Tz.
+255 659 700 002

AFYA TEA SPICE KWA AFYA BORA

 
FAMAREX PRODUCTS & CO.
The Home Of Natural Products.


Tunapenda kuitambulisha bidhaa bora kabisa ijulikanayo kama ''AFYA TEA SPICE''
 
Afya Tea Spice ni moja kati ya bidhaa za FamareX iliyojipatia umaarufu kwa virutubisho asilia, hukupa afya bora na nguvu zaidi.
Afya Tea Spice ni nzuri kwa rika zote pamoja na wagonjwa pia. Haina kemikali, ni asili, haihitaji kutumia majani ya chai; yenyewe inajitosheleza.





MUHIMU:
*** Ina kiwango kikubwa cha mchanganyiko wa virutubisho vingi vya madini, vitamini ‘flavoids’, ‘isoflavones’, ‘polyphenols’ ‘terpenes’ , saporins’ , phytosterols’, na phytate.

*** Husaidia kuzuia mtu asipatwe na Saratani zitokanazo na homoni za mwili, kama vile Saratani ya matiti na tumbo. Vile vile ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa mifupa na matatizo ya wanawake baada ya kufikia ukomo wa hedhi (menopause).

*** Bidhaa hii imejipatia umaarufu kwa kuwa na madini, vitamini na virutubisho vingine vinavyopatikana kwenye samaki, nyama, mayai na maziwa. Kwa maana nyingine mtu anayetumia AFYA TEA SPICE kutoka FAMAREX ni sawa na yule aliyekula vyakula hivyo.

*** Virutubisho vya AFYA TEA SPICE aina ya protini na ‘isoflavones’ hushusha kiwango cha kolesterol mbaya (LDL) mwilini, hali kadhalika hupunguza ugandaji wa damu hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya mtu kupatwa na mshituko wa moyo au kiharusi. Vile vile huboresha msukumo na mishipa ya damu mwilini.

*** Kumbuka kuwa protini mwilini huongeza uwezo wa mwili kuhifadhi na kunyonya madini ya ‘calcium’ kwenye mifupa. Kamba lishe (dietary fiber) iliyomo, hurekebisha kiwango cha sukari na uchujaji sumu wa figo.

*** Ni nzuri kwa watu wenye matatizo ya kuwa na macho mekundu, ukosefu wa choo na kusikia kiu kila wakati.

FAIDA NI NYINGI SANA KUZITAJA, HIZO HAPO JUU NI BAADHI/CHACHE TU.

MATUMIZI:
Kijiko kimoja cha chai (au kiasi unachopendelea - kwani haina madhara kiafya) kwa kikombe kimoja cha chai , maziwa au bakuli moja ya uji.
Jali Afya yako na ya familia yako, Tumia bidhaa za FamareX.

PIA TUNAZO SHAMPOO ZA NYWELE zilizotengenezwa kwa kutumia tunda la Apple. Ni nzuri sana, zinafanya nywele zing'ae, zisikatike wala kukakamaa, inasaidia kutibu mba (dandruff).
Kwa wenye mba - tunakuletea suluhisho.
Shampoo hizi ni kwa matumizi ya watu wa jinsia zote (wanaume na wanawake).

Wasiliana nasi:
                                                                                     
 Mkurugenzi,                                                                             
FamareX Products & Co.
0659 700 002
P.O.BOX 7331, Dar es Salaam, Tanzania.  

Marketing Manager,
FamareX Products & Co.
0766 730 360

KARIBU TUKUHUDUMIE.
The Home Of Natural Products.  

Obama takes blame for operation that killed two hostages!


President Barack Obama on Thursday revealed that an American and an Italian hostage were killed in a covert US counter-terrorism operation on the Afghan-Pakistan border in January, saying he took "full responsibility" for the tragedy.

Making public the previously classified finding, Obama expressed his "deepest apologies" to the families of the two hostages, Warren Weinstein and Giovanni Lo Porto.

Two other Americans linked to Al-Qaeda, including spokesman Adam Gadahn, were killed in operations at around the same time, the White House said.

"Based on information and intelligence we have obtained, we believe that a US counter-terrorism operation targeting an Al-Qaeda compound in the Afghanistan-Pakistan border region accidentally killed Warren and Giovanni this past January," Obama said in an unscheduled statement.

"As president and as commander-in-chief, I take full responsibility for all our counter-terrorism operations, including the one that inadvertently took the lives of Warren and Giovanni, he said.

"I profoundly regret what happened. On behalf of the United States government, I offer our deepest apologies to the families."

Weinstein was snatched after gunmen tricked their way into his home in Lahore on August 13, 2011 shortly before he was due to return home after seven years working in Pakistan.

He later appeared in a video in which, under apparent coercion, he asked the United States to free Al-Qaeda prisoners.

Italian aid worker Lo Porto, 39, disappeared in January 2012 in Pakistan.

Weinstein's widow said in a statement that "we are devastated by this news and the knowledge that my husband will never safely return home."

The White House statement did not identify which US agency carried out the operation, which suggests it was carried out by an intelligence service rather than a military unit.

If confirmed, it would be the latest controversy to hit Obama's counter-terrorism operations, which -- while killing Osama bin Laden -- have relied heavily on secret drone strikes.

"We have concluded that Ahmed Faruq, an American who was an Al-Qaeda leader, was killed in the same operation that resulted in the deaths of Dr. Weinstein and Mr. Lo Porto," the White House said.

"We have also concluded that Adam Gadahn, an American who became a prominent member of Al-Qaeda, was killed in January, likely in a separate US Government counterterrorism operation," it added.

"While both Faruq and Gadahn were Al-Qaeda members, neither was specifically targeted, and we did not have information indicating their presence at the sites of these operations."

In his statement, Obama said the US believed that the operation resulting in the hostage deaths "did take out dangerous members of Al-Qaeda."


Source: AFP


Tamko la Serikali Kuhusu Mauaji ya Watanzania Afrika Kusini.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema leo kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa katika mashambulizi dhidi ya wageni huko Durban na Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Mhe. Membe amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Watanzania watatu wameuwawa katika mashambulizii hayo siyo za kweli.

“Nimehakikishiwa na Waziri wa Usalama wa Afrika kusini, David Mahlobo, asubuhi hii kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa, ambao ni raia wa Ethiopia, Zimbabwe, Malawi na Swaziland,” ametaarifu Mhe. Waziri.
Amesema serikali ina taarifa kuwa kuna Watanzania watatu waliofariki dunia nchini Afrika Kusini, lakini hawakuuwawa katika mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni.

“Watanzania hao ni Rashidi Jumanne, ambaye imetaarifiwa alipigwa risasi katika tukio la ujambazi, kilometa 90 nje ya mji wa Durban; mfungwa Athumani China Mapepe, aliyeripotiwa kuchomwa kisu gerezani wakati wa vurugu za wafungwa, na Ali Heshima Mohamed, ambaye alifariki hospitalini kutokana na ugonjwa wa TB,” alieleza Mhe. Membe.

Mwili wa marehemu Mohamed ulirejeshwa nchini jana kwa mazishi. Mhe. Waziri alitaarifu kuwa kuna Watanzania 23 katika kambi iliyotayarishwa na serikali ya Afrika Kusini huko Durban kuhudumia wageni wanaokimbia mashambulizi hayo ya wenyeji, na kuwa utaratibu unafanywa kuwarejesha nyumbani raia 21 walioomba. “Wawili wamesema hawako tayari kurudi.”
Mhe. Membe amesema taarifa ya serikali ya Afrika Kusini inaonyesha kuwa hali ya utulivu imerejea Durban na Johannesburg katika saa 48 zilizopita kutokana na juhudi za Rais Jacob Zuma na kamati maalum ya mawaziri aliyoiteua kushughulikia mashambulizi hayo.

Mapema jana, Mhe. Membe alimwita Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Thamsanqa Dennis Mseleku, na kuelezea kukerwa kwa serikali na mauaji ya wageni na akataka hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha usalama wa Watanzania nchini Afrika Kusini.
Alisema Tanzania inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ambayo imelaani vikali mashambulizi ya Waafrika kutoka nje ya Afrika Kusini. Hata hivyo, Rais Mugabe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), amesifia hatua zinazochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini kukomesha mashambulizi hayo na kurejesha utulivu.
Mhe. Membe aliwataka Watanzania waishio Afrika Kusini na kwingineko nje ya nchi, kujitambulisha kwenye balozi zetu ili iwe rahisi kufuatilia usalama wao na kuwasaidia pale yatokeapo majanga.
“Hatuna takwimu sahihi za idadi ya Watanzania waishio Afrika kusini kwa sababu wengi wao wamekwenda huko kwa njia za panya,” alisema. Inakadiriwa kuna Watanzania 10,000 waishio Johannesburg na Durban.

Akijibu swali la mwandishi wa habari, Mhe. Membe alisema Tanzania inapaswa kutumia utajiri mkubwa wa gesi asilia ilionao ili kuendeleza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vitakavyotengeneza ajira za kuvutia kwa vijana ili wasikimbilie nchi za nje na kuhatarisha maisha yao.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
20 Aprili 2015. 

Source: www.joelnanauka.com

Juu