Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

JITAMBUE SAIKOLOJIA: DONDOO ZA MSINGI KWA WALIOKO KWENYE MAHUSIANO - Part 4.


KATIKA MAHUSIANO:

Kwa kadiri ambavyo wapenzi wakike wanazidi kurusha lawama, kulalamika na kuwa wapinzani, ndivyo ambavyo wapenzi wao wa kiume wanazidi kujikwepa nao, kujiepusha nao, na kujitahidi kuwanyamazia. Kwa kadiri ambayo wapenzi wakiume wanaendelea kujikwepa, kujiepusha na kuwanyamazia wapenzi wao wakike ndivyo pia ambavyo wapenzi wakike huzidi maradufu kulalamika, kulaumu na kuwa wapinzani, “Crazy cycle”. Kama mzunguko huu usiposhuhulikiwa na kuvunjwa mapema tena kwa busara basi mahusiano yenu yanaweza kabisa kuishia kwenye ganzi (mnaishi na mwenzako tu kama mpangaji mwenza na sio “soul mate”) au yanaweza ishia kwenye talaka. Na kwa hali hii ukisikia mwenzako ana “cheat” wala usihamaki na ku ‘panic” kwasababu hapa ndiko mbegu ya “cheating” inawekewa mbolea, nafahamu kabisa uliyeko kwenye hii “cycle” unaelewa ninazungumza nini.

Sio marazote wapenzi wetu wa kike wanapokinzana na sisi, kutupayukia, kukwaruzana na kuwa wabishi wanamaanisha hawana heshima kwetu, wanatudharau, wanatabia mbaya na labda hawajakuzwa vema, la hasha! Mara kwa mara hiyo ni lugha ya jinsia ya kike kupaza sauti kwako kuomba umpende, umpende zaidi, umpende kama zamani. Yamkini tafsiri yako ya kumpenda inayopelekea wewe kufanya unayoyafanya ukihisi yeye naye anatafsiri ni penzi kumbe sivyo. Chukua nafasi ya kumfahamu na kufahamu tafsiri halisi aliyonayo yeye, halafu mpende kwa tafsiri ile. Unapompenda mpenzi wako kwa tafsiri ya penzi aliyonayo yeye, unampa nafasi pia yeye kukupenda kwa ile tafsiri ya penzi uliyonayo wewe. Taratibu utaona ile mikikimikiki na mikwaruzano inapungua. Mahusiano yenu yanajawa na utoshelevu wa moyo, jambo ambalo wengi wetu ni mashahidi kuwa hautilipati kwenye mahusiano yetu “NI UELEWA TU, WALA SI UCHAWI”.

Katika utafiti uliofanywa kwa wanaume 400 walio ulizwa swali kuhusu kupendwa au kuheshimiwa na wapenzi wao wakike, asilimia 74 ya wanaume walijibu "ni bora niishi na mwanamke anayeniheshimu hata kama hanipendi kuliko kuishi na mwanamke anayenipenda lakini haniheshimu". Majibu ya wanaume hawa hayamaanishi kuwa wanaume hawa hawahitaji kupendwa bali kwao penzi ni kama CHAKULA na kuheshimiwa ni kama MAJI. Wanaweza kuishi pasipo chakula lakini sio pasipo maji. Sasa hapa kazi kwako kwenye kutafuna, kumeza au kutema.

Chris Mauki.
Saikolojia Ya Jamii Na Ushauri - UDSM.

Inaendelea...
Usikose Part 5
0659 700 002
0653 100 100

NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU 26,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.

JITAMBUE SAIKOLOJIA: DONDOO ZA MSINGI KWA WALIOKO KWENYE MAHUSIANO - Part 3.


KATIKA MAHUSIANO:

Suala la kutaka kuolewa au kutaka kuoa sio tu jambo la kuzungumza kwa kunuia au kutamani bali ni suala la kujitahidi “kuwa”, “it is not just a wish, but a matter of becoming”. Muda unaopoteza kutamani na kuongea tu kuhusu ndoto zako za kuoa au kuolewa ungeutumia vema katika kujitengeneza, ku “qualify” kuwa mume au mke bora. Hata kama unaongea sana na una “wish” sana na wazazi wako wana tamani sana pia kuona unaolewa au unaoa bado yote hii haikufanyi kamwe kuwa “a husband/wife material” kama bado hujaamua kuweka jitihada binafsi kuwa hivyo. Watu hawaoi mtu anayetamani kuwa mke, na hawaolewi na mtu anayetamani kuwa mume, watu wanaoa mke na wanaolewa na mume aliyeonyesha taswira ya kuwa mume au mke hata kabla hajaingia katika taasisi hiyo. Usitegemee ku “qualify” kuwa mume au mke ukishajisajili kwenye taasisi hiyo, “it will be too late” na kwa bahati mbaya wengine wetu tunaishi na wenza ambao ukimtazama kwa mtazamo yakinifu unaona bado anakazana na kujitahidi kuwa mke au mume. Kumbuka!! Mtu anakuwa rubani kwanza ndiyo anapewa “uniform” baadae, sio anapewa “uniform” kwanza halafu ndiyo akajifunze urubani, “never on earth”

Kila mara katika mahusiano yako zikabili changamoto ukiwa na mtazamo moyoni na nafsini mwako kwamba utashinda, bila kujali ushindi huo unakuja polepole kiasi gani. Kamwe usizikabili changamoto zako ukiwa umeinama moyo na kughubikwa na mtazamo wa kushindwa kwasababu nakuhakikishia "You will go down indeed".

Japokuwa wanaume wanaweza kuwa na uhakika mioyoni mwao kwamba wanapendwa na pia wanawapenda kwa dhati wapenzi wao bado huwa ngumu sana kwa wanawake kuwa na uhakika kama kweli wanapendwa na wapenzi wao.

Sio tu kwamba wanaume na wanawake huona vitu kwa mitazamo tofauti bali pia husikia mambo kwa mitazamo tofauti sana. Ujumbe uleule mmoja waweza kutafsiriwa kwa utofauti mkubwa sana na mara nyingine kuamsha mikwaruzano hususani kama hamjajipanga kuzifahamu tofauti hizi.

Chris Mauki
Saikolojia Ya Jamii Na Ushauri - UDSM.

Inaendelea...
Usikose Part 4
0659 700 002
0653 100 100 

 
NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU 26,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.

JITAMBUE SAIKOLOJIA: DONDOO ZA MSINGI KWA WALIO KWENYE MAHUSIANO - Part 2.


KATIKA MAHUSIANO:

 Huna haja ya kuvaa roho ya mbogo na faru kwa wakati mmoja pale ambapo mpenzi wako wa kiume amesahau siku yako ya kuzaliwa "birthday" au ameikumbuka ila hakuipa umuhimu ulioutarajia wewe. Wewe jiulize mbona mara nyingine yeye anasahau birthday yake mwenyewe? Usilitazame suala hili kama tatizo na kulitolea hukumu kwamba kule kusahau maana yake haupendwi, unadharauliwa, la hasha! Mara nyingine hata yeye aliyesahau hajielewi kwa nini alisahau, tena anaumia nakujichukia kwa nini kasahau. Ni tofauti za kijinsia baina yake na wewe ndizo zinazopelekea zaidi kuibuka kwa suala hili. Wote wawili hamna budi kusaidiana kwa upendo katika kushughulikia issue hii, na msiiruhusu iwaharibie furaha ya siku yenu. "Dont make mountains out of small hills".

Katika mahusiano ni bora tukafahamu kwamba maranyingi tunawasiliana kwa alama "codes", alama hizi huletwa na mambo mengi ikiwemo tofauti zetu za kijinsia. Pale mmoja anaposhindwa kuzisoma codes za mwenzake mikwaruzano huibuka. Nakupa mfano; wapenzi hawa wawili wanajiandaa asubuhi kuondoka kwenda kuanza siku makazini, mwanamke anasema "sina cha kuvaa" moyoni mwake anamaanisha "sina chochote kipya cha kuvaa, vyote vya zamani, nimevichoka". Mwanaume naye anasema "sina cha kuvaa" yeye akimaanisha "hakuna nguo safi iliyoandaliwa ya kuvaa". Sentensi ile ile imetafsiriwa kwa maana tofauti kutokana na kusemwa na jinsia mbili tofauti. Hii inakuonyesha jinsi ambavyo katika mahusiano kila mmoja anaangalia jambo kutokana na mahitaji na mtazamo wake, na mara nyingine kumwona mwenzake anavyotazama sio sahih na hivyo kutofautiana kuwa kwingi, jifunze kuzisoma "codes" za mwenzako. "When you know the right button to press, you will get the right response" fanya tofauti uone rangi yake

Mara kwa mara misuguano inapotokea katika mahusiano unakuta kuna mazingira ya mpenzi mmoja kuangalia zaidi mahitaji au uhitaji wake na kusahau kuupa kipaumbele uhitaji wa mpenzi mwenzake. Inakuwa kabisa kama vile wote mnahitaji hewa sawa ili kupumua lakini kila siku unaona mwenzako anaiminya mirija yako ya kupumulia wakati yeye anaongeza uwezekano wake wa kupumua vizuri. Kamwe hatuishi hivi kwenye mahusiano. Jifunze na ubadilike.

Sio tu uamue kumpenda pale atakapoonyesha mazingira ya kukuheshimu na sio tu uamue kumheshimu pale atakapoonyesha mazingira ya kukupenda. Ukweli ni kwamba haunabudi kumheshimu hata kama mazingira ya kukupenda ni madogo na yeye hana budi kukupenda hata kama mazingira ya kumheshimu yanaonekana kuwa finyu. LOVE and RESPECT ‘equation’ huanzia hapa. Kama kila mmoja kwenye mahusiano akijua jukumu na “call” yake katika mahusiano hayo, baadhi ya mikwaruzano na majibizano yatabaki kuwa historia.

Chris Mauki.

Inaendelea...
Usikose Part 3.
0659 700 002
0653 100 100 




NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU 26,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.

Juu