Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

IBADA YA JUMAPILI YA MWISHO - 2012 KATIKA KANISA LA EBENEZER (IPHC), TABATA SEGEREA CHINI YA BISHOP KUNDAEL MREMA.

Ebenezer ( International Pentecostal Holiness Church_IPHC) ni huduma inayoongozwa na Mmissionary, Dr, Bishop Kundael Mrema na ni kiongozi kitaifa. Makao makuu ya huduma hii kwa hapa Tanzania yapo Tabata Segerea, ikiwa na matawi Kilimanjaro, Namanga mkoani Arusha, Mbeya, Iringa, Kilosa Morogoro, Mwanza etc.


Ibada ya leo tar. 30/12/2012 ikiwa ndio jumapili ya mwisho ya mwaka 2012 iliongozwa na Bishop Kundael Mrema. Katika ibada hii mambo makuu matatu yalifanyika.
1. Mahubiri _ Bishop alihubiri.
Neno la msingi lilitoka katika kitabu cha Waefeso 1:15-18
Katika mahubiri yake moja ya vitu alivyosisitiza alisema, namnukuu;  Ili uwe na uwezo kuwa na furaha ya kweli wakati wa majaribu/mateso/shida/dhiki n.k. ni lazima UWE NA UFAHAMU juu ya kile unachokiendea/unachokipitia yaani macho ya moyo wako yatiwe nuru upate kulijua kusudi la Mungu, mwisho wa kunukuu!

Pia katika hali ya kusimamia lile kusudi la mwito wake ambalo kwa hilo Mungu alimuita, alisema; namnukuu:
Mungu ameniita kusimamia mambo makuu mawili kwa kanisa lake.
i> Neno
ii> Kumtolea Mungu ( 2Kor. 9:6-8)
Alisema, Ukiwa na mali/utajiri bila neno ni tatizo kubwa sana, lakini ukiwa na Neno pamoja na vyote Mungu alivyokubarikia ni hakika kwamba utautawala utajiri/fedha ulizo nazo na hutatawaliwa navyo.



 2. Katika ibada hii pia kulikuwa na ibada ya meza ya Bwana.





















 3. Kulikuwa na keki kwa ajili ya wale wote waliozaliwa mwezi Desemba.
            NA HII NDIO KEKI YENYEWE!


HAWA HAPA NI MIONGONI MWA WALE WALIOZALIWA DESEMBA.








Mzee wa kanisa Lukumay(kushoto) na Captain Ntanga (kulia)















Baraka (mch. mtarajiwa)









Blogger (kushoto) akiwa na mwanadada Vick Mallesa (kulia)

Ebenezer ni moto, Ebenezer ni hai,
Long Live Ebenezer (IPH) Church.























NAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2013.

Dream Big, Grow Big.
+255659 700 002
+255756 145 417
mdeejunior@gmail.com
@mdee_junior (Twitter)


Juu