Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

HATIMAYE CHRIS MAUKI AJA KIVINGINE! KIVIPI - TWENDE PAMOJA!

 




CHRIS MAUKI ni Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliyebobea katika ‘Saikolojia ya Kijamii na Ushauri Nasaha’. Kwa sasa Chris anafanya masomo yake ya Shahada ya Uzamivu Pretoria, Afrika Ya Kusini katika masuala ya ‘Maamuzi na Matokeo Ya Talaka’ – (matokeo hayo kwa watoto). Chris amekuwa ni baraka kwa jamii ya kitanzania kupitia vitabu, semina na vipindi mbalimbali vya redio na TV ambavyo ameandika na kufanya.

Siku ya jana 02/02/2014 Chris alifunua siri ya mafanikio  na jinsi ya kuandaa mazingira yatakayoleta au sababisha mafanikio hayo.
Chris alianza kwa kusema hivi:
Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kuvipata Lakini kati ya hivyo kuna kimoja ambacho huwezi kukisahau. Wengi tunataka kufanikiwa na tunasoma vitabu vya mafanikio na bahati mbaya Watanzania tunataka mafanikio ya haraka. Kwa hiyo watu wanatamani mafanikio tena ya haraka haraka.

Siku hizi kila kitu ni haraka na ndio maana watapeliwa ni wengi sana. Anayetapeliwa ni kwa sababu anataka au anatamani kupata fedha za haraka.
* Hata wasioongea mafanikio wanatamani mafanikio.
* Na wapo ambao wanaomgea mafanikio ya wengine.

NINI TAFSIRI YA MAFANIKIO / MAFANIKIO NI NINI?

Tofauti ya mafanikio inatokana na tafsiri ya mafanikio.
Mafanikio ni process / mchakato
Utajua mtu fulani kafanikiwa kulingana na tafsiri ya mafanikio.
* Mafanikio yasiyo na maelezo ni tatizo, na mafanikio ya namna aina hiyo lazima kuna Injustice/dhuluma/mapato yasiyo ya haki.
* Dunia ya sasa watu wanataka mafanikio bila process / mchakato.

Mafanikio yanategemeza mchakato mzima wa matendo kuyaendea maafanikio.

TAFSIRI:
Tafsiri ya mafanikio iliyopo ni ''UWEZO WA KUMILIKI'' hii ni tafsiri au mtazamo usio sahihi.
* Ukiingia kwenye mahusiano kwa tafsiri hii utajikuta unaingia kwa speed 100 lakini mwisho wa siku utatoka kwa speed 200, na utaumia.

TAFSIRI / MTAZAMO SAHIHI.
Ni mafanikio ya Ujumla - Well being, yaani ujumla wa utu wa mtu, hali ya kiroho, afya, mahusiano, vile macho yanaweza kuona na vile macho hayawezi kuona. Ni uwiano wa vile vinavyo onekana na vile visivyo onekana.

NJIA ZA KUJITENGENEZEA MAZINGIRA YA MAFANIKIO BINAFSI:

Mafanikio huenda kwa wale walioandaa mazingira ya kufanikiwa. Kwa hiyo mafanikio yanafananishwa na maji ya mvua.
* Tanzania tunaongoza kwa uvivu wa kufikiri
* Uvivu wa kufikiri huleta uvivu wa kutenda

1. Elewa umuhimu wa muda na jifunze kuukomboa
* Kuna tofauti ya kutunza muda na kuukomboa muda ( save time vs redeem time), you can save money but you can't save time. Hata usipoutumia muda utaenda tu!
To redeem means to use effectively / kukomboa muda ni kuutumia muda kiufanisi/kikamilifu bila kuupoteza.
* Epuka kufikiri kuwa una muda, hata kwenye maandiko matakatifu shetani ameambiwa kuwa ana muda mchache na anajua hivyo. Don't buy excuses!

2. Jifunze kujiwekea malengo na kuyafikia
Lengo ambalo hujalioaanisha/hujalihusianisha na muda hubaki kuwa ndoto 'a wish'.
Lengo ukilihusisha na muda utakuwa na focus.

AINA MBILI ZA MALENGO.
Kuna aina mbili za malengo. i>. Malengo ya muda mfupi (short term plan), kama mwaka mmoja hivi.
ii>. Malengo ya muda mrefu (long term plan), kuanzia miaka miwili hivi.
Hivyo usipojua lengo lako ni lipi itakupa shida.

Ili malengo ya muda mrefu yafanikiwe lazima malengo ya muda mfupi yawe yamefanikiwa. Usipofikia pale unatamani kufikia, itabaki kuwa ndoto. Ili ndoto ifikie kwenye uhalisia ''reality'' lazima uiwekee mikakati/malengo.
Ukishindwa kuweka malengo utaishia kuota ndoto.

3. Weka malengo yako kwenye akili.

4. Weka malengo yako moyoni - ili uweze kuyakumbuka kisha yaandike mahali / documentation.
Kisaikolojia, kuna uwezo mkubwa sana wa kukumbuka kitu ulichoandika kuliko usichokiandika.

5. Jifunze kupambana / fight. Pia uwe macho - don't loose focus!

MASWALI MATATU YA KUJIULIZA:
(a) Unataka nini maishani au kwenye malengo yako?
(b) Utatumia mbinu gani kufikia hilo lengo?
(c) Utatumia rasilimali gani - 'resources' kufikia malengo yako?

Sio kila mtu anaweza au anafaa kukufikisha kwenye lengo, mnaweza kuanza pamoja lakini msifike pamoja.
Hivyo basi, kama lengo lako ni kufanikiwa maishani uwe macho unaoa au unaolewa na nani.

UMUHIMU WA KUWEKA MALENGO
1. Malengo yanatusaidia sana kuweza kufikia tulichokipanga.
2. Malengo yanatusaidia kufahamu uwezo wetu (potentiality).
3. Malengo yanatusaidia kuweka kipaumbele ''focus'' kwenye matokeo, itakusaidia kutokuwa  - busy for nothing.

UNAWEZAJE KUKOMBOA MUDA.

1. Fahamu wewe ni mtu wa aina gani ( yaani uwezo wako wa kufanya vizuri ni asubuhi, mchana au usiku)
2. Elewa ni vitu gani vinakupotezea muda
3. Tofautisha kati ya muda bora na kazi bora
4. Kula vizuri - eat well (balanced diet). Uwezo wa kufikiri unategemezwa zaidi na kile unachokula.
5. Jifunze kupumzika - rest is not the waste of time.
6. Epuka kulundika kazi.
7. Tengeneza muda wako mwenyewe
8. Jifunze kusema hapana - ili ufanye mambo muhimu au upumzike.

KATI YA JANGA KUBWA KABISA DUNIANI SIO KIFO  BALI NI MAISHA YASIYO NA MALENGO.

Contacts:
0659 700 002
0756 145 417
0653 100 100 

MWISHO: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 





 


Juu