JOHN SHABANI TOUR TO VISIT NGORONGORO CRATER
-
The *Ngorongoro Conservation Area* is a protected area and a World
Heritage Site located 180 km (110 mi) west of Arusha in the Crater Highlands
area of...
HABARI MPYA
FUNDISHO LA MSINGI
PICHA NA MATUKIO
CAPACITY BUILDING CLASS
MAHUSIANO
NUKUU YA LEO
RIWAYA : JINAMIZI LA MABINTI
Imewekwa na: Mdee Junior Tarehe: 8:39:00 PM / maoni : 0 Riwaya / Hadithi
MTUNZI: ELIA MWAIPOPO
SEHEMU YA 1
KWA WASOMAJI WAPYA
Hadithi hii ni ya kubuni tu, lakini yenye kueleza uhalisi wa maisha na mambo yafanyikayo hasa kwenye ulimwengu wa roho (spiritual realm) na ule ulimwengu wa damu na nyama (physical realm), majina yaliyotumika hayana uhusiano wowote na watu wenye majina kama hayo …
Jinamizi lisilojulikana kwa kipindi kirefu, limeendelea kuwakumba mabinti wengi vigori kwa njia za kishirikina pasipo wao kujitambua. Mabinti hao licha ya kuwa na mvuto mkubwa mbele ya vijana watanashati wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuziteka hisia zao na kujikuta wakishawishika na kujiingiza katika mahusiano ambayo yanahatarisha maisha ya vijana hao kwa muda mrefu. Usiri mkubwa unatawala katika vifo hivyo vya kusikitisha hali inayopelekea kuibuka kwa hofu kubwa katika jamii….Hadithi inaanzia kwa msichana Monica, usiku wa manane huku akiwa kitandani anashituka na kuanza kushuhudia maruweruwe mengi, kwa taharuki kubwa anaamkaa na ……ENDELEA
******************************
Yapata majira ya saa nane za usiku, Monica anashituka ghafla akitokea usingizini alikokuwa amelala na kuanza kuona matukio ya ajabu machoni mwake, ghafla anahisi nywele zikimsisimka na kuanza kutetemeka, haukupita muda kijasho chembamba kinaanza kumtiririka usoni kwake hali iliyoambatana na hofu kubwa inayoyabadili kwa kiasi kikubwa mapigo ya moyo wake na kuyafanya yawe na kasi zaidi.
******************************
Huku haya yakiendelea Monica anahisi kupata hisia juu ya kile kilichokuwa kikiendelea lakini asijue nini cha kufanya. Anachungulia dirishani huko nako anapokewa na kiza totoro kilichosheheni weusi mithili ya mkaa. Taharuki inazidi kuukumba moyo wa Monica pale anapohisi joto na baridi vikiongezeka mwilini mwake kwa pamoja.
******************************
Zinapita dakika kumi na tano huku akiwa ameduwaa anajaribu kujitafutia msaada kwa kupiga yowe kubwa ambalo linakuwa halina maana yoyote kwani halikuwa likisikika na mtu yeyote aliyekuwa karibu na chumba chake. Kufumba na kufumbua macho Monica anajikuta yuko ndani ya kifuu mithili ya kile cha nazi kwa udogo na na taratibu anapaa kuelekea asikokujua huku joka kubwa likiwa limezunguka kingo za kifuu hicho ambacho kwa wakati huo kilikuwa kikipaa taratibu.
******************************
Wakati hayo yakitokea joka lilikuwa likitema moto wa cheche za kijani kuelekea machoni na kuzitisha mboni za Monica binti ambaye alikuwa akisifika kwa uzuri na sifa kem kem. Ndiyo ulikuwa ni msafara mkubwa uliokuwa ukiongozwa na Madubwana ambayo ni maarufu kama Majitu yaliyokuwa na sura za kutisha ambapo yalikuwa na macho matatu na pembe tatu..Juu ya mboni zao Madubwana hayo inasemekana kulikuwa na machipukizi ya viganja mithili ya vile vya binadamu na inasadikika kuwa hali hii ilitokana na mahusiano yao ya hapo zamani yaliyokuwepo baina ya Madubwana hayo na binadamu wa kawaida ambapo inasemekana uhusiano wao uliharibiwa na Madubwana pale yalipoanza kuwakamata na kuwala binadamu.
******************************
Wakati Monica akifikiria namna ya kujinasua akajikuta akipokea amri yenye vitisho ambayo ilimuamuru kutokugeuka wala kupiga kelele “Usigeuke wala kupiga kelele, achama mdomo wako ili tuingie na tujihifadhi kwa miaka ijayo” kisha amri hiyo ikafuatiwa na kicheko cha dharau “aaaaaaahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
******************************
Ilikuwa ni safari ya kuelekea angani liliko anga la kaskazini ambako inasemekana na kuaminika na wengi kuwa huko ndiko viumbe wengi na wa kila aina wenye kustaajabisha walikimbilia huko baada ya mifarakano mikubwa kutokea duniani yakiwemo Madubwana na viongozi wao. Awali, kabla ya Majitu kuja duniani na kumnyakua Monica palikuwa pametokea balaa kubwa sana la njaa hali iliyopelekea Madubwana mengi kupoteza maisha. Inasemekana takribani miaka saba Majitu yalikosa kabisa chakula na maji, mwanzoni katika kutatua tatizo hilo majitu yalianza kukamatana yenyewe na kulana kama chakula na wakati mwingine yalilazimika kukamata madubwana mazee ambayo yalikuwa dhaifu na kuanza kuyala kama chakula. Hali hii ilisababisha majitu kupungua kwa kasi kubwa sana.
******************************
Inaaminika baada ya madubwana mazee kuisha Madubwana yalianza kupunguza sehemu za viungo vyao na kuvifanya kama chakula chao. Mikia yao ambayo ilikuwa imenona mafuta na pembe zilizokuwa kavu mithili kuni zilizokaukia juani kwa kipindi kirefu nazo ziligeuka na kuwa msaada mkubwa sana kwa madubwana hayo. Habaari za taabu na kutaabika kwa majitu hayo zilimfikia kiongozi wao ambaye kwa wakati huo wala hakuwa na habari juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwani yasemekana ilipokuwa ikikaribia majira ya kipindi cha joto Kiongozi huyo maarufu kwa jina la Iisambo alishuka duniani na kuyaendeleza maisha yake yaliyoshabihiana kwa karibu kabisa na majini walioko duniani. Tofauti yao ilikuwa wakati majini walioko duniani walikuwa wakiishi kwa kunyonya damu binadamu na viumbe wengine, Irisambo aliishi kwa kutegemea nyama za binadamu na viumbe waliokuwa wakiishi katika dunia ya tatu.
Kwa kuwa hali ilikuwa ni tete katika anga hilo la kaskazini Irisambo siku moja aliitisha kikao kilichodumu kwa takribani masaa kumi na mbili akitafakari kwa kina kiini cha matatizo yake na suluhisho la matatizo yaliyokuwa yakiwakabiri madubwana hayo. Katika kutafuta suluhisho hilo akaja na mbinu ambazo kwa fikra za kijitu Irisambo aliona ni njia mbadala wa kutatua tatizo hilo………..ITAENDELEA
******************************
******************************
SHARE &COMMENT
ITAENDELEA JUMATANO 24/07/2013
UZINDUZI WA ALBAM YA ''AMANI YA BWANA'' YA RUNGU LA YESU KWA UDHAMINI MKUBWA WA KAMPUNI YA HALISTA ENTERPRISES.
Imewekwa na: Mdee Junior Tarehe: 12:57:00 PM / maoni : 0 Picha Na Matukio
UZINDUZI
HUU UNAKUJIA KWA UDHAMINI MKUUUBWAAA KABISA WA KAMPUNI YA HALISTA
ENTERPRISES WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI WA MAFUTA HALISI YA KUPIKIA YA
ALIZETI KUTOKA SINGIDA.
NUNUA MAFUTA HALISI YASIYOCHAKACHULIWA.
MAFUTA HAYA YATAKUWEPO SIKU YA UZINDUZI NA YATAUZWA KWA BEI NZURI
KABISA ( REASONABLE PRICE ), USIKOSE KUJA NA PESA UJIPATIE MAFUTA HALISI
YA ALIZETI katika ujazo wa Lita 1 Na Lita 5.
Mkurugenzi wa kampuni ya Halista Enterprises atakuwepo na atazungumza!
Ukitaka kujua bei za Mafuta tembelea http://halisitz.blogspot.com/ AU Tupigie 0659 700 002
ANANIA MWASOMOLA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA AJA NA KWAITO STYLE.
Imewekwa na: Mdee Junior Tarehe: 3:50:00 PM / maoni : 0 Picha Na Matukio
Anania Mwasomola azungumza na Blog hii. Mwandishi na mmiliki wa Blog hii alikuwa na machache ya kumuuliza kuhusu huduma yake ya uimbaji.
Blogger: Kijana mbona uko kimya sana, vipi uko wapi?
Anania: Niko Mbeya, nina mikutano kadhaa ya Injili. Nataraji kuja Dar mwanzoni mwa mwezi wa nane 2013.
Blogger: Wapenzi na washabiki wako watarajie nini baada ya ukimya huu?
Anania: Washabiki wangu watarajie mambo mazuri. Nakuja tena kwenye kazi ya Mungu na albamu ya pili.
Ni kitambo sija toa nyimbo mpya tangu nilipo achia albamu ya WEWE NI BABA ambapo hadi sasa video yake imekamilika na mwezi wa nane itakuwa sokoni. Wakati huo huo albmu yangu mpya ambayo jina nimelihifadhi nitaliweka wazi nikikamilisha kazi ila kwa wale wapenzi wa nyimbo za taratibu,wajiandae kupokea, Mungu kanipa nyimbo ya taratibu moja naamini itawagusa wengi sana kwa neema ya Mungu.
Blogger: Umesema kwenye albam mpya kuna wimbo mmoja wa taratibu, zilizobaki zipo kwa style ipi?
Anania: Nimetumia kwaito style kwenye nyimbo zangu naamini zitawabariki sana, nawapenda wapenzi wangu kama wanavyonipenda.
Blogger: Kwa nini umeamua kuja na kwaito.
Anania: Ooh kwaito naipenda sana kwani haiko kikwaya zaidi kitu ambacho inawafanya watu wamataifa (wasiomjua Mungu) waweze kusikiliza na ni rahisi kuwapata na wakaja kwa Yesu.
Kiukweli waimbaji wa gospel tunapenda kuigana kitaifa sio kimataifa so mimi nakaa kimataifa zaidi.
Anania Mwasomola aliendelea kufunguka zaidi kwa kuwatolea mifano baadhi ya waimbaji anaowakubali.
Mfano ni dada Christina Shusho, wabongo wengi hawa mwelewi anaimba nini, lakini ukienda mataifa ya nje Shusho anajulikana kuliko unao wajua hapa bongo, hii nimeona kwa nchi nilizo tembelea hapa africa.Wanampenda sana Shusho naamini nitafikia viwango vyake na kuzidi.
Pia John Lisu wabongo hawa mwelewi kabisa ila kiukweli ndo mwimbaji wangu sana na mwansasu wana uwezo wa kuimba live muda wowote.
Mwisho. Naomba wapenzi na mashabiki wangu wakae tayari kupokea kitu kipya kutoka kwenye albamu mpya (AUDIO)
Blogger: Mungu akuzidishe kama mchanga wa baharini.
TUMA MAONI YAKO.
Subscribe to:
Comments (Atom)
KUWA WAKALA WA BIDHAA ZA KII AFRICA
Mtu yeyote anaruhusiwa kuwa Wakala wa uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa na KII AFRICA (T). Wakala wa kawaida atauziwa kwa bei ya punguzo, Wakala ambaye ni mwanachama wa Kii Africa atauziwa kwa bei ya uanachama ambayo ni ya chini zaidi. Jiunge na Kii Africa uwe mwanachama Upate punguzo zaidi. Wasiliana nasi: 0653 100 100
iBooks
- Maarufu
- Maktaba
- Vipengele
Library | Maktaba
- Apr 06 (1)
- Sep 11 (1)
- Aug 14 (1)
- Sep 01 (1)
- Aug 30 (1)
- Sep 23 (1)
- Sep 07 (1)
- Apr 23 (1)
- Apr 20 (1)
- Apr 16 (1)
- Mar 03 (1)
- Nov 13 (1)
- Oct 01 (1)
- May 26 (1)
- May 15 (1)
- May 09 (1)
- Apr 18 (1)
- Apr 10 (3)
- Mar 15 (1)
- Mar 08 (1)
- Feb 26 (1)
- Feb 03 (1)
- Nov 26 (1)
- Oct 21 (3)
- Oct 06 (1)
- Oct 04 (1)
- Sep 26 (1)
- Sep 23 (1)
- Sep 20 (1)
- Sep 16 (1)
- Sep 04 (1)
- Sep 03 (1)
- Sep 01 (1)
- Aug 31 (1)
- Aug 16 (1)
- Aug 13 (1)
- Aug 06 (1)
- Aug 05 (1)
- Aug 03 (1)
- Jul 30 (1)
- Jul 23 (2)
- Jul 22 (1)
- Jul 21 (1)
- Jul 20 (1)
- Jul 16 (1)
- Jul 07 (1)
- Jul 05 (1)
- Jun 27 (1)
- Jun 25 (1)
- Jun 21 (1)
- Jun 16 (1)
- Jun 13 (2)
- Jun 07 (1)
- Jun 05 (1)
- Jun 04 (1)
- May 27 (1)
- May 24 (1)
- May 12 (1)
- May 09 (1)
- Apr 22 (1)
- Apr 20 (1)
- Apr 19 (1)
- Apr 17 (1)
- Apr 11 (1)
- Apr 10 (1)
- Apr 08 (1)
- Apr 07 (1)
- Apr 05 (2)
- Apr 03 (1)
- Mar 29 (1)
- Mar 26 (2)
- Mar 25 (2)
- Mar 19 (1)
- Mar 17 (1)
- Mar 13 (1)
- Mar 05 (1)
- Mar 04 (1)
- Feb 20 (1)
- Feb 19 (1)
- Feb 14 (1)
- Feb 12 (1)
- Feb 10 (1)
- Feb 04 (1)
- Feb 03 (1)
- Jan 30 (1)
- Jan 21 (1)
- Jan 18 (1)
- Jan 14 (1)
- Jan 10 (2)
- Jan 09 (1)
- Jan 08 (1)
- Jan 03 (1)
- Dec 30 (1)
- Dec 12 (1)
- Nov 27 (1)
- Nov 25 (1)
- Nov 24 (1)
- Nov 21 (1)
- Nov 20 (2)
- Nov 19 (1)
- Nov 17 (1)
- Nov 16 (1)
- Nov 15 (1)
- Nov 13 (1)
- Nov 09 (2)
- Nov 07 (1)
- Nov 05 (1)
- Nov 04 (2)
- Nov 03 (1)
WADAU
YALIYOMO
BENEFITS OF SUNFLOWER OIL
Capacity Building Class.
EVENTS
FamareX Products & Co.
Fundisho La Msingi
Habari mpya
HARAKATI ZA BLOG
JICHO LA TOFAUTI
KIOO CHA BLOG
KONA YA WATUMISHI
LAWS OF SUCCESS
MAHUSIANO
MATANGAZO
NUKUU YA LEO
Picha Na Matukio
RADIO
Results 4M4-2014
Riwaya / Hadithi
Speak Up For Orphans
WIMBO WA BLOG
MC LAWRENT MWANTIMWA
KINAPATIKANA MADUKANI
KAMA UNAHITAJI COPY YAKO, TUPIGIE: 0767 228 061 / 0715 228 061
KARIBUNI
UNATENGENEZA: LOGO, CD Cover, STICKER, BUSINESS & ID CARD, MATANGAZO... N.K.
Total Pageviews
KII AFRICA (T).
MITANDAO MINGINE
-
-
JANETH LUSHINGE SALAMA ROHONI MWANGU - Ambatana nasi kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi. www.facebook.com/gospelkitaa
-
HIVI NDIVYO RAIS MAGUFULI ANAVYO PENDWA NNCHINI KENYA...MASHABIKI WA VILABU KENYA WATENGENEZA TAWI LA MAGUFULI - [image: https://4.bp.blogspot.com/-POin-ICpMzk/Vxycbod3M9I/AAAAAAAA-ow/5_NzoDtRh4owGE8mr3leX16dBvvT8cwOACLcB/s640/13043528_976655849080443_90653603117684311...
-
-



