Alichosema Mnyika kuhusu tuhuma za rushwa na ripoti ya Ngwilizi hiki hapa.
Sijakubaliana na maamuzi ya leo spika kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge na hatma ya kamati ya nishati na madini. Nitamkatia rufaa. Ripoti yote ya Ngwilizi inapaswa iwekwe hadharani, amenukuu kumbukumbuku alizotaka yeye kuhalalisha maamuzi. Nimeamini bunge haliwezi kujichunguza lenyewe na kutoa maamuzi huru katika masuala yanayohusu wabunge. Aidha, katika suala la ununuzi mafuta mazito ya umeme wa dharura maelezo yamedhihirisha haja ya kuundwa kwa kamati ya bunge kuchunguza mchakato ulivyokwenda kwa makampuni yote kama nilivyopendekeza bungeni kwenye hotuba yangu tarehe 27 Julai, 2012.
John Mnyika.
John Mnyika.