Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

JICHO LA TOFAUTI_MC. HARRIS KAPIGA KATIKA G.T YA CLOUDS FM.

SIKILIZA JICHO LA TOFAUTI HAPA NA MC. HARRIS KAPIGA NDANI YA GOSPEL TRACKS YA CLOUDS FM KAMA ULIIKOSA HII.

Hii ni kuonyesha ni jinsi gani Blog Hii Inakujali mfuatiliaji wangu wa nguvu!
Itakuwa baraka sana kama utaandika comment zako hapa!

KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 






JINSI YA KUTATUA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO: AUNT SADAKA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA NA MAHUSIANO AZUNGUMZA.

     ''Watu wote duniani huwa tuna ndoto za kufanya kitu fulani lakini tumejikuta ndoto hizo
       hazijitokezi bayana kwa sababu ya kukosa UTHUBUTU''.

Migogoro ni ukinzani unaotokana na utofauti wa kiitikadi juu ya watu waaminio juu ya jambo fulani.
Mahusiano ni ukaribu wa watu ambao wana ushabihiano wa dhamira moja aidha dhamira ya kazi, au mapenzi mpaka ndoa.









Migogoro haiepukiki. Katika maisha lazima migogoro itokee kwa sababu ya mambo mbalimbali kama vile kitabia. Lakini wakati huo huo migogoro kwa wakati fulani ni mizuri kwani hutusaidia katika:

          * Kujitambua
          * Kujichuja kujua tabia ya mtu alivyo
          * Husaidia kujua msimamo wa mtu mwingine
          * Husaidia kuchomoza kwa mtu mwingine

Migogoro ya kimahusiano mahali pa kazi, familia na mapenzi hujitokeza na lazima itokee kila tunapokutana katika mzunguko wa maisha ya kila siku.

SABABU ZA MSINGI ZA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA KAZI:
1> Maeneo tutokayo na tuzaliwayo.
     Utofauti wa maeneo ni chanzo cha migogoro kwa sababu kila jamii au familia huzaliwa katika mitazamo 
     fulani, au uthamani fulani. Hivyo utofauti huo huleta migogoro.

Mfano: Mtu kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania hutofautiana kimtazamo, thamani na muonekano wake na aliyetoka mikoa ya kaskazini (Kilimanjaro), hivyo tukutanapo katika maeneo ya kazi na mapenzi huleta migongano awali kisha baadae hupoa.

   Hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kama umetoka katika familia inayoongozwa na upendo basi hata wafuasi
   wa familia hiyo kwa kiasi kikubwa wataongozwa na upendo, lakini mambo yakiwa kinyume na hapo
   basi kazini na hata katika mapenzi itakuwa Pakistani.

2> Muonekano (personality)
     Binadamu hutofautiana. Tumetofautiana katika maeneo makuu manne (katika mawasiliano).

# Namna tunavyotenda mambo yetu, katika kundi hili wapo wanaotenda mambo yao haraka wengine
   kwa wastani na wengine taratibu, hivyo hata katika mapenzi tofauti hizi hujitokeza.

# Tofauti katika mapenzi: Katika uga huu hutofautiana kwa kiasi kikubwa kwani wapo wanaopenda
   kubembelezwa na wale wasiopenda kubembelezwa, wengine wapo kimvuto zaidi na wengine  hapana.

# Masuala ya uchumi na fedha. Watu hutofautiana katika kupata fedha. Katika suala zima la kutunza  
   utumizi wa pesa, migogoro mingi katika familia nyingi Tanzania na duniani husababishwa na fedha kwani 
   watu hutofautiana. Wapo wanaojua kutafuta na kuzitumia fedha, wapo wanaozitafuta na wanakuwa
   wabahili wengine wanaweza kuzitafuta na watafunaji wazuri, Hivyo mtazame vyema mwenza wako na  
   umjue ili muweze kusuluhisha tatizo.

3> Matarajio (expectations)
     Jambo jingine linalosababisha migogoro katika maisha ya kimahusiano ya kikazi na katika kimapenzi ni
     matarajio. Watu wengi huwa na matarajio fulani lakini wengi wao wanapoingia na kukuta ndivyo sivyo
     na matarajio, huibuka migogoro.
Mfano kama unaomba kazi unategemea mshahara mzuri na kukuta sivyo, basi hapo ndipo mgogoro huibuka.

4> Kukosa Imani (lack of trust).
     Kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu katika maeneo ya kazi na mahusiano huzua migongano.
     Katika maeneo ya kazi uaminifu unapotoweka ndipo makundi na unafiki huibuka, pia katika mapenzi
     msipoaminiana lazima kutakuwa na migogoro. Kama miongoni mwenu kuna hisia kuwa unachezea timu 
     mbili basi utaibua mgogoro. Tambua kuwa katika maisha hakuna jambo zuri kama THAMANI; 
     Usimchukulie poa mpenzi wako. Daima elewa kuwa kupenda na kupendana ni kuonesha udhaifu ulio 
     nao kwa umpendaye. Katika mapenzi hakuna kuchukuliana poa.

     Tambua kuwa duniani kuna watu ambao huamini kuwa dunia inaweza kusimama kwa kupiga mluzi, yaani
     kila wanachokisema wao wako sawa na wana haki, watu wa aina hii wanapoingia katika mahusiano basi
     huwa ni hatari. Tabia hii ni heri akawa nayo mwanamme kuliko mwanamke.

5> Ubinafsi (selfishness)
     Watu wengi wana tabia ya ubinafsi hivyo wanasababisha migogoro katika mahusiano ya kimapenzi. 
     Hivyo unapokutana na mtu wa aina hii basi umeumia. Unaweza kuona umekosea na huwezi kuonekana
     kuwa hujui lolote. Watu wa aina hii hata ukimwambia... I MISS YOU...!
     Utasikia: kheeee! Leo umejifunza wapi?... Hivyo unaweza kuwa mtumwa, mwisho huchoka. Ipo athari 
     kama moyo uliopenda ukichoka hasa wa mwanamke kama vile:

@ Moyo wa mwanamke uchokapo ni kama bomu, kwa sababu huingiza maumivu na kutengeneza uvungu
     ambao hutengeneza bomu linalosubiriwa kulipuka.

@ Wanaume wao hubeba mambo, wanapotaka kulipuka hujulikana mapema.

@ Elewa uwekezaji mkubwa katika mapenzi kwa mwanamke ni hisia hivyo mwanamke anapoikosa basi
     hufanya chochote ili aipate. Hivyo wanaume wanatakiwa kuwatunza, kuwathamini na kuwajali vyema
     wake zao. Na uwekezaji mkubwa wa wanaume katika mapenzi ni hisia na fedha, daima moyo uwapo
     katika vuguvugu za kukosa amani basi utafanya ufujaji katika pesa kwa kununua vitu vya thamani ili
     kuitafuta amani iliyopotea, Je? Wanawake wangapi ambao wana magauni mapya ya thamani ambayo
     hayajavaliwa bado na wanaendelea kununua?

Tambua kuwa moyo uchokapo lazima utaingia katika DUARA la umasikini pia elewa kuwa vurugu vurugu za maisha zipo kila iitwapo leo, hivyo ukizikubali vurugu hizo zivunje miguu ya moyo wako utakuwa hoi kutumika.

VITU VYA KUFANYA ILI KUONDOKEWA NA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA KAZI:

Vipo vichocheo viwili ambavyo huweza kuondoa migogoro katika mapenzi na kazi, ambavyo ni:

a) Vitu tunavyoweza kufanya katika hatua yeyote ile (mahali popote)
b) Jinsi ya kutengeneza mahusiano (mapenzi) yenye afya.

Jambo muhimu daima ni kuwa tuingiapo katika mahusiano na kazi, kumpenda mtu hatutarajii kuumia na kuteseka. Yatafakari haya kwako na mengine hapo baadae.
Kisaikolojia hunenwa kuwa lazima uanze na wewe mwenyewe ndipo uende kwa mwingine. Watu wengi maishani hutumia muda mwingi kuwabadilisha wengine badala ya kuanza na wao wenyewe.
Hivyo uonapo hapo ulipo hapakufai anza kuleta mabadiliko wewe.

Vitu vya kufanya katika hatua yeyote ile:

  * Kuwa mtu mzima (grow up)
Hapa haina maana kuwa mtu mzima ni kuwa na ndevu (mabadiliko ya kibaiolojia), bali ni uwezo wa kusimamia mambo yako. Mtu mzima hahukumu watu wengine anapopatwa na migogoro. Mtu mzima hukubali makosa na kufikiria nafasi nyingine yenye usalama zaidi juu ya mahusiano yake.

  * Muombe Mungu akukuze, akupe busara na upeo.
Daima muombe Mungu akupe upeo na busara chanya ili uwe na uwezo wa kuchuja na kuacha mawazo mabaya. Elewa kuwa duniani watu waliofanikiwa ni wenye busara na upeo katika maamuzi yao.

  * Jikubali namna ulivyo.
Kwa bahati mbaya katika maisha wengi wetu hudanganya, na mpaka hujidanganya wao wenyewe. Katika kufanikiwa usijidanganye. Angalia mapungufu ulio nayo na uyafanyie kazi, kubali vitu usivyoviweza kisha fanyia kazi ili uweze.

  *Uwe tayari kujishusha.
Kuwa na tabia ya kuangalia na kusikiliza lakini si kwa kila kitu. Tambua siku zote kuwa ''kusikia si kuona na kuona si kweli''. Daima hakikisha kuwa unajua nini kinaendelea. Pia kuwa mnyenyekevu ingawa kitu kigumu duniani ni kuwa mnyenyekevu.

Watu wengi huona kuwa mtu mnyenyekevu ni mtu aliyeshindwa au ni muoga. Tambua kuwa kukubali ndio ushindi. Kwa nini ubishane?
Unyenyekevu katika mahusiano hususan katika mapenzi ni moja ya silaha  kuu ambayo itaufanya uhusiano wenu kuwa wa mfano. Daima unyenyekevu utawavusha katika mpando na mshuko wenu katika mahusiano. Mungu akiwapa neema hii (unyenyekevu) basi mtakuwa imara na wa mfano katika ndoa yenu.

b) Kichocheo cha pili.
Ni namna ya kujenga mahusiano yenye afya njema. Kila binadamu hupenda thamani yake ipande kila iitwapo leo lakini watu hushushana kila siku. Kila binadamu hupenda, hupendwa na kuthaminiwa.

MISINGI YA KUTENGENEZA MAHUSIANO YENYE AFYA.

a] Mkubali mpenzi wako.
Kama unahitaji kupendwa lazima umkubali mpenzi wako. Mtu anayemkubali mpenzi wake huyo hujiheshimu. Mtu anayejiheshimu hawezi kumdhalilisha mwingine kwani unapomdhalilisha hujidhalilisha mwenyewe.

b] Mheshimu na jiheshimu mwenyewe.
Mtu anayejiheshimu hatumii lugha chafu, huonesha heshima yake kuwa mwanzo wake. Hateremshi chupi ovyo ovyo.

c] Onesha mapenzi kwa kila hali.
Tambua kuwa unapompenda mtu hii humaanisha kuwa umemkubali na umekubali vitendo vyake, namna anavyosema n.k. Wasilisha upendo wako kwa namna zote iwe katika kuongea ama kushirikiana, kuweni marafiki. Neno samahani, ashakum si matusi.

Ngoja niulize kidogo.
'Ni nani yupo tayari kujamba mbele ya mpenzi wake?' (wote kimya)
Mkifikia hapa mjue mpo huru na mnapendana; ukiwa na hofu tambua kuwa hakuna upendo. Daima upendo huanzia machoni, kwenda kinywani, kisha huishia moyoni ambako hutulia tuliiii!!!!!. Bahati mbaya siku hizi mapenzi huanzia katika zipu au mfukoni.

d] Pokea na utoe mapenzi.
Ukiona kuwa wewe ni wa kutoa au kupokea mapenzi siku zote za mahusiano yenu basi unatakiwa uondoke mapema. Au anza upya.

e] Jipende mwenyewe.
Kumbuka kuwa huwezi kufanya mambo yote haya kama hujipendi wewe mwenyewe. Kama utajipenda wewe mwenyewe basi utajua namna ya kupenda. Ukimuona au ukisikia mtu anasema kuwa yuko tayari kufa kwa ajili yako huyu achana naye maana huweza kukuacha pia hata wewe ukitokwa na uhai. Pia kama mpenzi wako amekugeuza baba au mama basi achana naye. Omba Mungu akupe uwezo wa kumpenda na uwezo wa kuwa mkamilifu siku zote. Nyakati zote muombe Mungu, ukiwa katika unyenyekevu.

f] Daima muombe Mungu.
Daima omba Mungu kwani yeye hutuwazia mambo mema siku zote na majibu yake huwa ni ndiyo, si sasa na nina mawazo au mpango mzuri.

DONDOO MUHIMU:

// Uvumilivu katika mapenzi ni muhimu. Elewa kwa moyo uliopenda hauchoki wala kuhukumu, uko hai siku 
  zote.
// Unapoamua kumsamehe mtu samehe na kusahau. Na kama hujamsamehe kwa wakati huo mwambie ili 
   ajue na atafute mbinu m'badala ya kukuomba radhi.
// Zipo tabia ambazo hutokana na mazingira, kaeni chini muelimishane.
// Usione aibu katika mapenzi, elezaneni ukweli.
// Jifunzeni kutafuta chanzo na kiini cha tatizo.
// Ni vyema kuwa na mahusiano yenu binafsi. Pia kuelewa ndio jambo muhimu katika maisha.
// Usiingie katika mapenzi (mahusiano) kiupofu.
// Msome mwenzi wako.
// Mapenzi ni namna unavyomuonesha, unavyosema, matendo na ukifanyacho juu ya umpendaye. Fanyia kazi
   mahusiano yako.
// Pesa ni upendo siku zote. Usikubali kuingia katika mahusiano kwa sababu ya pesa.
// Mawasiliano ni muhimu. Muulize mpenzi wako namna anavyotaka apendwe na wewe .
// Nyumba ndogo ni hatari.
// Mtu anayependa kweli hachoki. Mtu hupenda mara moja.
// Usiingie ukurasa mpya wa mapenzi mapya kabla ya kuufunga wa awali.
// Elewa kusamehe na kusahau ndiyo nguzo ya mahusiano.
// Utandawazi usitufanye tuache mila na desturi za upendo wa kifamilia au kuwapeleka kwa bibi na babu.
// Mpenzi wako akifunga virago pengine anahitaji SAIKOLOJIA PUMZISHI (rest psychology) akizidi
   mueleze kuwa siku nyingine ukienda nitakuacha uende jumla.
// Msaidie kujaza imani iliyotoka juu ya mapenzi.
// Elewa kuwa watoto wana haki ya kuona baba na mama hata kama mkiachana.


BLOG HII INAKARIBISHA MAONI, ASANTENI.

KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 
















Juu