Daima fikra ya mali isiyo kadiri ni mzigo usiochukulika ndivyo LIFE CHANGERS MEDIA chini ya mtumishi wa Mungu, Mwinjilisti, Mwalimu na Mjasiriamali MDEE JUNIOR [
], naamini kuwa mafanikio huanza kwa fikra ya mtu kupata chakula bora cha ubongo, kwani moyo wa mtu hulogwa na upendo ila fikra komavu ziletazo uzalendo na mabadiliko hutokana na elimu ifaayo.
Hii ni kwa sababu maarifa yafaayo huja kwa elimu ifaayo. Hivyo Blog hii inaendelea kuwaletea elimu sana wasomaji wake wote ambao wanahitaji kupiga hatua Kiuchumi kwa kuwapa maarifa toka kwa Watanzania wachache wazalendo wenye utayari kutoa maarifa ya namna ya kufanikiwa katika mipango waliyo nayo ya kimaisha. Hakika elimu hii itakutoa katika ulimbo ambao ulikuwa umekunasa mithili ya kundi la ndege lisilojua ulimbo ulipo.
Sikiliza mazungumzo ya watu wengine.
Mfano ni mimimwenyewe nilitamani kuwa kama Erick Shigongo tangu nikiwa darasa la sita ndoto hiyo nilikuwa nayo hadi sasa amekuwa rafiki yangu na Dr. Reginald Mengi huwa nawasikiliza na kujifunza toka kwao. Na ili kuweza kuulisha ubongo wangu na kuuchavusha kila mwezi nimejiwekea ratiba ya kujinunulia kitabu kimoja.
''Kumbuka kuwa maana japo ya wino hafifu ni bora kuliko kauli nzito''
7] Kuwa mwenye afya njema (physical fit).
Tambua kuwa mwili wako unaweza kukufanya usifikie mafanikio yako, inasemekana kuwa magonjwa ya mwanadamu chanzo chake ni mfumo wa maisha yake. Hivyo ukiujali na kuutengeneza vyema mwili wako kwa uangalifu utaondoa hofu ya kifo, hofu ya kutokufikia malengo yako. Jali maisha yako.
8] Kuwa mwenye tabia njema (social wellbeing).
Je, nikija mtaani kwenu nitasikia watu wanasema nini juu yako. Tambua kuwa watu ni mtaji. Unapokuwa na watu jaribu kuwa msikilizaji tu.
Wape nafasi wakueleze vya kwao ya kwako yawe ya mwisho. Usiwe mbishi. Tengeneza mahusiano ili uweze kuwa na sifa njema ambazo hata mtoto wako zinaweza kumbeba hapo baadae.
Namna ya kutengeneza mahusiano yenye tija katika jamii yako.
* Shirika katika shughuli mbalimbali kama vile harusi, misiba n.k
* Usiwe mbishi
* Shiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiutamaduni kwani mtu hujitengeneza anavyotaka kuwa.
* Hakikisha uwezo ulio nao unajulikana kwa watu
* Ondoa uoga
* Fanya vitu vyako vionekane
* Tambua kuwa imani na kumtanguliza Mungu katika kila ulifanyalo, kwani imani inakusaidia kukabiliana na hofu
* Amini kuwa umeumbwa kwa makusudi maalum. Jiulize wewe mwenyewe kuwa upatapo changamoto huwa unamtumaini nani?
CHANZO / ASILI YA HOFU
Hofu huweza kutokana na:
/ Picha zilizojengwa akilini mwetu.
Hii husababishwa na mazingira ambayo mtu husika amekulia au anayoyaishi ama aliyoyaishi.
Mfano, mtoto mdogo wa kike anaweza kubakwa na mwanamme hivyo kila atakapokuwa anamuona mwanamme atakumbuka tukio hilo.
/ Kupandikizwa na watu wengine.
Hii inatokana na maneno tunayonenewa na ndugu, jamaa na marafiki zetu pindi tuamuapo kufanya jambo fulani hususan mambo yajayo kinyume... kauli kama hizi ''tulijua tu hautaweza''
/ Taasisi za kijamii. ( familia, elimu, mfumo wa nchi )
Mazingira ya nyumbani huweza kusababisha hofu katika maisha yetu.
mfano, taasisi ya ndoa kila leo unakuta vurugu tu baba au mama huweza kupanda mbegu ya uoga kwa watoto. Pia kutoandaliwa vyema kielimu husababisha hofu.
/ Mfumo wa nchi ( mfumo wa kiuchumi ).
Tulifuata misingi ya ujamaa katika uchumi wetu kwa kufanya kazi kwa pamoja, hakuna aliyefanya kazi pekee lakini sasa tupo katika mfumo wa kibepari unaoruhusu mtu mmoja kumiliki njia kuu za uzalishaji mali na kumudu shughuli zote. Hivyo, mfumo wa uchumi unapobadilika huweza kuzua hofu.
/ Uongozi.
Ukiwa na kiongozi muoga basi watu wake wanaomfuata watakuwa waoga.Hivyo, kiongozi lazima awatoe watu wake hofu na woga.
Tambua kuwa:
* Kuanza si kupitia mahali pazuri, lazima upitie changamoto
* Usijihisi mnyonge kwa sababu dunia ya sasa haiwataki wanyonge.
* Anza wewe mwenyewe
* Usikurupuke katika kutenda au kuamua.
* Penda kufanya kitu ukipendacho.
* Tambua kuwa hata unapojihisi umefanikiwa usisahau mambo yaliyokufanya ufike hapo hasa changamoto
* Wakati mwingine mafanikio hayaonekani.
WOGA.
Asili yako ni nini
Chanzo chako ni nini
Dawa yako ni ipi
AU
Dawa yako ni yowe
Dawa yako ni woga?
Dawa yako ni umati?
Hakika... waoga hufa maradufu kabla ya kifo halisi..
Comment kama imekusaidia kwa namna moja au nyingine:
contact: 0659 700 002