USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU - KITABU CHA RUTHU. ''SEHEMU YA KWANZA''
UTANGULIZI:
Kioo cha Blog leo kinamtazama mtumishi wa Mungu Ruthu katika kitabu cha RUTHU. Amekuwa KIIO CHA BLOG kwa sababu ni mfano mahususi sana katika kujifunza kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu na ndio ilikuwa siri ya kufanikiwa kwake.
Maandiko Ya Utangulizi:
Marko 4:34
Wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.
Zaburi 25:14.
Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.
Mithali 3:32.
Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA, bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU:
Ni uhusiano binafsi na Roho Mtakatifu, ni kumshirikisha mambo yetu, kuwa na muda naye, kuzungumza naye, kuwa na wakati na Mungu.
Neno la Mungu linatuambia:
* Akawaeleza siri zote kwa faragha - huonyesha ushirika aliokuwa nao.
* Hatuwezi kupata siri za Bwana bila ushirika naye wa binafsi.
* Watu wanafanikiwa kwa sababu wanazo siri za Bwana, yaani ushirika na Roho Mtakatifu.
mfano: Petro, Yohana n.k walikuwa na ushirika na Yesu / Roho Mtakatifu.
* Siri za mafanikio hutoka katika ushirika na Roho Mtakaifu.
Isaya 48:17
BWANA, mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
* Kama hatufundishwi na Bwana hatuwezi kupata mafanikio/faida; bali kufundishwa na kuongozwa na Mungu huleta mafanikio.
Zaburi 32:8
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
* Kila Bwana atakapotufundisha tutapata faida.
* Ushirika na Roho Mtakatifu hufunua siri za Bwana.
Wafilipi 2:1
... Ukiwako ushirika wowote wa Roho'...
2Kor 13:14
Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na Ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
* Ushirika na Roho Mtakatifu hutuletea asili ya Mungu ndani ya maisha yetu.
2Petro 1:3-4
Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa WASHIRIKA wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
* Ushirika na Roho Mtakatifu unatufanya tuwe washirika wa TABIA YA UUNGU.
Mithali 13:20
Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
*Petro alitembea na Yesu, naye akawa na hekima.
Mithali 27:17,19
Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
USHUHUDA WA WATU WALIOKUWA NA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU.
Itaendelea Juma Lijalo, Usikose!