ANANIA MWASOMOLA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA AJA NA KWAITO STYLE.
Anania Mwasomola azungumza na Blog hii. Mwandishi na mmiliki wa Blog hii alikuwa na machache ya kumuuliza kuhusu huduma yake ya uimbaji.
Blogger: Kijana mbona uko kimya sana, vipi uko wapi?
Anania: Niko Mbeya, nina mikutano kadhaa ya Injili. Nataraji kuja Dar mwanzoni mwa mwezi wa nane 2013.
Blogger: Wapenzi na washabiki wako watarajie nini baada ya ukimya huu?
Anania: Washabiki wangu watarajie mambo mazuri. Nakuja tena kwenye kazi ya Mungu na albamu ya pili.
Ni kitambo sija toa nyimbo mpya tangu nilipo achia albamu ya WEWE NI BABA ambapo hadi sasa video yake imekamilika na mwezi wa nane itakuwa sokoni. Wakati huo huo albmu yangu mpya ambayo jina nimelihifadhi nitaliweka wazi nikikamilisha kazi ila kwa wale wapenzi wa nyimbo za taratibu,wajiandae kupokea, Mungu kanipa nyimbo ya taratibu moja naamini itawagusa wengi sana kwa neema ya Mungu.
Blogger: Umesema kwenye albam mpya kuna wimbo mmoja wa taratibu, zilizobaki zipo kwa style ipi?
Anania: Nimetumia kwaito style kwenye nyimbo zangu naamini zitawabariki sana, nawapenda wapenzi wangu kama wanavyonipenda.
Blogger: Kwa nini umeamua kuja na kwaito.
Anania: Ooh kwaito naipenda sana kwani haiko kikwaya zaidi kitu ambacho inawafanya watu wamataifa (wasiomjua Mungu) waweze kusikiliza na ni rahisi kuwapata na wakaja kwa Yesu.
Kiukweli waimbaji wa gospel tunapenda kuigana kitaifa sio kimataifa so mimi nakaa kimataifa zaidi.
Anania Mwasomola aliendelea kufunguka zaidi kwa kuwatolea mifano baadhi ya waimbaji anaowakubali.
Mfano ni dada Christina Shusho, wabongo wengi hawa mwelewi anaimba nini, lakini ukienda mataifa ya nje Shusho anajulikana kuliko unao wajua hapa bongo, hii nimeona kwa nchi nilizo tembelea hapa africa.Wanampenda sana Shusho naamini nitafikia viwango vyake na kuzidi.
Pia John Lisu wabongo hawa mwelewi kabisa ila kiukweli ndo mwimbaji wangu sana na mwansasu wana uwezo wa kuimba live muda wowote.
Mwisho. Naomba wapenzi na mashabiki wangu wakae tayari kupokea kitu kipya kutoka kwenye albamu mpya (AUDIO)
Blogger: Mungu akuzidishe kama mchanga wa baharini.
TUMA MAONI YAKO.