Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

HALI YA MWIMBAJI WA INJILI NCHINI SI NZURI, YUPO CHUMBA CHA UPASUAJI SASA, MUOMBEE KAMA VILE HUJAWAHI KUOMBA TENA.



Maombi yako yanahitajika ili Mungu amponye mwimbaji wa muziki wa injili nchini Debora John Saidi ambaye hali yake inaelezwa kwamba si nzuri nasasa yuko chumba cha upasuaji hospitali ya Mwananyamala kuondolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao umesababisha alie kwa maumivu makali.

Upasuaji wa kutoa uvimbe huo ulitarajiwa kufanyika kesho, lakini kutokana na maumivu pamoja na kilio kutoka kwa mwimbaji huyo imebidi kupelekwa chumba cha upasuaji mchana huu. Ambapo mchana wa leo baadhi ya waimbaji wenzake akiwemo Joshua Makondeko, Tumaini Njole walifika hospitalini hapo kumjulia hali. Mdau wangu sema neno la uponyaji kwa ajili ya Debora John Saidi.
Zaburi 103:3-4.





Source: GK.

Debora akilishwa kabla ya kupelekwa chumba cha upasuaji.
Mungu akuponye Debora.



Joshua Makondeko akimnywesha maji Debora.

ROSINE SWAI: MKALI MPYA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA - AJA NA LADHA TOFAUTI.

MKALI MPYA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA - LADHA TOFAUTI.
NI Rosine Swai KUTOKA MKOANI KILIMANJARO.

WASILIANA NAYE KWA WHATSAPP: 0759 037 903,
PIA MUDA SI MREFU ZITASIKIKA KWENYE INTERNET NA MITANDAO MINGINE YA KIJAMII PIA UNAWEZA KUTUMIWA WIMBO KUPITIA WHATSAPP KWA NAMBA HIYO HAPO JUU.

ROSINE SWAI: ANAOMBA WAPENDWA NA WADAU WOTE WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA NA HATA NJE YA TANZANIA MUMSAIDIE KU-SHARE HII KWA MARAFIKI MBALIMBALI.

NOTE: HAYA NI MAANDALIZI YA UJIO WA ALBUM YAKE YA KWANZA AMBAYO IKO JIKONI,
MUDA SI MREFU ITASIKIKA MASIKIONI MWA WAPENZI NA WADAU WOTE WA MUZIKI WA INJILI.




Mtafute kwa namba hizi:
0759 037 903, Pia inatumika kwa Whatsapp.



NAJUTA KWA NINI NILIKUBALI KUOLEWA, Na Mary Muna katika page yake ya SINGLES.

   Wakati dada Mary kutoka mkoani Arusha anaeleza kisa hiki kuhusu masuala mazima ya ndoa, Mdee Junior ( Ze Blogger ) anajiandaa kwa engagement Jumapili hii ya tarehe 20 Jan. 2013 katika kanisa la Ebenezer ( International Pentecostal Holiness Church ) lililopo Tabata Segerea. UNAKARIBISHWA KUMSINDIKIZA kijana huyu, kuwasiliana naye tumia mawasiliano hapo chini kabisa.



   Sawa, baada ya utangulizi huo mfupi; hebu sasa jiweke tayari kusikia kile kinachojiri ndani ya wana ndoa hawa amabo ni Merian na Joseph ( sio majina yao halisi, kwa sababu maalum ).


NImejifunza jambo kutoka kwenye huu ushuhuda nadhani na wewe utapata kitu.

NAJUTA KWA NINI NILIKUBALI KUOLEWA!

Baada ya mwaka mmoja wa ndoa, Merian asema anajuta kwa nini alikubali kuolewa. Merian na Joseph (haya siyo majina yao halisi) ni mtu na mumewe. Nikiwa katika Mkoa wao kikazi, niliamua kuwatembela wanandoa hawa. Merian alinipokea na kunikaribisha ndani kwa furaha sana. Tukaanza kuongea nami nikamuuliza, Joseph yupo? Akaniambia bado hajarudi kutoka kazini, hata hivyo kaniambia yupo njiani anakuja.

Tukaanza kuzungumuza mambo kadha wa kadha na kisha nikamuuliza mnaendeleaje na ndoa yenu changa? Baada ya kuwa nimemuliza swali hili akacheka na kisha akaanza kwa kusema, nyie maisha haya ya ndoa yaacheni tu, kwa kweli najuta kwa nini nilikubali kuolewa? Kauli hii ilinishtua sana kwa sababu kwanza sikuitegemea na pia ndoa hii ilikuwa ndio imetoka kutimiza mwaka wa kwanza tu.
Kwa haraka kabla hajaendelea nikamzuia asiseme hayo maneno tena, maana nilijua kadri anavyosema ndivyo anavyozidi kuumba uharibifu kwenye ndoa yake. Akaniambia usinizuie, si umeuliza tunaendeleaje, subiri nimalize kukuelezea. Ndipo akaanza kuniambia kile kilichompelekea kusema anajuta kwa nini alikubali kuolewa (Kwa ufupi ni changamoto ambazo kwa ujumla naweza kusema za kawaida, hata hivyo sitaweza kuziandika hapa kwa sababu maalum).
Katika maelezo yake Merian aliniambia, vijana wengi sana walinifuata ili kunioa, mie nikawakataa, natamani ningeolewa na yoyote kati ya wale wengine, lakini si hapa nilipo na laiti likitokea lolote sasa (kwa maana ya mwenzake kufa) sitakubali kuolewa tena.
Mpenzi msomaji sijui kama unakiona ninachokushirikisha kupitia maisha ya wanandoa wenzetu hawa. Kumbuka ni mwaka mmoja tu wa ndoa, na leo tunashuhudia Merian akijutia maamuzi yake ya kuolewa na Joseph. Licha ya kwamba ni mwaka wa kwanza tu, lakini wawili hawa wameokoka pia.
Maelezo ya dada Merian yaliniletea maswali matano (5) ndani yangu ambayo ndiyo ninayotaka tujifunze kutoka kwake;
Swali la kwanza; Je! Merian, alijua nini maana ya ndoa kabla ya kuolewa?
Swali la pili: Je, Merian alijua aina ya maamuzi anayotaka kufanya kabla ya kuolewa?
Swali la tatu: Je, Merian alimuhusisha Mungu kabla ya kuolewa ili ampate mwenzi sahihi wa kuishi naye?
Swali la nne: Je, Merian alikuwa amejiandaa/andaliwa kifikra kuishi kama mke?
Swali la tano: Je, mpaka sasa, Merian anajua wajibu wake ni nini kwenye ndoa?
Kutokana na maswali haya niliwaza mambo matatu ambayo, nafikiri kama vijana wangefahamu yatawasaidia katika ndoa zao;
Moja, ni vema vijana wajifunze kumshirikisha Mungu awaongoze kupata mwenzi sahihi wa maisha, kabla hawajaingia kwenye hizo ndoa.
Mbili, ni vema vijana wakajifunza kufikiri kimapana kabla ya kuingia kwenye ndoa. Swali la msingi katika kufungua tafakuri hii, ni kwa nini mtu aoe au kuolewa? Ni swali fupi lakini kama wewe ni mtu ambaye hufikiri kimapana swali hili litakujengea msingi mzuri wa baadaye. Naam kile kitabu cha 1 Wakorinto sura nzima ya saba kikuongoze katika tafakuri hii.
Tatu, ni vema vijana wangefunzwa/kuandaliwa vya kutosha kuhusu ndoa na hasa wajibu uliopo mbele yao. Endapo kama Serikali inawasomesha watumishi wake kwa lengo la kuwaongezea uwezo na maarifa ya kutekeleza majukumu yao, basi ifike mahali kanisa, wazazi, viongozi wa vijana nk makundi haya yaone umuhimu wa kuwaandaa vijana wao kuyakabili maisha ya ndoa.
Watu wengi hufikiri chanzo cha matatizo kwenye ndoa zao ni Shetani. Ndio hii ni sababu moja, lakini sababu nyingine kubwa, ni watu wengi kukosa ufahamu wa masuala ya ndoa kabla na baada ya kuingia kwenye hizo ndoa. Naam wakati watu wanasema Shetani anaangamiza ndoa zetu, Mungu anasema, ndoa za watoto wangu zinaangamizwa kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6).
Ni imani yangu kwamba, kama mambo haya yatazingatiwa, sehemu kubwa ya changamoto ambazo wanandoa wanapitia, zingepata ufumbuzi wa haraka. Natoa wito kwa wadau mbalimbali wa masuala ya ndoa na hasa Wachungaji, Walimu na Viongozi wa makundi ya kiroho, kuanzisha utaratibu wa kuwa na mafunzo maalum kuhusu ndoa, kwa vijana ambao wameweka wazi dhamira zao za kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Ni vema pia, hata kwa wale ambao wako ndani ya ndoa, wakawekewa utaratibu wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara, maana kwa mtazamo wangu ndoa ni shule ambayo, wahusika wanapaswa kuongeza (kujifunza) ufahamu wao kila siku, ili kulitumikia vema kusudi la Mungu.

   Naamini umepokea kitu, kwako wewe ambaye bado hujaingia kwenye ndoa na wewe ambaye tayari upo kwenye ndoa! Haya ni mambo ya msingi sana kuyazingatia, na kwa sababu hiyo basi naomba mniombee sana maana najiandaa kuingia na engagement yangu ni jumapili hii tarehe 20. Jan. 2013 pale Tabata Segerea, karibu tushiriki pamoja.
Nitafurahi kukuona.

Mawasiliano:

+255 659 700 002
+255 756 145 417

mdeejunior@gmail.com (barua pepe)
@mdee_junior  (twitter)
mdee.junior (skype)

DREAM BIG AS YOU GROW BIG.

NDOA INAPOGEUKA KUWA NDOANA.

Haya ni moja ya mazungumzo niliyoweza kuzungumza na dada mmoja rafiki yangu kutoka Africa ya Kusini kupitia mtandao wa facebook. Huyu dada (jina nalihifadhi ila nitatumia jina la Leez kuwakilisha jina lake, pia nitatumia John kuwakilisha jina la mume wake) aliwahi kunishirikisha nimuombee juu ya ndoa yake ipate kusimama. Nilifanya hivyo na ikafika kipindi Mungu akaonekana kwao, nakumbuka siku moja alinipigia simu akiwa na mumewe akaniambia 'hivi tulikuwa tunakuzungumzia na mume wangu' ndo mana nimekupigia, nimemwambia mume wangu tupange tuje Tanzania kukutembelea.

Nimeondoa picha yake kwa sababu za msingi.
Mazungumzo yalikuwa hivi;


  • Mdee Junior
    Hi
    Leez
    nice to have you online today....stay blessed!

    Leez.
    i'm glad to have u on line my friend, be blessed!

  • Mdee Junior

    Abundant Life and breakthrough for you Leez, 
    • January 25, 2011
    • Leez
      God Bless you
      You are God send Mdee thanks for your message, i am filing for a divorce Mdee i dont know what to do anymore. I have prayed for John but he just doesn't want to change. I cried a lot on Saturday, he left for work Saturday morning and only came back on Sunday at 1am, he didnt even show remorse, he never even try to explain where he came from. Mdee i really need God's devine intervention but i am going ahead with the divorce but my wish is to stay with my husband but he doesn't love me anymore. i am beautiful and i have NEVER cheated on him i dont even wish to be cause i am God's vessel. Mdee i dont know what to do (crying)

      • Mdee Junior

        Leez, i do understand and wanna see your marriage stands firm, i still praying for you both. One thing i would ask you is to change prayers! From now am gonna pray for the WILL OF GOD TO BE DONE'' as Jesus our Savior did the time He was approaching the Cross! He prayed, Father let your will be done not mine'' ts incredible! Leez, stand firm for the LORD will fight for you to the Destination!

        • Mdee Junior

          He's Jehovah ADONAI ''LORD THE MASTER''
          • Baada ya muda kitambo tukakutana tena mtandaoni, ikawa hivi.
          • Mdee Junior

            How is your family! tell me how is your precious husband doing.
            • Leez

              Eyy my friend things are not looking good that is why I spend most of my time on face book. We are sleeping in different rooms and he doesn't see anything wrong with that. He is so depended on me and gets upset if I can't help him financially. We have a baby now and he doesn't seem interested in the baby either and it looks like he isn't aware that what he is doing is totally wrong

              Inafika mahali mwanandoa anaamua kutafuta faraja facebook. Mungu tusaidie.
              • Mdee Junior

                OOoohh nooo!!!! sorry my dear, so how do you feel. though i hesitate to ask such a question!

                Hapa alikaa kimya kidogo bila kujibu chochote. Nikaendelea kuchokonoa...
                • Mdee Junior

                  my friend, i know how painful ts but the end has come n u shall cry no more! You just TRUST THE LORD n show appreciation to him (husband)

                  Hapa anafunguka na kuanza kuzungumza, nahisi alikuwa analia...
                  • Leez

                    That is exactly what I'm doing Mdee. I prayed for my partner before I got married. He is the only man I have know so if this is what God want me to have then I accept but I will keep on praying for him. I used to cry but not anymore I don't think I'm capable of loving anymore I just live to see my children grow but one day God will answer me I don't know how but he shall answer my prayers
                    • February 25, 2012 Muda ulipita kidogo bila mawasiliano, mara tunakutana tena mtandaoni.
                    • Mdee Junior

                      hello my dear sis.
                      • Leez

                        Hey Mdee how are you my brother I miss our interactions a lot
                        • Mdee Junior

                          i'm highly favored, how are kids doing?
                          • February 28, 2012
                          • Leez

                            They are great my brother and also growing strong in the Lord, they are my angels I luv and appreciate them.
                            • April 11, 2012
                            • Mdee Junior

                              IS IT REALLY YOU? Hapa nalimuuliza kwa mshangao kwa sababu ilikuwa ni miezi kadhaa imepita bila mawasiliano.
                              • Leez

                                What did I do now my friend lol
                                • Mdee Junior

                                  nothing, just greetings en happy to meet u online! how are you my friend!
                                  • Leez

                                    I'm good Mdee and u. Its been long since we chat I miss that I will definitely call u 2morrow

                                    Kama nilivyokuwa nimezungumza hapo awali, ni kweli siku iliyofuata alinipigia simu akiwa na mumewe.
                                    • July 5, 2012   Miezi kadhaa ikapita, tukakutana tena mtandaoni.
                                    • Mdee Junior

                                      hello friend!
                                      • Leez

                                        Hi Mr how are you
                                        • Mdee Junior

                                          am gud missing you.
                                          • Leez

                                            Also miss you my friend
                                            • Mdee Junior

                                              thanks frnd
                                              • Leez

                                                It's been long since we chat I miss that a lot
                                                • Mdee Junior

                                                  yes i know, that's why some times i tried to call.
                                                  i understand the connection we have between us, Godly connection.
                                                  • HUYU DADA ANA MIAKA NANE KWENYE NDOA, AMEFIKA MAHALI AMEKATA TAMAA ANATAMANI TALAKA.
                                                  • KUNA USHUHUDA ALIWAHI KUNIANDIKIA KITU MUNGU ALIFANYA KWA MUMEWE, MUNGU ALIFUNUA TATIZO LILIPO, IKAMFANYA AWEZE KUOMBA MAOMBI YA KULENGA. NITAUTAFUTA HUO USHUHUDA HALAFU NITAKUSHIRIKISHA MANA NI TAKRIBANI MIAKA MIWILI ILIYOPITA KAMA SIO MWAKA MMOJA.
                                                  • PIA NITAMTAFUTA KWENYE SIMU NIMUULIZE NDOA IMEFIKIA WAPI, KWANI SIMPATI facebook, amekuwa kimya sana; inawezekana ni majukumu ya kazi kwani alinishirikisha kuna mahali alikuwa aende kufanya interview hivyo tukaomba; akafanya interview akafaulu na kupata ajira.

                                                  Rafiki yangu unayefuatilia blog hii hasa katika segment ya KONA YA WATUMISHI, hebu tafakari kwa kina, jiweke katika nafasi ya huyu dada kisha jiulize swali hili: JE! NINGEFANYA NINI?

                                                  Namshukuru Mungu kwa ajili ya huyu dada (yeye ni mzaliwa wa Afrika Ya Kusini), kiukweli amemshika Mungu sana vinginevyo tungerejea ile tamthilia ama riwaya ya ''THINGS FALL APART''

                                                  Ukiguswa na hali anayopitia huyu dada, piga goti muombee kwa machozi na kwa kuugua!


                                                  Nakupenda, Mungu akuongeze na kukuzidisha!
                                                  AMINA!


                                                  +255 659 700 002
                                                  +255 756 145 417
                                                  mdeejunior@gmail.com (barua pepe)
                                                  mdee.junior (skype)
                                                  @ mdee_junior (twitter)


                                                  TUNAKARIBISHA MAONI NA USHAURI KUHUSU BLOG HII, Tumia mawasiliano hapo juu
                                                  au andika comment yako/maoni yako hapa chini. 


                                                  DREAM BIG AS YOU GROW BIG.




                                                  KONA YA WATUMISHI: Kutoka kurasa za facebook na groups mbalimbali.

                                                     Hiki ndicho alichofundisha mtumishi wa Mungu Gasper Madumla kupitia page yake ya NENO LA MTUMISHI. Blog hii imeona vema kukushirikisha nawe upate kile Mungu anataka upokee siku ya leo na ndio kusudi la blog hii. Karibu twende pamoja.

                                                     Pia mtumishi wa Mungu Upendo Benson, na Mary Muna katika kurasa zao za facebook wamezungumza kitu ambacho kitakusaidia kutafakari. Upendo Benson ametoa dondoo (highlight) fupi juu ya mahusiano, ni kazi yako kupanua akili na ufahamu wako juu ya kile ambacho ametoa kama highlight.
                                                  KARIBU.


                                                  Mtumishi Gasper Madumla

                                                  Bwana Yesu asifiweee……

                                                   NENO:SIMAMA IMARA UKAUONE WOKOVU WA BWANA.
                                                  Ninanakusalimu mpendwa katika jina la Yesu Kristo aliye hai,nikimuomba Bwana Mungu afungue moyo wako ili upate kupokea hiki ninachokuletea siku ya leo,maana ujumbe huu umekusudiwa kwako wewe mpendwa usomaye ujumbe huu, na wala si mwingine aliyekusudiwa bali ni wewe.
                                                  Ninakuhakikishia kabisa endapo utafanikiwa kusoma mpaka mwisho,Mungu atakufanyia jambo,nawe utapenya kupitia somo hili,litakuwa Baraka sana kwa kila atakayesoma.

                                                  Wokovu wa Bwana haupatikani kwa njia nyepesi. Maaana hata maandiko yanatuambia kwamba -yeye takayevumilia hata mwisho ndio atakaye okoka. 

                                                  Swala la kuokoka ni jambo la muda mfupi sana yaani ni dakika tu pale utakapokuwa umeongozwa sala ya toba na kumaliza,ila kuna maisha mengine baada ya hapo,hayo maisha ni WOKOVU. 

                                                  Na tunaokoka ili tufanye kazi ya Mungu,na sio kwenda mbinguni tu,maana ingekuwa swala ni kwenda mbinguni tu,basi watu wote waliokoka wangekuwa wamekufa tangu siku ile walipookoka,BALI WAPO HAI ILI WAYAFANYE MAPENZI YA BABA NA MWISHO NDIO WAFIKE MBINGUNI. Halleluyaaa..

                                                  • Maisha ya wokovu ni mchakato wa maisha ya utauwa
                                                  • Utauwa ni maisha ya kumlingana na Mungu,yaani maisha ya UTAKATIFU
                                                  • Na kumbuka bila huo utakatifu hakuna atakaye muona Mungu,( Waebrania 12 :14 )
                                                  Kumbe ! Yatupasa tuwe watakatifu kwanza ili tuweze kumuona Mungu, Watu wengi utawasikia “ Jamani nimemuona Mungu kwa njia tofauti tofauti, Hali wao si WATAKATIFU,maisha yao yamejaa dhambi tupu,HAPO HAKUNA MUNGU LABDA KUNA mungu . Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mungu na mungu,

                                                  ^ Mungu = Baba wa Mbinguni aliye hai,Jehova, MUNGU MWENYE NGUVU
                                                  ^ mungu = miungu ya wapagani,anaweza labda kuwa ngombe,n.k HANA UTUKUFU

                                                  Wewe mpendwa endapo utasimama imara kuutafuta uso wa Mungu, Hakika utauona wokovu wa Mungu, na hapo utakuwa ni wa tofauti na pale ulivyokuwa kabla.

                                                  Tunasoma KUTOKA 12 : 1-2

                                                  “ Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 
                                                  Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. ”

                                                  Hawa wana wa Israel walikuwa utumwani muda wa miaka 430 (Kutoka 12 : 40 ) ila Mungu alikuwa ana haja nao,Haja ya Mungu ilikuwa anataka ajitwalie utukufu kupitia wao waende kumuabudu Mungu aliye hai,

                                                  Kumbuka Mungu akiwa na haja na wewe ni lazima atakupata tu,na atakupandisha juu pindi utakapo tii sauti yake kwa BIDII 

                                                  Tunasoma Luka 19 : 29-31

                                                  “ Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi, 
                                                  akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa. 
                                                  Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji. ”

                                                  Huyu Punda alikuwa kifungoni yaani alikuwa amefungwa katika NIRA ambayo kwa hiyo alikuwa hana uwezo wa kufanya chochote kile atakacho kufanya isipokuwa ni kufanya yele atakayo bwana wake aliyemfunga.

                                                  Halleluuyaaa…

                                                  Punda wa sasa anawaeza kuwa wewe,ikiwa umefungwa yaani hauwezi kufanya chochote kile utakacho na kufanikiwa BASI UPO KIFUNGONI shetani yeye ufunga watu,

                                                  Sasa tazama pale Yesu anasema “ 31” na alipofunguliwa huyu punda tunaona anatandikiwa nguo zao njiani naye huyo punda anapita kwa heshima kubwa kabisa ambayo hapo mwanzo alikuwa hawezi kuipata kabisaa,kwa sababu alikuwa AMEFUNGWA 

                                                  Tena huyo punda baada ya kufunguliwa na Yesu,Bwana Yesu Kristo akampanda,akaka juu yake huyo punda na watu woteee wakapaza sauti zao kwa kelele za shangwe 

                                                  Maana tena walikuwa hawamuoni punda bali wanamuona Yesu wa nazareti aliye hai akitembea juu ya punda,MAANA YEYOTE YULE ALIYEMBEBA YESU,SI YEYE ATAKAE ONEKANA BALI NI YESU NDIE ATAKAYEONEKANA BADALA YAKE, 

                                                  NA MTU HUYU NI YULE ALIYESIMAMA IMARA KATIKA MAISHA YA UTAUWA ,NA WATU WATAKUPA KIBALI NA HESHIMA KUU, SABABU SI WEWE BALI NI YESU JUU YAKO.

                                                  Ooooh,HALLELUYAAAAAA,
                                                  Mtu mmoja aseme AMEN,

                                                  Najisikia nikuhubirie zaidi,THANKS JESUS 
                                                  Kwa kukufanya wewe kuendelea kusoma ujumbe huu,hakika Bwana Yesu ana haja na wewe,maana wewe ni kama huyo mwanapunda ambaye Yesu alikuwa ana haja naye.

                                                  Sasa turudi katika andiko la kwanza
                                                  KUTOKA 12 : 1-2

                                                  Hawa wana wa Israel baada ya kuishi miaka mingi namna hiyo tunaona Mungu anawaambia kwamba mwezi huu utakuwa ni ni mwezi wa kwanza wa miaka kwao,

                                                  hii inamaanisha siku ile ndio ilikuwa haswaaa ni siku ya kuokoka kwao, maana hata miezi ilibadilika,miaka pia ilibadilika, KWA SABABU HII “ YAKALE YAMEPITA YAMEKUWA MAPYA” Yaani mtu yeyote mwenye dhambi akija kwa Yesu Kristo mtu huyo anafanyika mpya na Bwana Mungu azikumbuki tena dhambi zake.

                                                  • Ukisimama imara utauona wokovu wako
                                                  JAMANI MAMBO MENGINE HUJALOGWAAA!
                                                  BALI TU ,MUNGU ANATAKA UMTUMIKIE ILI NA YEYE AKUPIGANIE.

                                                  Tunasoma Kutoka 14 : 13
                                                  “ Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. ”

                                                  Ninakuambia hivi ;
                                                  Kwa yale makwazo yanayokufanya ushindwe kupokea ahadi za Mungu,leo ndio mwisho wake na hutayaona tena endapo utamaanisha kulichukua somo hili na kulifanyia kazi
                                                  Maana njia ni moja tu ,nayo ni YESU KRISTO PEKEE yeye ndio njia na kweli.

                                                  Tazama mstari huo,Mungu anasema “ USIWAOGOPE HAO WAMISRI ”
                                                  • Magonjwa uliyonayo ni wamisri
                                                  • Kufungwa Kutokuolewa/kuoa ni wamisri
                                                  • Kudumaa kiroho ni wamisri tu
                                                  • Ugumu wa maisha ni wamisri tu N.K

                                                  HAYO YOTE USIYAOGOPE WEWE SIMAMA NA YESU KRISTO UKIMTUMIKIA KWA FURAHA ZOTE,MAANA HAO WAMISRI HAUTAWAONA TENA KATIKA JINA LA YESU KRISTO,POKEA…..

                                                  Ni ombi langu kwako kuwa,Wakati uombapo usiwe unapenda kuomba mambo ya maisha yanayoharibika,na yenye kupita mfano kuomba kila wakati MUME,MKE,KUJENGA,KUPATA KAZI,KUNUNUA GARI,KUPANDISHWA KAZI NA MAMBO KAMA HAYO, 

                                                  Bali wewe taka sana mambo ya rohoni naye yote utazidishiwa omba MUNGU AKUFUNGUE MACHO YA ROHONI,.AKUPE NJAA YA KUMTAFUTA,NA YOTE YA ROHONI,NA HAPO NDIPO UTAWEZA KUSIMAMA IMARA UKAUONE WOKOVU WAKO.




                                                  • Kipengele kinachoitwa kupenda hakina professor wala Dr wala mwalimu wala mtaalam wala police wala rais wala waziri... ukishapenda tu wewe baaasi.... ikifika pa kutendwa utatendwa tu, pa kufanywa zoba utakua zoba tu, pa kudanganywa utadanganywa tu, pa kulizwa utalizwa tu, pa kusalitiwa utasalitiwa tu.. kwenye kipengele hiki cheo hakina kazi na ujanja wako unawekwa kapuni.



                                                    Give all of you to Jesus...and He will make what you think is nothing...into something. What you keep from Jesus-keeps you in confinement...what you give to Jesus-is what defines you. Give Him what you have so He can define you! (John 1:3).



                                                  Mungu awabariki kwa kufuatilia blog hii.
                                                  Tunakaribisha maoni kuhusu blog hii.

                                                  Wasiliana nasi kwa:

                                                  +255 659 700 002
                                                  +255 756 145 417
                                                  mdeejunior@gmail.com (email)
                                                  @mdee_junior (twitter)
                                                  mdee.junior (skype)

                                                  DREAM BIG AS YOU GROW BIG.


                                                  Juu