Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

Ushauri, Maombi na Maombezi.

Listen to Ufahamu sahihi Maisha sahihi by Rafiki255 Tuzungumze #np on #SoundCloud https://soundcloud.com/rafiki255/karibu-shule-ya-fikra

Obama takes blame for operation that killed two hostages!


President Barack Obama on Thursday revealed that an American and an Italian hostage were killed in a covert US counter-terrorism operation on the Afghan-Pakistan border in January, saying he took "full responsibility" for the tragedy.

Making public the previously classified finding, Obama expressed his "deepest apologies" to the families of the two hostages, Warren Weinstein and Giovanni Lo Porto.

Two other Americans linked to Al-Qaeda, including spokesman Adam Gadahn, were killed in operations at around the same time, the White House said.

"Based on information and intelligence we have obtained, we believe that a US counter-terrorism operation targeting an Al-Qaeda compound in the Afghanistan-Pakistan border region accidentally killed Warren and Giovanni this past January," Obama said in an unscheduled statement.

"As president and as commander-in-chief, I take full responsibility for all our counter-terrorism operations, including the one that inadvertently took the lives of Warren and Giovanni, he said.

"I profoundly regret what happened. On behalf of the United States government, I offer our deepest apologies to the families."

Weinstein was snatched after gunmen tricked their way into his home in Lahore on August 13, 2011 shortly before he was due to return home after seven years working in Pakistan.

He later appeared in a video in which, under apparent coercion, he asked the United States to free Al-Qaeda prisoners.

Italian aid worker Lo Porto, 39, disappeared in January 2012 in Pakistan.

Weinstein's widow said in a statement that "we are devastated by this news and the knowledge that my husband will never safely return home."

The White House statement did not identify which US agency carried out the operation, which suggests it was carried out by an intelligence service rather than a military unit.

If confirmed, it would be the latest controversy to hit Obama's counter-terrorism operations, which -- while killing Osama bin Laden -- have relied heavily on secret drone strikes.

"We have concluded that Ahmed Faruq, an American who was an Al-Qaeda leader, was killed in the same operation that resulted in the deaths of Dr. Weinstein and Mr. Lo Porto," the White House said.

"We have also concluded that Adam Gadahn, an American who became a prominent member of Al-Qaeda, was killed in January, likely in a separate US Government counterterrorism operation," it added.

"While both Faruq and Gadahn were Al-Qaeda members, neither was specifically targeted, and we did not have information indicating their presence at the sites of these operations."

In his statement, Obama said the US believed that the operation resulting in the hostage deaths "did take out dangerous members of Al-Qaeda."


Source: AFP


Tamko la Serikali Kuhusu Mauaji ya Watanzania Afrika Kusini.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema leo kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa katika mashambulizi dhidi ya wageni huko Durban na Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Mhe. Membe amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Watanzania watatu wameuwawa katika mashambulizii hayo siyo za kweli.

“Nimehakikishiwa na Waziri wa Usalama wa Afrika kusini, David Mahlobo, asubuhi hii kuwa hakuna Mtanzania kati ya watu wanane waliouwawa, ambao ni raia wa Ethiopia, Zimbabwe, Malawi na Swaziland,” ametaarifu Mhe. Waziri.
Amesema serikali ina taarifa kuwa kuna Watanzania watatu waliofariki dunia nchini Afrika Kusini, lakini hawakuuwawa katika mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni.

“Watanzania hao ni Rashidi Jumanne, ambaye imetaarifiwa alipigwa risasi katika tukio la ujambazi, kilometa 90 nje ya mji wa Durban; mfungwa Athumani China Mapepe, aliyeripotiwa kuchomwa kisu gerezani wakati wa vurugu za wafungwa, na Ali Heshima Mohamed, ambaye alifariki hospitalini kutokana na ugonjwa wa TB,” alieleza Mhe. Membe.

Mwili wa marehemu Mohamed ulirejeshwa nchini jana kwa mazishi. Mhe. Waziri alitaarifu kuwa kuna Watanzania 23 katika kambi iliyotayarishwa na serikali ya Afrika Kusini huko Durban kuhudumia wageni wanaokimbia mashambulizi hayo ya wenyeji, na kuwa utaratibu unafanywa kuwarejesha nyumbani raia 21 walioomba. “Wawili wamesema hawako tayari kurudi.”
Mhe. Membe amesema taarifa ya serikali ya Afrika Kusini inaonyesha kuwa hali ya utulivu imerejea Durban na Johannesburg katika saa 48 zilizopita kutokana na juhudi za Rais Jacob Zuma na kamati maalum ya mawaziri aliyoiteua kushughulikia mashambulizi hayo.

Mapema jana, Mhe. Membe alimwita Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Thamsanqa Dennis Mseleku, na kuelezea kukerwa kwa serikali na mauaji ya wageni na akataka hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha usalama wa Watanzania nchini Afrika Kusini.
Alisema Tanzania inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ambayo imelaani vikali mashambulizi ya Waafrika kutoka nje ya Afrika Kusini. Hata hivyo, Rais Mugabe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), amesifia hatua zinazochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini kukomesha mashambulizi hayo na kurejesha utulivu.
Mhe. Membe aliwataka Watanzania waishio Afrika Kusini na kwingineko nje ya nchi, kujitambulisha kwenye balozi zetu ili iwe rahisi kufuatilia usalama wao na kuwasaidia pale yatokeapo majanga.
“Hatuna takwimu sahihi za idadi ya Watanzania waishio Afrika kusini kwa sababu wengi wao wamekwenda huko kwa njia za panya,” alisema. Inakadiriwa kuna Watanzania 10,000 waishio Johannesburg na Durban.

Akijibu swali la mwandishi wa habari, Mhe. Membe alisema Tanzania inapaswa kutumia utajiri mkubwa wa gesi asilia ilionao ili kuendeleza viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vitakavyotengeneza ajira za kuvutia kwa vijana ili wasikimbilie nchi za nje na kuhatarisha maisha yao.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
20 Aprili 2015. 

Source: www.joelnanauka.com

MAAHUSIANO / UCHUMBA - KUELEKEA NDOA/CHOOSING YOUR MATE.


Shalom_Shalom‬,
Mabibi na Mabwana - Singles & Couples Karibuni kwa meza ya Bwana tupate kula na kunywa pamoja. Namshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa ajili yenu amenichagua niwe mpishi wenu siku ya leo; Nami najitoa kwa nia ya dhati kabisa kwa ajili yenu/yetu sote kwa kusudi jema kabisa la Kujenga na Kupanda.

 Ni mimi ‪‎Mjoli‬ wenu katika KRISTO_YESU‬ Bwana wetu.




1KORINTH 7:1-11, Key Verse Yetu.
Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.... ' Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa ' ...!
NB: Unaweza kutusaidia maandiko mengine ku-support andiko/somo tajwa hapo juu.
Ni ukweli usiopingika kwamba huwezi kuzungumzia Mahusiano ukayamaliza, mahusiano ni mfano wa bahari ambayo ndani yake kuna/imebeba mambo mengi sana na mengi mapya huzaliwa kila iitwapo leo.
Mahisiano ni hali ya kuhusiana/kubaliana/relate/share/patana/connections - na kinyume chake chaweza kuwa sahihi pia.

DONDOO_MUHIMU_UTANGULIZI‬.
* Kuwa na msimamo ( sio kuwachezea wasichana/umiza hisia/feelings zao/tesa mioyo yao)
* Usimwambie msichana kwamba unampenda kama hutamwambia utamuoa
* Mwanaume ndiye anayeanzisha/initiate urafiki
* Kawaida mwanaume ana huruma kwa mwanamke - hawezi kumkatalia mwanamke
* Usiwe omba omba wa upendo, na kamwe usimvulie nguo yako ya ndani ili kumthibitishia/mwonyesha kuwa unampenda, kama zipu yako mbovu ama sketi yako imekatika kifungo - Hima wahi kwa fundi (YESU KRISTO) aweke mambo sawa nawe utakuwa salama.
Tunapozungumzia mahusiano lazima yawe baina/kati ya watu wa jinsia mbili tofauti kike na kiume, ni mahusiano ya urafiki kati ya jinsia hizi mbili ambayo yatapelekea uchumba hatimaye yatapelekea ndoa.
Mahusiano haya yanahitaji maarifa/ufahamu na ustadi. Mahusiano ya uchumba sio kuangaliana usoni ama kukodoleana macho tu basi, Bali ni pamoja na kuulizana maswali magumu na kuzungumza juu ya mambo ya msingi kwa sababu ni kitu/jambo la maisha.

WAKATI_GANI_USIO_MZURI_KUINGIA_KWENYE_UCHUMBA_MAHUSIANO‬!
a> Kamwe usiingie kwenye mahusiano/uchumba kama hujui ‪‎WITO_WAKO‬ - Mungu amekuitia nini.
Mfano: kama huna muelekeo wa huduma (nazungumza na kijana aliyeokoka) - Efeso‬ 4:1, ...' mwenende kama inavyoustahili wito_wenu‬ mlioitiwa.
Kuoa/olewa na mtu asiye na muelekeo ni hatari sana. Ni lazima NIITWE/UITWE pamoja na mke wangu/wako katika huduma.
Muelekeo wa watu wawili ni muhimu - makusudi na nia ya mioyo ipatane/shikane pamoja.
Wito wa Mungu katika maisha lazima uwe nambari moja (1) katika kuoa/olewa, wito/muelekeo/shauku ya moyo iwe ni mapenzi Mungu na sio kutaka tu kutimiza mambo yako/nia zingine (ke/me).
Ndio maana utakuta mke/mume kabla ya kuoa/olewa alikuwa mtumishi mzuri sana na kujitoa sana kwa ajili ya Mungu/BWANA, lakini mara tu baada ya kuoa/olewa huduma inakuwa si huduma tena ama inakufa/zorota au kushney kabisa.
b> Kama umekata tamaa usiingie kwenye mahusiano.
Usifanye maamuzi kama umefishwa/vunjwa moyo - maana 95% ya maamuzi yako yatakuwa mabovu na mwisho wa siku utaujutia uamuzi ulioufanya.

 Itaendelea.

Next: SABABU 11 MBOVU ZINAZOFANYA WATU WAOANE.

Wasiliana na mwalimu wa somo hili:
0766 730 360 / 0659 700 002




HALI YA MWIMBAJI WA INJILI NCHINI SI NZURI, YUPO CHUMBA CHA UPASUAJI SASA, MUOMBEE KAMA VILE HUJAWAHI KUOMBA TENA.



Maombi yako yanahitajika ili Mungu amponye mwimbaji wa muziki wa injili nchini Debora John Saidi ambaye hali yake inaelezwa kwamba si nzuri nasasa yuko chumba cha upasuaji hospitali ya Mwananyamala kuondolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao umesababisha alie kwa maumivu makali.

Upasuaji wa kutoa uvimbe huo ulitarajiwa kufanyika kesho, lakini kutokana na maumivu pamoja na kilio kutoka kwa mwimbaji huyo imebidi kupelekwa chumba cha upasuaji mchana huu. Ambapo mchana wa leo baadhi ya waimbaji wenzake akiwemo Joshua Makondeko, Tumaini Njole walifika hospitalini hapo kumjulia hali. Mdau wangu sema neno la uponyaji kwa ajili ya Debora John Saidi.
Zaburi 103:3-4.





Source: GK.

Debora akilishwa kabla ya kupelekwa chumba cha upasuaji.
Mungu akuponye Debora.



Joshua Makondeko akimnywesha maji Debora.

Magonjwa Ya Moyo Na Presha Sasa Basi...




MARA NYINGI MAZOEA NDIO YANAYOTUFANYA TUJIKUTE TUNAINGIA KWENYE GHARAMA ZISIZO ZA LAZIMA.




NYAKATI HIZI MAGONJWA KAMA YA MOYO / HIGH BLOOD PRESSURE YAMESHIKA KASI NA KUWA TISHIO NA YAMEINGIA HADI KWA WATOTO, UNABAKI KUJIULIZA HIVI MTOTO MDOGO KAMA HUYU HUU UGONJWA KAUPATA WAPI, MWISHO WA SIKU UNAANZA KUMTAFUTA MCHAWI NI NANI... Kiukweli ni lazima tujali ni vyakula vya aina gani tunatumia, Je! Ni vyakula asilia au vimejazwa makemikali ambayo ndio chanzo cha matatizo haya yote?




HABARI NJEMA KWAKO LEO.


Kampuni ya ''Halista Enterprises'' wanasema - MAGONJWA SASA BASI, Ni baada ya kuanza kuzalisha mafuta Halisi ya Alizeti inayolimwa hapa hapa Tanzania.




WASILIANA NAO KWA NAMBA ZILIZOKO KWENYE STICKER YA TANGAZO.
 TANGAZA KUPITIA:   MJ Media - making business known.

ROSINE SWAI: MKALI MPYA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA - AJA NA LADHA TOFAUTI.

MKALI MPYA WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA - LADHA TOFAUTI.
NI Rosine Swai KUTOKA MKOANI KILIMANJARO.

WASILIANA NAYE KWA WHATSAPP: 0759 037 903,
PIA MUDA SI MREFU ZITASIKIKA KWENYE INTERNET NA MITANDAO MINGINE YA KIJAMII PIA UNAWEZA KUTUMIWA WIMBO KUPITIA WHATSAPP KWA NAMBA HIYO HAPO JUU.

ROSINE SWAI: ANAOMBA WAPENDWA NA WADAU WOTE WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA NA HATA NJE YA TANZANIA MUMSAIDIE KU-SHARE HII KWA MARAFIKI MBALIMBALI.

NOTE: HAYA NI MAANDALIZI YA UJIO WA ALBUM YAKE YA KWANZA AMBAYO IKO JIKONI,
MUDA SI MREFU ITASIKIKA MASIKIONI MWA WAPENZI NA WADAU WOTE WA MUZIKI WA INJILI.




Mtafute kwa namba hizi:
0759 037 903, Pia inatumika kwa Whatsapp.




Juu