Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

JINSI GANI MTANZANIA ANAWEZA KUJIAJIRI - BENSON MAHENYA AZUNGUMZA NA VIJANA NDANI YA CHIMBO ''SCHOOL OF THOUGHT''






Benson Mahenya: Mmiliki wa Kampuni ya BM PUBLISHERS wachapishaji wa Gazeti La ''Afya Tabibu''











Alianza kwa kusema hivi: 

Ipo kauli isemayo kuwa ''Furaha ya mtu hujitengenezea mwenyewe'' hivyo kufikiri, kuona na kufanya ulichozaliwa nacho ni furaha kubwa sana. Inawezekana tafakuri na fikra zako umetumia muda mwingi na mlango huo uuonao bado ni mlango ambao huoni mpenyo wa kupita lakini ukiuamini na kuchukua hatua kuingia ndani hakika ipo milango mingine saba wazi inakusubiri. Daima elewa kuwa kungoja kwako kunaufanya mlango huo wa kupitia kufungwa. Ili uweze kufika sehemu fulani lazima ukutane na mtu sahihi kwani msaada wako utapatikana pale utakapochukua hatua ya kuanza. Daima mabadiliko huja baada ya kuanza.

Dondoo Muhimu.
kuanza...
kila kitu kilianza...
dunia imekuwako kwa kuanza...
mimi na wewe tuna mwanzo...

Hakika mwanzo tufe ni mvutano.

 MTAZAMO WA BIASHARA TANZANIA.

Mtazamo ni kitendo cha kulielewa jambo na kuuona mwelekeo wake katika ufahamu wa taarifa zake. Pia tunaweza kusema kuwa ni ujenzi wa mawazo juu ya jambo, tukio ama kitu halisi kilichopo au kilichopo katika ulimwengu bwete (kifikra). Hivyo mawazo yako au mtazamo wako juu ya jambo fulani daima haulingani na mtu mwingine.
Amua maisha yako mwenyewe pasipo kusubiri mtu akuamulie. 
Kwa mfano mimi mwenyewe (Benson Mahenya) nilipotaka kujiajiri nilipata vipingamizi sana na kipingamizi kikuu kilikuwa ni familia yangu ikizingatiwa ni kijana wa kwanza kati ya watoto kumi na sita yenye baba mmoja lakini mama tofauti tofauti. Hivyo mshahara wangu wa kwanza na mingine nilikuwa naituma nyumbani kusaidia ndugu zangu nikifikiri kuwa itakuwa suluhisho la matatizo yaliyowakabili ndugu zangu, lakini kumbe ndivyo nilivyozidi kuchelewa kufikisha ndoto zangu. Lakini nilipotambua kuwa yanipasa nijikwamue kwanza mimi kisha wao (ndugu). Niliwekeza katika ndoto zangu hakika sasa nimewaajiri ndugu zangu.

Kwa mtazamo wa kibiashara nchini ni vema kuweza kujua msingi wa mtazamo ambao ni Biashara. Pasipo kujua msingi wa biashara ni vigumu pia kuelewa fursa zake katika kuzifanyia kazi.

Awali ya yote tujue dhana fafanuzi ya neno biashara.
Zipo fasiri nyingi juu ya neno biashara zikiwemo;
Biashara ni kitendo cha kuuza na kununua bidhaa na huduma kulenga faida. Hii ina maana kuwa biashara yoyote lazima ilete faida ama ilenge kuleta faida. 
Unapojihusisha na biashara weka msingi mzuri wenye tija na manufaa utakaokuingizia faida.

Ujasiriamali kwa sasa ndilo neno lenye kusikika masikioni mwa watu wengi sana kwa sasa.
* Ujasiriamali ni shughuli endelevu kupata faida.
* Fasiri nyingine ni kwamba, ni kuona fursa na kuitumia.
* Ni kuona fursa, kuifuata kwa ujasiri na kuitekeleza.
Kuonekana ni neno lisilosikika tena bali ni vitu viwili vyenye mwingiliano mmoja _ UJASIRIAMALI.

VITU VYA MSINGI KATIKA KUFANYA UJASIRIAMALI NA BIASHARA.

Yajue malengo yako:
Katika ujasiriamali na biashara kwa ujumla ni vema kutambua malengo yako. Pasipo kutambua malengo ni kikwazo cha mafanikio na kusonga mbele kwa biashara.
Malengo huwekwa na mhusika mwenyewe wa biashara ama mjasiriamali. Ukiwa mjasiriamali malengo yako ni lazima yatazame kufanikisha kupatikana pesa.

Katika suala la biashara na ujasiriamali pesa ni suala muhimu kwani laweza kusimama na kuchangia kwa sehemu kubwa.
Kuhusiana na suala la pesa ni vyema ukajua malengo yako na kutaka uzifanyie nini. Katika kulenga pesa elewa utazitumia kwa ajili gani na matumizi yapi yatafanyika kukupeleka mbele au kusonga na kupiga hatua zaidi.

Unapolenga pesa katika kuzihitaji usiiangalie pesa bali kufikia malengo yako. Mfano kusomesha watoto, kupanua mradi wako.
Ukiwa mfanyabiashara mwenye mtazamo wa kusonga mbele hakikisha biashara yako inakupa faida. Boresha biashara yako upate faida kubwa. Ubunifu wenye ubora utakupa faida yenye manufaa katika biashara yako. Jenga tabia ya kufanya marekebisho yenye kuboresha biashara yako ili uwe na soko la uhakika.

Faida yaweza kuwa kubwa au kuwa nzuri kukufanikisha haraka na muda mwingine yaweza kuwa ndogo ikakufanikisha pia. Biashara yenye faida wakati mwingine yaweza kuanza pasipo faida ila itategemea uendeshwaji wake ikatoa faida na kujengeka vyema.

Mfano:
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 siku moja katika sherehe za maonesho ya saba saba mkoani Dar es salaam, katika ufunguzi wa maonesho hayo kulikuwa na mabanda ya ujasiriamali mbalimbali likiwemo na banda la ndugu Reginald Mengi ambalo lilikuwa ni banda lililotembelewa na rais wa awamu ya kwanza hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo mwalimu alikutana na biashara ya maji ambayo yalikuwa yanauzwa hakika alishangazwa mno, unajua kwa nini? Wakati ule maji ya kunywa katika chupa hayakuwa na soko Tanzania kama wakati huu. Hivyo, hata faida yake haikuwa kubwa lakini hakukata tamaa hadi leo hii anaendelea.

Hivyo katika biashara suala la faida yawezekana kabisa biashara yako unapata faida ndogo usihofu maana yawezekana kabisa kesho Taifa litakutegemea kupitia hiyo biashara yako. Kataa kabisa kukata tamaa bali bidii iwe ndio msingi wa mambo yako. Ni vyema ukaitazama biashara yako kwa mtazamo wa kijasiriamali.

UJASIRIAMALI NI NINI?  Suala la biashara kupata faida ni muhimu kulitazama katika muonekano wa ujasiriamali.

Katika suala la faida si bei kubwa ndio itakupa faida bali biashara yenye mzunguko ndio itakuingizia faida.
Watu wengi wameanzisha biashara nyingi sana na nzuri lakini kukosa walengwa wa faida imesababisha biashara zao kutoendelea.
Katika mtazamo huu wa faida haikatazwi kuuza vitu vya bei ya juu bali lenga vyema faida itakayokupa mzunguko wa biashara yako.

   Kwa upande wa huduma pia, faida itazamwe vyema kwa mfano:
   Kuna huduma nyingi sana zina faida sana lakini jinsi ya kulenga kupata faida huduma hizo zimesababisha kuzorota na kutoendelea kabisa. Mfano... ''Kuna vituo fulani vya afya katika tafiti ambazo niliwahi kufanya eneo fulani kila hatua mgonjwa anayopita kutibiwa anatozwa hela. Kuandikisha majina unalipia fomu, kuonana na daktari unalipia hela, kuchukua vipimo unalipia hela, tena ni maeneo ya watu wa hali ya chini kabisa wakiwa ni wakulima pekee. Hii ilipelekea wateja kukosekana kwani faida ililengwa zaidi.
Kwa ushauri wangu (Benson Mahenya) faida ni vema iwepo lakini itakayokuza biashara. Mara nyingi unapoanza biashara anza na gharama yenye kulenga faida kidogo. Ikijulikana gharama yaweza kupanda kidogo.

Suala la faida katika biashara ni vema litazamwe vyema kwani laweza kukuza biashara ama kuiangusha. Ni vema faida ikapewa kipaumbele cha kuboreshea mazingira ya biashara ili iweze kukua.

ZINGATIA HAYA JUU YA PESA ZAKO.
> Katika suala la pesa na malengo yako, jitahidi kuiheshimu pesa ya biashara au jaribu kuitofautisha kabisa 
   na pesa ya matumizi hasa starehe.
> Usiingie mkopo hela ya biashara kununua vipodozi, kustarehe na kufanyia anasa.
   Tafuta chanzo kingine cha pesa kufanyia hivyo si biashara kwani mkopo utakugharimu.
> Pesa ya biashara iwe ndio msingi wa hatua nyingine ya kukutangaza kwenye soko. Jinsi utakavyoiheshimu,
   itakuheshimu na kukupa heshima, wengine hudai pesa yaweza kukukalisha na yeyote na kusikilizwa na
   yeyote.

> Pesa ni sabuni ya roho, yaweza kuleta kicheko japo simanzi imewazunguka wengi.
> Jitahidi kutunza/kuwekeza zaidi kuliko kutumia. Matumizi yako yasizidi kipato chako.
> Usidharau pesa ndogo kwani ndio iletayo pesa kubwa na nyingi.
> Punguza matumizi yasiyo ya lazima kwenye mzunguko wako, mfano:

* Sio kila kitu cha kununua na kula
* Zima taa ukimaliza shughuli zako nyumbani
* Zima vifaa vyote vinavyotumia umeme ofisini kwako.
* Usiendeshe gari unaongea na simu kwani waweza pata ajali ikakupa matumizi mengine.
* Zingatia usalama barabarani kuepuka kupigwa faini, mfano kuendesha gari kwa kasi, kuendesha kwa
   uzembe na kuchelewa kuamka.
* Punguza safari za kusalimia kila mtu kwani waweza pata matumizi usiyotarajia, mfano: kuchangia
   chakula kwa kuwanunulia rafiki zake mpenzi wako kwa kutokupanga (kuhonga ili kuficha aibu)
> Pesa yako ya biashara isikufanye ukaidharau ndoa yako hasa kwa wana ndoa waliofanikiwa kwa 
   kuanzia hali duni. Mmoja akifanikiwa iwe ni biashara sio kumnyanyasa mwingine. Waweza sababisha
   talaka itakayowatesa watoto.

*************************************************************************

Tuwasiliane kwa:
0659 700 002
halisitz@gmail.com


MWISHO: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 




  


TOFAUTI ZA KIJINSIA NA JINSI ZINAVYOATHIRI MAHUSIANO YETU_Chris Mauki





Mwanasaikolojia Chris Mauki azungumza ndani ya Nchi Ya Ahadi jinsi tofauti za kijinsia zinavyoweza kuathiri mahusiano yetu.



 
 Ni vema ukifahamu, Tunavutiwa na vitu tofauti 
Inawezekana sana mwanaume kwa jinsi alivyoumbwa akakupenda siku ya kwanza kwa mengi yale yaliyo nje yako, yeye anajua nini kimemvutia kwako na taratibu mkikubaliana kupendana ndio anaanza kugundua na kuvumbua vilivyofichwa ndani yako na hivyo ndivyo vinamfanya aidha kukukimbia au kugandana na wewe.
Lakini ni vema sana wanaume kujua kuwa siku ya kwanza mwanamke anakuona anavutiwa zaidi na “qualities” zilizoko ndani yako, sio sana vile vilivyoko nje yako. Kwahiyo ongeza juhudi katika kujenga vilivyo ndani yako kwasababu vinamashiko sana katika mahusiano yako kuliko kupoteza muda kujenga vilivyo nje yako wakati havina tija. Ni sawasawa na kutumia nguvu ngingi kutengeneza mtego wa kunasa nguruwe pori huku ukiwa na nia ya kwenda kutega kware.
Siku zote dhana ya mahusiano inaweza kuwa na namna mbili tofauti kutokana na tofauti za jinsia zetu wenyewe. Lakini kwanza tujiulize nini maana ya MAHUSIANO?

Mahusiano_ Ni ujenzi wa uhusiano wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke unaohusisha sana hisia.

TUNAWEZA KUYAGAWANYA MAHUSIANO KATIKA MAKUNDI MANNE.

1> Kundi la watu walio katika mahusiano ya urafiki hadi uchumba.
2> Kundi la watu wanaoanza kujiunga/kujiingiza kwenye mahusiano.
3> Kundi la watu ambao tayari wako kwenye ndoa.
4> Kundi la watu ambao hawajajiingiza kwenye mahusiano kabisa.

TOFAUTI ZA KIJINSIA.

Mara nyingi kunaweza kuwa na tofauti mbalimbali kutokana na utofauti wa kijinsia unaotokana na chanzo au vyanzo mbalimbali vinavyoleta tofauti ambayo inatokana na Asili Yetu.
Asili yetu ni pale mmoja asemapo ''mimi ni mwanaume, yeye ni mwanamke''

VYANZO VYA TOFAUTI HIZI.

a) Malezi. 
Mara nyingi malezi ndiyo yanayoweza kuonyesha tabia asilia ambayo anayo mtu kulingana na jinsia yake. Wazazi ndio nyenzo kuu ya kumfanikisha mtoto kuwa na malezi bora yenye mtazamo mzuri wa kuwa na mahusiano mazuri kwa wazazi wenyewe na hata kwa jamii inayomzunguka.
Lazima wazazi watumie vyema fursa zao kuwajenga watoto wao katika misingi iliyo thabiti katika maisha yao yote.

b) Makuzi.
Katika hatua ya ukuaji mzazi ndiye amtengenezaye mtoto katika hatua zote za ukuaji wa kimwili na kiroho kutokana na umri wake.

Utafiti alioufanya Chris Mauki.

Katika utafiti wangu ( Chris Mauki), 2012 huko Afrika Ya Kusini imeonyesha kuwa familia nyingi huwa na mzazi mmoja (single parent family) ambapo watoto huwa chini ya uangalizi wa malezi ya mzazi mmoja, hivyo mtoto huathiriwa kisaikolojia zaidi.

Mfumo/aina za familia:
Familia ni mkusanyiko wa watu wenye uhusiano mmoja na kukaa pamoja.

Aina za familia.
-familia yenye mzazi mmoja na watoto (single parent family)
-familia yenye wazazi wawili (nuclear family)
-familia yenye wazazi, watoto na ndugu wengine (extended family)
-familia ambayo haina wazazi (non-parents family)

c) Watu wanaokuzunguka (marafiki).
Huenda marafiki au watu wanaokuzunguka ndio wanaoweza kuwa chanzo cha kuibua utofauti, kwani unaweza kusikia maneno yanayosemwa kwa kujadili mambo ambayo ni sumu kali ya kuibua tatizo katika jamii.

d) Maisha yako ya awali (life background).
Ujionavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo na ndivyo watu watakavyokuona. Maisha yako ya awali yanaweza kukupa swali la kujiuliza; 'jinsi ujionavyo nafsini mwako ndiyo chimbuko la kuibua furaha au huzuni maishani mwako'.

Matatizo ya kimahusiano:
Matatizo siku zote hutokana na namna mtu anavyoweza kujitengenezea mwenyewe.
Lakini matatizo ya kimahusiano watu wengi hushindwa kuyatatua kwa sababu ya kutokujua tofauti zao za kijinsia.

Mifano ya tofauti za kijinsia.
i> Wanawake wengi wameathiriwa na manunuzi (shopping) wakati wanaume hawazingatii sana manunuzi/shopping.

ii> Wanawake wengi hawazingatii sana mpangilio wa muda katika mipango yao. Lakini wanaume wengi huzingatia muda zaidi.

iii> Kwa matumizi ya pesa wanawake hutumia vibaya kuliko wanaume.

Nini tufanye kutatua tatizo?

- Lazima kila mtu aelewe chanzo cha tatizo na kulitatua
- Utayari wa kuchukuliana udhaifu
- Kuendana tabia.

JE! WANAWAKE WANASEMA NINI KWA WANAUME?
Kwa tafiti zilizofanywa nchini, imeonekana kuwa wanaume hawawezi kuelezea hisia zao walizo nazo kwa undani zaidi.

Wanaume pia hawana ukweli katika kuonyesha uhusiano zaidi.

Wanaume wengi wana fikra hasi kwa wanawake.

######################################################################

HAKIKA UHUSIANO BORA HUIBUA FURAHA MAISHA YOTE.


MWISHO: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 








SIKILIZA JICHO LA TOFAUTI HAPA_ Na HARRIS KAPIGA NDANI YA GOSPEL TRACKS YA CLOUDS FM.

Twende sawa sasa, bofya kwenye kitufe cha Play uanze kusikiliza_Ni series tatu.


MUNGU WANGU NA AKUBARIKI KWA KUWA MFUATILIAJI MZURI WA BLOG HII.
ENDELEA  KUFUATILIA UPATE MENGI ZAIDI, PIA USISAHAU KUMSHIRIKISHA NA MWINGINE.

Wasiliana nasi kwa:
0659 700 002
0653 100 100

Barikiwa.

RIWAYA: JINAMIZI LA MABINTI

Unto Jesus every knee shall bow and tongue confess that He's Lord!

MTUNZI: ELIA MWAIPOPO

SEHEMU YA TATU (3)
*********************


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Siku ya saba akashushwa duniani akiwa ni binti tofauti na Yule wa zamani, ambapo
yasemekana uzuri wa macho yake angavu na kidevu kilichochongoka kwa ustadi mkubwa
vilizidi kuwa kivutio kikubwa kwa wasichana wenzake, hali kadhalika wanaume pia ambao
siku zote walikuwa wakitamani kuwa na binti huyo mrembo. Alikuwa ana kiuno cha
mduara kilichobinuka mithili ya kichuguu, ngozi yenye ulaini na unadhifu ulishikamana
sambamba na uasili wa nywele zake. Kwa vijana wengi safari hii alipewa jina la “ Maria
Cleopatra” (mwanamke anayeaminika kuwa ndiye mwanamke aliyewahi kuwa mzuri kuliko
wanawake wote ulimwenguni).
*********************
Kitu kikubwa na cha kushangaza ni kwamba Monica hakuonewa wivu na wasichana
wenzake tu bali hata wavulana pia. Kwa kawaida haikushangaza kusikia minong’ono
kuwa binti huyu alikuwa akijisikia au (kuwa na mapozi) kama wasemavyo vijana wa siku
hizi waliokulia mijini. Kuhusu mwendo wake mara nyingi ulizua taharuki kubwa na
mihemuko ya kihisia kwa vijana makapela na wazee hali iliyohamisha hisia zao huku wengi
wakihisi wapo dimbani wakisakata kabumbu na binti huyo. Utanashati sifa yake kuu kwani
tangu udogo wake hakuwahi kukutwa na matope wala kuvaa nguo kuu kuu, licha ya kuwa
na maisha ya kawaida katika familia ya Mzee Wazza Likuhusulo.
*************
ENDELEA………
Siku moja wakati wa sherehe za Krisimasi na Mwaka Mpya Monica alijumuika na vijana
wenzake katika sehemu moja ya starehe iliyoko karibu kabisa na upwa wa bahari ya hindi;
sehemu hiyo maarufu ndani na nje ya jiji la Dar es salaam ijulikanayo kama Coco beach
imejizolea jina kubwa sana hasa kwa wageni waingiao na kutoka nje ya jiji la Dar es salaam.
Umaarufu wa sehemu hiyo haukuja hivi hivi tu bali inasemekana ni kutokana na matukio ya
kihistoria ambayo yalikuwa yakizunguka na kutokea sehemu hiyo. Tangu ukoloni
inaaminika kuwa Watawala wa kikoloni hasa Wajerumani na Waingereza walipenda
kujumuika na familia zao katika sehemu hiyo ambapo ujio wao pahali hapo palichangia
kiasi kikubwa sana kuipa umaarufu upwa wa fukwe ya bahari hiyo kwa wakazi jirani na
maeneo hayo. Akiwa ni miongoni mwa wahudhuriaji na wageni wa eneo hilo monica
alifanikiwa kujipenyeza na kuwaambukiza nguvu za Madubwana hayotakribani mabinti
kama tisa wakiwamo Merina,sara,jackline,tinna,shamsa.
*****************************
wakia katika tafrija hiyo mabadiliko yalianza kuonekana taratibu kadri muda ulivyozidi.
Mvuto wa mabinti hao wadogo ambao ilikadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi na tano
mpaka kumi na saba (15-17) hivi ulizidi kuzisumbua hisia za vijana wengi waliokuwapo
eneo la tukio. Wakati wa kipindi cha kuogelea kilipofika ndipo mboni za macho ya vijana
wengi waliokuwepo eneo la tukio hawakuamini kile walichokuwa wakikiona kwa mabinti
hao ambao hawakuwahi kuguswa na kiumbe chochote kile chenye jinsia ya kiume. Kifupi
mabinti hao warembo ambao walikuwa ni wabichi kama wasemavyo vijana wa ishio mjini
siku hizi, huku wengine wakiwa na mtanabaisho tofauti kwa mabinti hao na kuwaita
machenza; hakika ilikuwa ni siku huru kwa kila aliyekuwapo eneo la tukio ambapo
mawasiliano ya macho na ubongo wa kila aliyekuwapo eneo la tukio vilimvuta na
kuhitimisha matamanio ya kila aliyekuwapo ndani ya mioyo yao. Hakika ilikuwa ni siku ya
kustaajabisha na kuhuzunisha kwa vijana ambao walihisi wasingeweza kuwamiliki mabinti
hao.
*****************************
John, kijana msomi na mtanashati aliyekuwapo eneo la tukio wakati hayo yote yakiendelea
alijikuta anashindwa kuvumilia na kuamua kujisogeza taratibu kwa Monica ambaye wakati
huo alikuwa akiyanyonga maungo yake kama binadamu aliyekosa mfupa.

“Habari yako dada? Aliuliza John na kufungua pazia la mazungumzo kati yao “nzuri tu
mambo vipi kaka (Monica anajibu kwa sauti laini iliyomkosha John na kuzidi
kumuongezea hamu ya kusema zaidi na binti huyo) Naitwa John Peter, naishi Mbezi, vipi
naweza kupata mawasiliano yako dada? Naitwa Monica ninaishi Ubungo (river side)
mawasiliano ya nini kaka yangu?
**************
Mazungumzo yao yalisindikizwa kwa muziki wa taratibu uliosikika kando kando ya ufukwe
wa bahari hiyo, sasa ulikuwa ni muziki wa kimagharibi ambao ulikuwa ukipigwa na
hakuwa mwingine bali alikuwa ni mwanamuziki anayeaminika kuwa na sauti nyororo na
nzuri Shania Twain na kibao chake “Forever and for always” kilichokuwa na mistari
iliyowafanya vijana wengi kusogeleana karibu na kuanza kujizungusha taratibu wakiwa
wamekumbatiana. Kusikika kwa wimbo huu saa kuliamsha hisia za John na kumfanya
atumie vyema viungo vyake katika kumbembeleza mwanadada huyo, hapo taratibu
mikono ya John ilisogezwa naye kumshika Monica huku sauti ya John mwenyewe ikiwa ni
ya kubembeleza zaidi, aliivuta mikono ya Monica na kuisogeza taratibu kuzunguka kiuno
chake, sijui ni wimbo au sauti ya bembeleza iliyomsahaulisha Monica ugumu wa nafsi yake
katika kukubaliana na vijana wa kileo kwani taratibu alijikuta akifanya kile John
alichokitaka, wazo la mawasiliano ikiwa ndio kiini cha mazungumzo yao likatiwa kapuni
kwa sasa na kilichoibuka kati yao ikawa ni “Naomba tucheze basi” aliongea John na
kujibiwa kwa vitendo na kisura huyo aliyosheheni sifa zote za urembo, alimwangalia John
na kuachia tabasamu zito, safi na mwanana na kisha lips zake zikafungamana tena kama
aliyehesabiwa sekunde za kutabasamu, aliitoa mikono yake katika kiuono cha John na
kiuipeleka mabegani mwa kijana huyu, taratibu miguu yao ilianza kurandaranda katika
mchanga wa fukwe kuonesha nayo imeafikiana na maamuzi yao, kadiri wimbo ulivyosonga
mbele ndivyo umbali wa wawili hawa ulizidi kufifia na kisha kutoweka kabisa na kuwa ule
wa O distance kama wasemavyo wajuzi wa mambo haya. Wimbo huu ulizidi kuzibamba
nafsi zao….


In your arms I can still feel the way you
Want me when you hold me
I can still hear the words you whispered
When you told me
I can stay right here forever in your arms

And there ain't no way
I'm lettin' you go now
And there ain't no way
And there ain't not how
I'll never see that day


[Chorus]
Cause I'm keeping you
Forever and for always
We will be together all of our days
Want to wake up every
Morning to your sweet face always

Mmmm, baby
In your heart I can still hear
A beat for every time you kiss me
And when we're apart,
I know how much you miss me
I can feel your love for me in your heart

And there ain't no way
I'm lettin' you go now
And there ain't now way
And there ain't no how
I'll never see that day

[Chorus]
(I want to wake up every morning)
In your eyes (I can still see
The look of the one) I can still see
The look of the one who really loves me
(I can still feel the way that you want)
The one who wouldn't put anything
Else in the world above me
(I can still see love for me) I can
Still see love for me in your eyes
(I still see the love)

And there ain't no way
I'm lettin' you go now
And there ain't no way
And there ain't no how
I'll never see that day

[Chorus: x2]

I'm keeping you forever and for always
I'm in your arms

Kadiri maneno haya yalivyopenyeza na kupasua ngome za masikio yao ndivyo vijana hawa
walivyozidi kupata misisimko katika fikra zao na kufanya waliokumbatiana wazidi
kushikana vyema na waliokaa wakasimama wakianza kucheza nao kwa madaha wengine
wakitumia nafasi hizi kuomba mahusiano ya kudumu huku walio tayari katika hili
wakiweka ahadi za uchumba………
 


INAENDELEA.......

Juu