Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

HATIMAYE CHIMBO - SCHOOL OF THOUGHT CHINI YA MC. HARRIS KAPIGA YAPIGA HATUA MBELE ZAIDI



Ile Shule maarufu ya kubadilisha fikra ijulikanayo kwa jina la ''CHIMBO - SCHOOL OF THOUGHT'' Inayofanyika kila siku za Jumapili jioni kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 1:00 Usiku ambapo inakusanya watu/vijana zaidi ya 100 wanaohudhuria kila siku za Jumapili.

Ni hakika ukiwa na maono kama ya Tai, utatamani kila siku upige hatua moja mbele. Ndivyo ilivyokuwa kwa CHIMBO - SCHOOL OF THOUGHT kwa kuwa imelenga kubadilisha fikra za Watanzania na kuwa na mkakati madhubuti wa kuwafikia Watanzania wote kwa idadi yake, MC na Mtangazaji Harris Kapiga (Founder) akishirikiana na jopo zima la CHIMBO - Directors wameanzisha Radio Program ambayo itaanza Jumamosi Hii ya tarehe 07/09/2013 katika kituo cha radio cha Praise Power 99.3 FM kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 11:00 Jioni.
Watangazaji watakuwa ni: Peter Msilu akishirikiana na Sarah K, ambao pia ni miongoni mwa CHIMBO - Directors.

NB: Ile program ya kila Jumapili NCHI YA AHADI inaendelea.

IFUATAYO NI JINGLE YA KIPINDI CHA REDIO CHA CHIMBO, NDANI YA PRAISE POWER RADIO 99.3 FM. Ikiambatana na baadhi ya picha za CHIMBO DIRECTORS waliovalia sare za kijani, pamoja na wadau/washiriki wa CHIMBO.





NI MATUMAINI YANGU KUWA, wewe kama mfuatiliaji wangu mzuri wa Blog Hii Utaendelea kubarikiwa sana kwa sababu nitakuwa nakuletea kila kinachojiri pale CHIMBO Nchi Ya Ahadi.

Nakukaribisha pia CHIMBO Nchi Ya Ahadi, Sinza (zamani kamanyola)tujifunze pamoja, Blog Hii Pia Inakuwepo pale kila siku za Jumapili ambapo utapata fursa ya kuonana nami pia nikiwa kama mmoja wa Directors Wa CHIMBO.

MUNGU AKUBARIKI

JE WAJUA NI NANI ALIYEGUNDUA KIPAJI CHA MWIMBAJI WA GOSPEL HIP HOP GODFREY BENJAMIN a.k.a G & SET ALIYETAMBA NA WIMBO WA ''KUTANA NAYE''?

Godfrey Benjamin afunguka alipofanya mahojiano na Blog hii kupitia Platform Yetu Ya ''GOSPEL EXCLUSIVE INTERVIEW PLATFORM - GEIP''

Aidha alisema kuwa ALLEN CHISUNGA a.k.a pastor peter (mtoto wa mchungaji) ndiye aliyemuonyesha kipaji chake.
Msikie hapa kwenye hii Clip.

Nawe kama ungependa tukufanyie Interview; Usisite kutupigia kwa: 0659 700 002

BARIKIWA!

NITA-SUPPORT GOSPEL HIP HOP - Asema Rev. RON SWAI Ndani Ya Gospel Exclusive Interview Platform_ The GEIP.

NITA-SUPPORT MUZIKI WA GOSPEL HIP HOP - Asema Rev. Ron Swai wa kanisa la DAR CALVARY TEMPLE lililopo Tabata Shule:
Hapa akiwa ndani ya EXCLUSIVE YA: GEIP inayomilikiwa na Blogger (mdeejunior.blogspot.com) ambaye pia ni Admin wa ''GOSPEL EXCLUSIVE INTERVIEW PLATFORM''._ https://www.facebook.com/exclusive.interview Click uweze Ku-LIKE Page Yetu.


MH. FREDRICK T. SUMAYE AZUNGUMZA NA VIJANA WA KITANZANIA NDANI YA CHIMBO - SCHOOL OF THOUGHT.


Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mh. Fredrick Sumaye siku ya Jumapili ya tarehe 11/8/2013 alikuwa mzungumzaji ndani ya CHIMBO - School Of Thought iliyo chini ya Harris Kapiga ambaye ni Mchungaji, MC na Mtangazaji wa CLOUDS TV na CLOUDS FM Radio ya jijini Dar es Salaam.

Chimbo-School Of Thought hufanyika kila siku za Jumapili kuanzia saa 9:00 Alasiri Hadi saa 1:00 Usiku, Mahali ni Sinza Nchi Ya Ahadi (zamani kamanyola).
Mh. Sumaye alizungumza na umati mkubwa wa vijana waliohudhuria siku hiyo juu ya jinsi na namna ya kuitunza amani ya Tanzania kwa ajili yetu na kizazi kijacho baada yetu.

HIKI NDICHO ALICHOSEMA MH. SUMAYE.

Mh. Fredrick Sumaye alifunguka kwa kuonyesha uzalendo wake na mapenzi yake kwa nchi ya Tanzania ambapo hakuzungumzia chama chochote cha siasa pamoja na kuwa yeye ni mwanachama wa chama fulani kikubwa hapa nchini.

Mh. Sumaye alisema:
Amani ya Tanzania inaletwa na itatunzwa na sisi wenyewe, unajua tunaitumia siasa vibaya. Lazima sisi kama viongozi wa siasa tunatakiwa tuwe makini sana kama kweli tunataka amani iendelee kuwepo. Na umakini wetu lazima haki ionekane inatendeka ipasavyo.
Lazima vyama vya siasa viwe makini, wote tufuate sheria, tume ya uchaguzi iwe muelekezi mkuu wa taratibu za uchaguzi na tusitumie vijana kuvuruga au kuwapambanisha.

Aidha aliendelea kusema kuwa:
Zipo dalili mbalimbali za vyama vya siasa kuanzisha majeshi na hilo ni jambo la hatari litakalovuruga amani yetu kama sio kuipoteza kabisa - alisisitiza.

Katika hotuba yake, Mh. Sumaye alionekana kuongea kwa hisia sana na kuwasihi umati mkubwa wa vijana waliojitokeza kuwa makini maana wao ndio wanaotumika kwa sababu wana nguvu na rahisi kuchochewa. ''Lakini mkiwa makini hamtatumika kuchochea vurugu/fujo''-alisema kwa msisitizo.
Endapo mtakubali kutumika na kuchochea fujo/vurugu mtambue kwa hakika kuwa hizo fujo na vurugu mtakuwa nazo ninyi kwa muda mrefu kuliko mtu mwingine yeyote akimaanisha kizazi hiki na kile kijacho baada ya hiki.

Kwa hiyo kama tunataka kurithisha amani hii kwa wenzetu wanaokuja huko baada ya sisi na baada na ninyi (vijana) na vizazi vingine ni lazima tufuate taratibu nzuri za siasa.

*****************************************************************************

Click hapa uweze ku-LIKE Ukurasa wetu wa CHIMBO-SCHOOL OF THOUGHT

Jumapili hii ya Tarehe 18/8/2013 Mh. Jerry Slaa atazungumza ndani ya Chimbo-School Of Thought
mada atakayozungumza ni ''JINSI GANI UNAWEZA KUIISHI NDOTO YAKO'' How to Live your Dream.






MH. SUMAYE AKIWA AMEPIGA PICHA YA PAMOJA NA CHIMBO DIRECTORS

Wasiliana na Blog hii:
0659 700 002
0653 100 100
halisitz@gmail.com


Juu