KATIKA MAHUSIANO:
Kwa kadiri ambavyo wapenzi wakike wanazidi kurusha lawama, kulalamika na kuwa wapinzani, ndivyo ambavyo wapenzi wao wa kiume wanazidi kujikwepa nao, kujiepusha nao, na kujitahidi kuwanyamazia. Kwa kadiri ambayo wapenzi wakiume wanaendelea kujikwepa, kujiepusha na kuwanyamazia wapenzi wao wakike ndivyo pia ambavyo wapenzi wakike huzidi maradufu kulalamika, kulaumu na kuwa wapinzani, “Crazy cycle”. Kama mzunguko huu usiposhuhulikiwa na kuvunjwa mapema tena kwa busara basi mahusiano yenu yanaweza kabisa kuishia kwenye ganzi (mnaishi na mwenzako tu kama mpangaji mwenza na sio “soul mate”) au yanaweza ishia kwenye talaka. Na kwa hali hii ukisikia mwenzako ana “cheat” wala usihamaki na ku ‘panic” kwasababu hapa ndiko mbegu ya “cheating” inawekewa mbolea, nafahamu kabisa uliyeko kwenye hii “cycle” unaelewa ninazungumza nini.
Sio marazote wapenzi wetu wa kike wanapokinzana na sisi, kutupayukia, kukwaruzana na kuwa wabishi wanamaanisha hawana heshima kwetu, wanatudharau, wanatabia mbaya na labda hawajakuzwa vema, la hasha! Mara kwa mara hiyo ni lugha ya jinsia ya kike kupaza sauti kwako kuomba umpende, umpende zaidi, umpende kama zamani. Yamkini tafsiri yako ya kumpenda inayopelekea wewe kufanya unayoyafanya ukihisi yeye naye anatafsiri ni penzi kumbe sivyo. Chukua nafasi ya kumfahamu na kufahamu tafsiri halisi aliyonayo yeye, halafu mpende kwa tafsiri ile. Unapompenda mpenzi wako kwa tafsiri ya penzi aliyonayo yeye, unampa nafasi pia yeye kukupenda kwa ile tafsiri ya penzi uliyonayo wewe. Taratibu utaona ile mikikimikiki na mikwaruzano inapungua. Mahusiano yenu yanajawa na utoshelevu wa moyo, jambo ambalo wengi wetu ni mashahidi kuwa hautilipati kwenye mahusiano yetu “NI UELEWA TU, WALA SI UCHAWI”.
Katika utafiti uliofanywa kwa wanaume 400 walio ulizwa swali kuhusu kupendwa au kuheshimiwa na wapenzi wao wakike, asilimia 74 ya wanaume walijibu "ni bora niishi na mwanamke anayeniheshimu hata kama hanipendi kuliko kuishi na mwanamke anayenipenda lakini haniheshimu". Majibu ya wanaume hawa hayamaanishi kuwa wanaume hawa hawahitaji kupendwa bali kwao penzi ni kama CHAKULA na kuheshimiwa ni kama MAJI. Wanaweza kuishi pasipo chakula lakini sio pasipo maji. Sasa hapa kazi kwako kwenye kutafuna, kumeza au kutema.
Chris Mauki.
Saikolojia Ya Jamii Na Ushauri - UDSM.
Inaendelea...
Usikose Part 5
0659 700 002
0653 100 100
NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU 26,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.
No comments:
Post a Comment