Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

CAPACITY BUILDING CLASS: NIDHAMU KATIKA MUDA Na MC. Harris Kapiga NDANI YA NCHI YA AHADI..

  
Harris Kapiga ni mtu ambaye kwa muda mfupi nilioweza kumsikiliza nimeweza kujifunza vitu vingi sana katika maisha yangu, ushuhuda wa maisha yake unaweza kubadilisha maisha ya mtu yeyote yule ambaye amefika mahali pa kujiona kuwa si chochote silolote anasubiria kufa tu biashara iishe. Natamani kama wewe ni mmoja wapo miongoni mwa watu waliofikia hatua hii, fanya maamuzi ya kuonana na Mc. Harris Kapiga. Mwanzoni mwa blog hii kuna tangazo linasema KARIBU NCHI YA AHADI MINISTRY, Tumia namba ya simu iliyopo hapo au mwishoni somo hili utaona mawasiliano hapo pia unaweza kutumia.


   Baada ya utangulizi huo mfupi naomba twende moja kwa moja kwenye somo la leo linalosema NIDHAMU YA MUDA sanjari na DONDOO KUMI BINGWA KATIKA KUKUWEZESHA KUTUMIA MUDA WAKO, aliyefundisha somo hili ni MC. HARRIS KAPIGA mwenyewe!

Harris alianza na swali kwa umati wa watu waliokuwa wamehudhuria!

MUDA NI NINI? Kila mtu alijibu vile alivyoweza kwa ufahamu na mtazamowake; mwishoni Harris akaja na jibu sahihi kabisa lililomfaa kila aliyehudhuria na ninaamini hata wewe litakufaa sana na utakubaliana naye.

Muda ni kipindi ambacho vitu hutokea _ Time Is a point or a period at which things occurs. Aliendelea kufafanua kuwa kuna aina mbili za muda.

KUNA AINA MBILI ZA MUDA.

1. Muda wa saa (clock time) 
Yaani muda wa saa tulizo nazo kila siku; mfano. katika dakika moja kuna sekunde 60, siku moja ina masaa 24, mwaka una siku 365. Muda wa saa uko fixed maana yake ni kwamba ukipita umepita huwezi kuubadilisha / kuurudisha nyuma. Kwa maana hiyo basi Muda wa kwenye saa hauhusiki na maisha yetu kwa uko fixed.

2. Muda halisi (Real time).
Muda halisi ndio muda wenyewe hasa unaohusika na maisha yetu na tunapaswa kupeleka macho yetu huko. Mfano. unaweza ukakaa mahali mwezi 1. ukadhani umekaa miaka 10 au ukakaa mwaka 1. ukadhani siku moja kulingana na mazingira halisi ya hapo mahali.
Muda halisi ni muda ambao uko kwenye akili, muda halisi unautengeneza wewe. Na kitu halisi unachokitengeneza wewe unaweza kukimiliki. Ukiutengeneza muda wako una uwezo wa kuumiliki.

NJIA TATU ZA KUTUMIA MUDA WAKO.
Kila mtu anaweza kuangukia katika moja ya njia hizi.

1. Kufikiri 2. Mazungumzo / kupiga stori. 
Mfano; ukiwa peke yako na hufanyi kitu chochote lazima kuna vitu vitakuwa vinaendelea ndani yako, unafikiri / unasemezana na nafsi yako; hapo utakuwa unatumia muda.

3. Vitendo / kitendo.
Namna ya kutumia muda imekuwa tatizo sana, tunatumia vibaya rasilimali ya muda. Ni bora kutengeneza muda wako kwa sababu muda wa saa huwezi kuukimbiza, ukipita umepita (clock time). Swali la kujiuliza; je! tangu umeamka umefanya nini au sasa hivi unaposoma ujumbe huu unafikiria nini?
Mafanikio yako katika kitu chochote yanategemea unatumiaje muda wako katika mambo hayo matatu. Zingatia; chochote unachokifanya au unachokitenda lazima kikunufaishe wewe na huko ndiko kutumia muda kwa faida.
Katika kufikiri kuna vitu vizuri vinapita kwenye akili, hivyo basi ni lazima unapokuwa mahali popote hakikisha unakuwa na kijitabu ili uweze kuandika kila wazo linalokujia akilini. Tumia muda wako mwingi kwa kufikiri _ positively. Usipoteze muda wako kwa mazungumzo ambayo hayakuletei faida kwa sababu yatakuwa yanakupotezea muda bila mafanikio.

DONDOO KUMI (10) KATIKA KUKUWEZESHA KUTUMIA MUDA WAKO.

Lazima utambue thamani ya muda ambao unaishi duniani. Kama hautafika mahali ukawa mjeuri hakika utapoteza muda wako. Ukiwa na nidhamu ya muda watu wengi watakuona wewe ni mjeuri kwa sababu utakuwa kinyume na ratiba zao. Mfano ratiba yako inaonyesha muda fulani utakuwa mahali fulani ukifanya jambo fulani, halafu muda huo mtu anakupigia simu eti muende kwenye harusi, sasa ukimuambia sitaweza kwenda kwa sababu nina kazi ni rahisi sana akakuona wewe ni mjeuri tena unaringa.

1. Hakikisha unaandika Ratiba ya Matukio / Vitu / mambo unayoenda kufanya.
Pangia vitu vyako ratiba ya siku. Tanguliza kile ambacho kinakuletea faida. Kabla hujaamka lazima ujue utafanya nini. Fahamu ratiba yako ya siku utafanya nini au kama huwezi ya siku panga ya wiki.

2. Shughuli yeyote / mazungumzo ya maana katika kukuletea mafanikio lazima uyapangie muda, utaanza saa ngapi na utamaliza saa ngapi.
Kitu chochote ambacho ni cha maana katika maisha yako lazima ukipangie muda.

3. Panga kutumia angalau asilimia hamsini 50% ya muda wako katika mawazo au shughuli zenye matokeo ya kukunufaisha wewe. Mfano; naweza kutumia muda wa kufikiria jinsi gani naweza kuiboresha kazi / shughuli ninayoifanya ili iweze kuwa na utofauti na za wengine. Hii itakusaidia kuboresha kile ulicho nacho na mafanikio yake huwa makubwa sana. Lazima utoboze. (Creativity)

4. Angalau tenga dakika 30. za kupanga ratiba yako ya siku.
Ni marufuku kuanza siku yako kama hujaandaa ratiba ya siku inayofuata.

5. Usione aibu kumwambia mtu, samahani sitaweza kuja au usije nina kazi au usinisumbue nina kazi.
Ukiishi kwa kuwafurahisha watu, mwisho wa siku utaumia (itakula kwako). Na huu sio ujeuri m'baya au kiburi au tabia mbaya, hapana ni NIDHAMU. Nidhamu ya muda ni kanuni ya maisha na kufanikiwa (hapa nimeongezea)

6. Jizoeze kutokujibu sms au kupokea simu kwa sababu tu unataka kupokea au kujibu.
Panga muda maalum wa kujibu sms au kupokea simu.

7. Wakati mwingine unaweza ku-block social networks mfano facebook, twitter n.k. kama unaweza, lengo ni kutumia muda kwa manufaa. Hebu jaribu kufikiria miaka kumi nyuma, halafu angalia umefanya nini katika hiyo miaka kumi? halafu fikiria miaka kumi ijayo utakuwa umefanya nini?


mdee junior (mwanaharakati).
   Ki-ukweli baada ya Harris Kapiga kuuliza swali hili, nilitulia kama dakika moja hivi nikafikiria miaka kumi iliyopita; huwezi amini ilinilazimu nijikaze kuzuia machozi yasitoke kwa sababu nilijiona nimepoteza muda mwingi sana halafu hakuna cha maana nilichokifanya ambacho naweza kukionyesha kwa watu.
NB. Siku 21 zinatosha kabisa kubadilisha tabia.

8. Kabla hujapiga simu yeyote jiulize:
a> unataka kupata nini katika simu hiyo, kama ina mantiki na inakunufaisha, piga. Ukitumia muda vizuri kutakuletea maendeleo. Piga simu zenye tija au sms zenye tija.

9. Tenga muda wa kuchat na kupiga simu unazotaka kupiga.
Hakikisha huo muda ulioupanga ukiisha hama hapo ondoka anza kitu kingine kulingana na jinsi ulivyopanga.

10. Wakati mwingine huwezi kumaliza kila kitu lakini hakikisha basi mawazo / mazungumzo yako yanakunufaisha / yanakufaidisha asilimia themanini 80%.

Harris Kapiga ni Mc. na ni Mchungaji kiongozi katika huduma ya NCHI YA AHADI.; pia ni mtangazaji wa kipindi cha Gospel Tracks na Temino, Clouds Fm Radio.

Kama umebarikiwa au unataka kufika nchi ya ahadi unakaribishwa na semina hizi zinafanyika kila siku ya jumapili kuanzia saa tisa alasiri.
Mungu akubariki kwa kushiriki pamoja nami baraka hizi. Ukifanyia kazi hiki ulichojifunza, hakika UTATOBOZA TU! FIKA NCHI YA AHADI UPATE MENGI ZAIDI.

KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 


HJ



Mawasiliano:

+255 659 700 002
+255 756 145 417

mdeejunior@gmail.com
mdee.junior (skype)
@mdee_junior (twitter)

Dream Big As You Grow Big.





Juu