Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FEDHA BINAFSI.

   Yale mafundisho ya msingi yenye kufungua fahamu bado yanaendelea NCHI YA AHADI kila siku ya Jumapili kuanzia saa tisa alasiri na kuendelea! 
   Katika mwendelezo huo Jumapili ya tarehe 10. Feb. 2013 darasa liliendelea na mada iliyokuwa mezani likuwa ni; NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FEDHA BINAFSI.
Kimsingi wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa ni kituko fulani pale mtu anapokuwa na fedha (haijalishi ni kiasi gani) halafu hajui namna sahihi ya kuitumia ili kujiongezea kipato. Ni jambo moja kutumia fedha zikaisha lakini pia ni jambo lingine kutumia fedha kuongeza kipato. Ili kutumia fedha uliyonayo kuongeza kipato ni lazima uwe na Nidhamu, Je! Nidhamu hiyo unaipata wapi? Fuata na mtaalamu wa masuala ya Fedha, ndugu JOE BISHOTA ambaye ndie aliyekuwa mzungumzaji siku hiyo. 
Kumbuka, ili upate kila kitu kwa ukamilifu wake, Blog hii inakukaribisha NCHI YA AHADI>>> unaweza kuwasiliana kwa mawasiliano yaliyoandikwa mwishoni kabisa katika somo hili.

NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FEDHA BINAFSI (Personal Financial Management).
Na Joe Bishota.

Huhitaji misuli mikubwa kuwa na nidhamu katika fedha yako binafsi, unachohitaji ni kanuni rahisi sana ambazo mtawala wake ni TABIA na UFAHAMU. Tabia inatawala kwa asilimia themanini 80% na Ufahamu unachukua asilimia ishirini 20%.

1. Tabia
Hizi ni tabia ambazo zinakuja kisirisiri kukuchukulia fedha yako bila kujijua. Mfano; mtu mwingine amejiwekea utaratibu kuwa kabla hajaenda kulala usiku ni lazima anywe bia moja au mbili kwa mfano, kimsingi hii ni tabia ambayo inakuchukulia fedha bila kujitambua kwa sababu ukipiga hesabu ya mwezi mzima ni pesa nyingi sana umetumia pasipo ulazima wowote wa kinywaji hicho.

* Kumbuka, utakachokipanda ndicho utakachokivuna.
* Kanuni utakazozipanga maishani mwako ndizo zitakazoamua maisha yako ya usoni (will determine your   future).
* Hizi ni kanuni zinazoendesha maisha yetu kimya kimya.
* Asilimia tisini 90% ya matatizo ya fedha tunasababisha sisi wenyewe kwa kutokuwa na mipango thabiti kama sio imara.
* Ni lazima uamue mwenyewe kubadilisha mazingira yako ya fedha.
* Ni lazima ujue nafasi yako (position)
* Lazima ujue thamani yako (value)
* Lazima ujue thamani ya rasilimali zako (assets).

Fanya zoezi la kuorodhesha madeni yako, fanya zoezi la kuandika thamani ya rasilimali ulizo nazo halafu chukua thamani ya rasilimali zako utoe thamani / jumla ya madeni yako; utapata kiasi kinachobaki.
Kama kiasi kilichobaki ni hasi (negative figure) hiyo ndio thamani yako kwa maneno mengine ujue kuwa umefilisika. Kama kiasi kinachobaki ni chanya ujue unaenda vizuri.

* Ukitaka kuendelea katika maisha lazima ujue thamani yako / nafasi yako.
* Mapato yako lazima yazidi matumizi yako, na kile kinachobaki baada ya matumizi ndio utajiri wako. Matumizi yako yakizidi mapato huwezi kutoka kimaisha.

2. Lazima ujue unataka kwenda wapi (Ufahamu).
> Ili kujua unataka kwenda wapi lazima uamue unaanzaje.
> Lazima uendane na wakati / nyakati kuweza kukabiliana na mabadiliko ya ulimwengu / mazingira na nyanja mbali mbali (updates).

KANUNI TANO (5) KATIKA MATUMIZI YA FEDHA BINAFSI.

1. Matumizi Yasizidi Mapato Unayopata.
> Lazima ujue kinachobaki ndio chanzo cha utajiri wako.
> Wekeza kile kinachobaki baada ya matumizi.

2. Lazima Utafute Namna Ya Kuongeza Mapato.
> Unaweza kuanza na vitu vidogo. Watu wengi wanapata promotion kwa sababu tu wanawahi kazini.
> Kuwa smart, usiingie ofisini ukiwa shaghala baghala.
> Jaribu kufanya kitu cha maana katika muda wako wa ziada.
> Kujitolea na kufanya kazi kwa bidii.
> Jenga mahusiano mazuri na watu. Watu wengi wanapenda kufanya kazi na watu wanaoelewana nao. Mahusiano mazuri yatakupa ndisha daraja na kukupa promotion.
> Kwenye mambo ya fedha tabia ndio inayotangulia.
> Kuwa na tabia ya kutaka kuongoza.
> Kuwa tayari kukubali makosa pale unapokosea.
> Usiwe mtu wa kulalamika
> Jifunze kusimamia mambo yako mwenyewe.

3. Jifunze Kuishi Katika Mapato Yako.
mfano. unapoenda kufanya manunuzi (shopping) andika orodha ya vitu unavyoenda kununua (shopping list) na gharama zake. Siku zote unaponunua kitu / vitu omba punguzo (discount).
> Vunja tabia zingine zisizo na manufaa kwako.
> Lazima ujue vitu unavyohitaji na vitu unavyotaka ( hivi ni vitu viwili tofauti).
> Jifunze kununua vitu kwa jumla (wholesale).

4. Lazima ujue namna ya kutunza pesa yako.
Kile kiasi (cash) kinachobaki ndio mlango wako wa kutokea.
Kabla hujalipa madeni, tenga pesa kidogo ya akiba. Ni mwiko kuigusa hiyo pesa ya akiba (emergency fund).
Kabla hujaanza kuwekeza hakikisha tayari una akiba ya dharura.
Haya yote yatakusaidia kujua jinsi ya kushughulika na madeni.


Watu wanaohudhuria darasa la kupanua ufahamu.

































5. Tafuta namna ya kufanya kitu cha tofauti.


Itaendelea juma lijalo, usikose. Fika Nchi Ya Ahadi.

KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 






Mawasiliano:

+255 659 700 002
+255 756 145 417

Dream Big As You Grow Big.
mdee junior.







WELCOME TO GOIG MODERN SCHOOLS




GOIG MODERN SCHOLLS FOR THE FUTURE OF YOUR KIDS

For more information please call this number.  +255 716 230 441











CAPACITY BUILDING CLASS: NIDHAMU KATIKA MUDA Na MC. Harris Kapiga NDANI YA NCHI YA AHADI..

  
Harris Kapiga ni mtu ambaye kwa muda mfupi nilioweza kumsikiliza nimeweza kujifunza vitu vingi sana katika maisha yangu, ushuhuda wa maisha yake unaweza kubadilisha maisha ya mtu yeyote yule ambaye amefika mahali pa kujiona kuwa si chochote silolote anasubiria kufa tu biashara iishe. Natamani kama wewe ni mmoja wapo miongoni mwa watu waliofikia hatua hii, fanya maamuzi ya kuonana na Mc. Harris Kapiga. Mwanzoni mwa blog hii kuna tangazo linasema KARIBU NCHI YA AHADI MINISTRY, Tumia namba ya simu iliyopo hapo au mwishoni somo hili utaona mawasiliano hapo pia unaweza kutumia.


   Baada ya utangulizi huo mfupi naomba twende moja kwa moja kwenye somo la leo linalosema NIDHAMU YA MUDA sanjari na DONDOO KUMI BINGWA KATIKA KUKUWEZESHA KUTUMIA MUDA WAKO, aliyefundisha somo hili ni MC. HARRIS KAPIGA mwenyewe!

Harris alianza na swali kwa umati wa watu waliokuwa wamehudhuria!

MUDA NI NINI? Kila mtu alijibu vile alivyoweza kwa ufahamu na mtazamowake; mwishoni Harris akaja na jibu sahihi kabisa lililomfaa kila aliyehudhuria na ninaamini hata wewe litakufaa sana na utakubaliana naye.

Muda ni kipindi ambacho vitu hutokea _ Time Is a point or a period at which things occurs. Aliendelea kufafanua kuwa kuna aina mbili za muda.

KUNA AINA MBILI ZA MUDA.

1. Muda wa saa (clock time) 
Yaani muda wa saa tulizo nazo kila siku; mfano. katika dakika moja kuna sekunde 60, siku moja ina masaa 24, mwaka una siku 365. Muda wa saa uko fixed maana yake ni kwamba ukipita umepita huwezi kuubadilisha / kuurudisha nyuma. Kwa maana hiyo basi Muda wa kwenye saa hauhusiki na maisha yetu kwa uko fixed.

2. Muda halisi (Real time).
Muda halisi ndio muda wenyewe hasa unaohusika na maisha yetu na tunapaswa kupeleka macho yetu huko. Mfano. unaweza ukakaa mahali mwezi 1. ukadhani umekaa miaka 10 au ukakaa mwaka 1. ukadhani siku moja kulingana na mazingira halisi ya hapo mahali.
Muda halisi ni muda ambao uko kwenye akili, muda halisi unautengeneza wewe. Na kitu halisi unachokitengeneza wewe unaweza kukimiliki. Ukiutengeneza muda wako una uwezo wa kuumiliki.

NJIA TATU ZA KUTUMIA MUDA WAKO.
Kila mtu anaweza kuangukia katika moja ya njia hizi.

1. Kufikiri 2. Mazungumzo / kupiga stori. 
Mfano; ukiwa peke yako na hufanyi kitu chochote lazima kuna vitu vitakuwa vinaendelea ndani yako, unafikiri / unasemezana na nafsi yako; hapo utakuwa unatumia muda.

3. Vitendo / kitendo.
Namna ya kutumia muda imekuwa tatizo sana, tunatumia vibaya rasilimali ya muda. Ni bora kutengeneza muda wako kwa sababu muda wa saa huwezi kuukimbiza, ukipita umepita (clock time). Swali la kujiuliza; je! tangu umeamka umefanya nini au sasa hivi unaposoma ujumbe huu unafikiria nini?
Mafanikio yako katika kitu chochote yanategemea unatumiaje muda wako katika mambo hayo matatu. Zingatia; chochote unachokifanya au unachokitenda lazima kikunufaishe wewe na huko ndiko kutumia muda kwa faida.
Katika kufikiri kuna vitu vizuri vinapita kwenye akili, hivyo basi ni lazima unapokuwa mahali popote hakikisha unakuwa na kijitabu ili uweze kuandika kila wazo linalokujia akilini. Tumia muda wako mwingi kwa kufikiri _ positively. Usipoteze muda wako kwa mazungumzo ambayo hayakuletei faida kwa sababu yatakuwa yanakupotezea muda bila mafanikio.

DONDOO KUMI (10) KATIKA KUKUWEZESHA KUTUMIA MUDA WAKO.

Lazima utambue thamani ya muda ambao unaishi duniani. Kama hautafika mahali ukawa mjeuri hakika utapoteza muda wako. Ukiwa na nidhamu ya muda watu wengi watakuona wewe ni mjeuri kwa sababu utakuwa kinyume na ratiba zao. Mfano ratiba yako inaonyesha muda fulani utakuwa mahali fulani ukifanya jambo fulani, halafu muda huo mtu anakupigia simu eti muende kwenye harusi, sasa ukimuambia sitaweza kwenda kwa sababu nina kazi ni rahisi sana akakuona wewe ni mjeuri tena unaringa.

1. Hakikisha unaandika Ratiba ya Matukio / Vitu / mambo unayoenda kufanya.
Pangia vitu vyako ratiba ya siku. Tanguliza kile ambacho kinakuletea faida. Kabla hujaamka lazima ujue utafanya nini. Fahamu ratiba yako ya siku utafanya nini au kama huwezi ya siku panga ya wiki.

2. Shughuli yeyote / mazungumzo ya maana katika kukuletea mafanikio lazima uyapangie muda, utaanza saa ngapi na utamaliza saa ngapi.
Kitu chochote ambacho ni cha maana katika maisha yako lazima ukipangie muda.

3. Panga kutumia angalau asilimia hamsini 50% ya muda wako katika mawazo au shughuli zenye matokeo ya kukunufaisha wewe. Mfano; naweza kutumia muda wa kufikiria jinsi gani naweza kuiboresha kazi / shughuli ninayoifanya ili iweze kuwa na utofauti na za wengine. Hii itakusaidia kuboresha kile ulicho nacho na mafanikio yake huwa makubwa sana. Lazima utoboze. (Creativity)

4. Angalau tenga dakika 30. za kupanga ratiba yako ya siku.
Ni marufuku kuanza siku yako kama hujaandaa ratiba ya siku inayofuata.

5. Usione aibu kumwambia mtu, samahani sitaweza kuja au usije nina kazi au usinisumbue nina kazi.
Ukiishi kwa kuwafurahisha watu, mwisho wa siku utaumia (itakula kwako). Na huu sio ujeuri m'baya au kiburi au tabia mbaya, hapana ni NIDHAMU. Nidhamu ya muda ni kanuni ya maisha na kufanikiwa (hapa nimeongezea)

6. Jizoeze kutokujibu sms au kupokea simu kwa sababu tu unataka kupokea au kujibu.
Panga muda maalum wa kujibu sms au kupokea simu.

7. Wakati mwingine unaweza ku-block social networks mfano facebook, twitter n.k. kama unaweza, lengo ni kutumia muda kwa manufaa. Hebu jaribu kufikiria miaka kumi nyuma, halafu angalia umefanya nini katika hiyo miaka kumi? halafu fikiria miaka kumi ijayo utakuwa umefanya nini?


mdee junior (mwanaharakati).
   Ki-ukweli baada ya Harris Kapiga kuuliza swali hili, nilitulia kama dakika moja hivi nikafikiria miaka kumi iliyopita; huwezi amini ilinilazimu nijikaze kuzuia machozi yasitoke kwa sababu nilijiona nimepoteza muda mwingi sana halafu hakuna cha maana nilichokifanya ambacho naweza kukionyesha kwa watu.
NB. Siku 21 zinatosha kabisa kubadilisha tabia.

8. Kabla hujapiga simu yeyote jiulize:
a> unataka kupata nini katika simu hiyo, kama ina mantiki na inakunufaisha, piga. Ukitumia muda vizuri kutakuletea maendeleo. Piga simu zenye tija au sms zenye tija.

9. Tenga muda wa kuchat na kupiga simu unazotaka kupiga.
Hakikisha huo muda ulioupanga ukiisha hama hapo ondoka anza kitu kingine kulingana na jinsi ulivyopanga.

10. Wakati mwingine huwezi kumaliza kila kitu lakini hakikisha basi mawazo / mazungumzo yako yanakunufaisha / yanakufaidisha asilimia themanini 80%.

Harris Kapiga ni Mc. na ni Mchungaji kiongozi katika huduma ya NCHI YA AHADI.; pia ni mtangazaji wa kipindi cha Gospel Tracks na Temino, Clouds Fm Radio.

Kama umebarikiwa au unataka kufika nchi ya ahadi unakaribishwa na semina hizi zinafanyika kila siku ya jumapili kuanzia saa tisa alasiri.
Mungu akubariki kwa kushiriki pamoja nami baraka hizi. Ukifanyia kazi hiki ulichojifunza, hakika UTATOBOZA TU! FIKA NCHI YA AHADI UPATE MENGI ZAIDI.

KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 


HJ



Mawasiliano:

+255 659 700 002
+255 756 145 417

mdeejunior@gmail.com
mdee.junior (skype)
@mdee_junior (twitter)

Dream Big As You Grow Big.




KUKUA KIROHO (SPIRITUAL LEVELS) NA SAM SASALI a.k.a Papaa NDANI YA NCHI YA AHADI JUMAPILI YA LEO.

Ze blogger Sam Sasali, Papaa leo alishusha nondo za ukweli kama sio misumari ndani ya huduma ya Nchi Ya Ahadi iliyo chini ya mchungaji kiongozi Harris Kapiga, Sinza Kamanyola; Dsm.

Andiko lililokuwa limebeba ujumbe mzima lilitoka kwenye kitabu cha Wagalatia 4:1...
''Mrithi awapo mtoto hana tofauti na mtumwa ingawa ni bwana wa wote''. Atakuwa chini ya uangalizi mpaka wakati ulioamriwa na baba (Mungu).
* Ishu hapa sio kwamba urithi haupo la hasha ila ishu ni kwamba Mrithi ni mtoto na mrithi akiwa mtoto ni sawa sawa na mtumwa.
* Tatizo sio kwamba Mungu hajatupa ahadi bali tatizo ni level / viwango katika kuiendea ahadi.
* Kila mtu anapewa kulingana na level aliyo nayo.

1Sam 17:16-17.  Kuomba vibaya sio yale maneno unayoongea mbele za Mungu bali NIA uliyo nayo juu ya kile unachoomba kwa Mungu.
* Unapokaa vizuri na Mungu hata level yako ya kukua inaongezeka.
* Hatumjui Kristo kwa kuimba mapambio.
* Shetani hana haja/agenda na mimi au wewe bali ana agenda na kile ulicho nacho / kile kilicho nyuma yako ambacho kinaweza kukupeleka level nyingine.
* Shetani hakuwa na agenda na Adamu au Eva bali kile walichokuwa nacho; alilenga kile walichokibeba. Adamu alipewa agizo asile tunda hivyo agenda ya shetani ilikuwa ni lile agizo alililopewa Adamu na Mungu.
* Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea, kilichopotea hapa sio mtu bali ushirika kati ya mtu na Mungu (fellowship).

MAENEO YA KUONGEZA LEVEL / VIWANGO.

Mfalme yule alitoa talanta kwa kila mjoli wake kulingana na level / uwezo wa kila mtu.
Ugomvi wa Mungu na mwanadamu ni UTII / OBEDIENCE.

1. Kulifahamu / kulisikia na kulijua Neno la Mungu.
Mungu huzungumza kupitia Neno lake.
Level au uwezo ulio nao lazima utofautiane na yule anayeokoka leo. Kila mtu anakua (growth) kutokana na level aliyo nayo.

* Yesu anapotoa mwaliko ''njooni kwangu nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha'' Swali linakuja, je! nini kinafuata baada ya kupumzika?
Hahahhaaa ts funny, Baada ya kupumzika unakuwa umepata nguvu mpya za kukuwezesha kubeba mizigo yako uliyo nayo na kuendelea na safari yako kwani utakuwa na nguvu za kubeba hiyo mizigo/ jaribu ulilo nalo mara baada ya kupumzishwa na kujifunza miguuni kwa Yesu jinsi ya kuendelea na safari. Maana asema hivi; mjifunze kwangu, hivyo kuna shule ya kujifunza hapo kwa sababu Yesu hajasema njooni mniachie mizigo yenu bali njooni niwapumzishe then mwendelee na safari yenu.
* Ukristo ni mchakato endelevu. / Continuous Process. Lazima tukue katika kulisoma Neno la Mungu.

2. Maombi (sio maombezi).
* Watu wengi wanaopenda maombezi hawana Neno ndani yao. Mtu mwenye Neno / aliyejaa Neno ana maneno mengi ya kumwambia Mungu kwa sababu anazijua haki zake za msingi.
* Haijalishi ni watu wangapi watakuelewa katika kile unachokifanya / unachokisema au kile unachokiamini.
* Kuna nyakati lazima Farao akukimbize / akufuatie nyuma ndipo njia itakapopatikana.
* Kuna gharama za kulipa kufika daraja la kwanza (first-class / kiwango cha juu).
* Kuna wakati hakuna mtu wa kukubeba / kukusaidia, ni lazima ujitie nguvu mwenyewe. (David strengthened himself in the Lord).

3. Mtazamo (perception).

* Kile ambacho unakitazama / unakiona kwenye ubongo wako ndicho utakachokimiliki. Yesu hakumuona mariamu kama kahaba bali chombo chake. Akionacho Yesu lazima na sisi tukione.

Papaa Ze Blogger alimalizia kwa kusema hivi:
SIO KILA MKRISTO ANA VITA, BALI MWENYE KITU NDIE MWENYE VITA. I like this.


mdee junior na sam sasali papaa.



             










Born to praise team.















Mungu akubariki, Karibu NCHI YA AHADI.

Mawasiliano:


+255 659 700 002
+255 756 145 417

mdeejunior@gmail.com
mdee.junior (skype)
@mdee_junior (twitter)

Dream Big As You Grow Big.


Juu