RAIS WA KOREA KASKAZINI AAGIZA WAKRISTO 33 KUNYONGWA
Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini.©Manlycurls |
Wakristo duniani wametakiwa kuomba kwa ajili ya mabadiliko ya ki Mungu
katika taifa la Korea Kaskazini ambako Rais wa nchi hiyo Kim Jong Un
ameagiza kunyongwa kwa wakristo wapatao 33 wa nchini humo ambao
wanadaiwa kupokea msaada wa kuendesha makanisa ya siri kutoka kwa
mmisionary wa Korea ya Kusini Kim Jong Wook.
Kwa mujibu wa Rais wa shirika la Open Door la nchini Marekani bwana David Curry
katika ujumbe wake jumatatu hii amesema Korea kaskazini ni nchi
inayoshika namba moja katika orodha iliyotolewa na shirika hilo kwa nchi
ambazo wakristo wanaishi katika hatari kubwa duniani ikiwa katika
nafasi hiyo kwa miaka 12 mpaka sasa. Amesema kwasababu nzuri kabisa
unapoona manyanyaso yanazidi katika taifa ndipo moyo wa kumuhubiri na
kumtangaza Kristo unapoongezeka hivyo kuwataka wakristo kuungana naye
kuliombea taifa hilo.
Wiki iliyopita moja ya gazeti la Korea kusini limeripoti kwamba Rais Kim
Jong Un ametoa maagizo ya kunyongwa kwa wakristo hao 33 baada ya
kugundulika kupokea msaada huo ambao ni wakujenga makanisa 500 ya siri
kitu ambacho ni kinyume cha sheria nchini humo kwa kujiunga katika
vitendo vya kidini adhabu yake ikiwa ni vifungo ama kunyongwa hadharani
katika taifa hilo la Korea ya kaskazini.
Rais Kim akiwa na marehemu mjomba wake Jang aliyenyongwa mwaka jana.©kyodo News |
Shirika la Open Doors limewaomba wakristo kuomba rehema kwa watu wote
ambao wamehukumiwa kifo huko Korea ya kaskazini, pamoja na wamisionari
wengine ambao wameshikiliwa nchini humo kutokana na imani yao, ikiwa
pamoja kuliombea taifa zima la Korea kaskazini na Rais wao kwamba Mungu
awape mioyo myepesi na kumrudia yeye.
Mwaka jana Rais huyo aliyerithi nafasi kutoka kwa marehemu baba
yake aliagiza kunyongwa kwa mjomba wake Jang Song -Thaek ambaye alikuwa
mtu muhimu sana kwa taifa hilo kutokana na historia yake katika utawala
na mambo ya siasa kwakosa la kudaiwa kutumia vibaya madaraka yake.
Marehemu Jang mjomba wa Rais Kim akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kukamatwa. ©AFP/Getty Images |
Chanzo GK