Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

KANUNI KUMI ZA NAMNA YA KUJITENGENEZEA JINA AU ALAMA BINAFSI YA KIBIASHARA/HUDUMA.



Kanuni hizi ndizo ambazo nami pia nazitumia:


Jesus Christ has commanded
and authorized me to commission you.
Awali ya yote naomba tujiulize swali hili kuhusu neno alama (BRANDS) ni nini?
Alama katika somo hili tunatafsiri kuwa ni Jina kwa ufupi. Jina ulilo nalo huweza kukuletea heshima na fedha katika jamii ikuzungukayo. Heri kuchagua jina jema... Mithali 2:1.

1. LAZIMA UTAFUTE ULINGANIFU (wakati) KATIKA KILA JAMBO NA ULITENDE BILA KUKOSEA (consistent).
Tambua kuwa kutengeneza jina au alama ni jambo rahisi mno katika jamii.

Mfano.
wewe ni mfanyabiashara wa duka na umezoea kufungua duka lako saa kumi na moja alfajiri basi daima ukumbuke kuwa hiyo ndiyo iwe kanuni yako na ufanye kwa uhakika bila ya kukosea yaani kiutimilifu.

Tukifanya mambo yetu kwa wakati na kwa ukamilifu (umakini) basi itakuwa ni rahisi kutengeneza alama binafsi ya kibiashara.

Tambua kuwa huwezi kujitengenezea jina katika maeneo yako ya kazi, kipaji chako au biashara yako kama hautakuwa na umakini katika shughuli zako uzifanyazo. Elewa kuwa jina au alama huja kulingana na utendaji wako wa huduma kwa wakati na kufanya kwa wakati.

2. KUWA MWAMINIFU NA MUWAZI KATIKA KILA ULIFANYALO. (be honest).Daima kumbuka kuwa ni mbashiri mwema afanyaye ayasemayo kuwa mwaminifu na muwazi katika shughuli zako uzitendazo. Ukweli utakufanya uweze kutengeneza jina au alama binafsi ya kibiashara. Kumbuka kuwa hakuna kitu kizuri au kibaya kama ushahidi wa mdomo. Hivyo kufanya kazi uliyo nayo kwa uaminifu na uwazi katika kila ufanyalo.

3. KUWA NA MTAZAMO CHANYA. (be positive).

Mtu mwenye mtazamo chanya hufikiria mambo chanya. Kufikiri vitu chanya husaidia kuongelea watu wengine vyema. Jifunze kuongelea vyema (chanya) habari za mtu.
Kumbuka kuwa katika biashara ukimuongelea vibaya mtu mwingine unajiharibia na wewe mwenyewe. Tambua kuwa katika biashara daima masikio ya watu hupenda kusikia taarifa mbalimbali nzuri, zinazovutia. Hivyo mtazamo chanya utakusaidia sana kuufanya moyo au nafsi yako kupunguza hofu na migogoro ya kinafsi katika shughuli zako na utajitengenezea alama binafsi ya kibiashara.

4. SAIDIA WATU (engage others)

Heri kutoa kuliko kupokea. Mkono utoao daima ndio ubarikiwao. Unapotoa daima unajitengenezea alama ya biashara. Ukiwasaidia watu katika mambo mbalimbali hata kwa ushauri au fedha kidogo ama maarifa uliyo nayo ishadari na isibu utakumbukwa na kuombewa mema. Hata ukifa utabaki katika mioyo ya watu.

5. HAKIKISHA UPO MARA ZOTE.

Uwepo wako katika eneo ufanyialo kazi mara kwa mara au eneo la biashara ni daraja moja wapo la kujitengenezea alama binafsi ya kibiashara. Tambua kwamba kuwaachia watu wengine kazi au shughuli zako huweza kupata uharibifu, achana na uvivu nenda kazini au eneo lako la biashara ya kila siku hii itakusaidia sana kuendelea na kujitengenezea alama binafsi ya kibiashara. Uwepo wako katika eneo ulifanyialo biashara una faida sana.

6. AMINI KUWA WEWE UKO SAWA NA MTU MWINGINE.

Kuamini kuwa wewe uko sawa na watu wengine waliofanikiwa kutakusaidia kuanzisha na kufanya kitu kama wao na kufanikiwa katika shughuli zako za kibiashara au kazi.
Kujiamini daima huondoa hofu ya kimazingira  au elimu ambayo ni tatizo kubwa.
Kujiamini kwako hujengwa na mazungumzo unayojizungumzia wewe mwenyewe. Kiutaalamu mtu hujiongelea mwenyewe kwa asilimia themanini (80%) wakati asilimia ishirini (20%) ni wengine.
Chunguza namna unavyojiongelea.

7. KUWA WEWE MWENYEWE (be yourself)

Ni kweli kwamba kila mtu ameumbwa na Mungu ila tuna utofauti. Kila binadamu ana upekee wake ambao humtofautisha na mtu mwingine na ndio maana wewe ni wewe tu. Upo uzuri wa kufanya mambo yako kama wewe mwenyewe.
Usijaribu kuishi au kufanya kazi kama mtu mwingine maana unaweza kukwama. Upekee katika ufanyaji wa mambo yako utapata uhuru, kufanikiwa na nguvu hata utakaposhindwa.

8. KUWA M'BUNIFU MWENYE UBUNIFU WENYE TIJA.

Ubunifu ni hali ya kuunda kitu kipya kutokana na mazingira yanayotuzunguka. Hivyo kwa ufafanuzi huo tambua kuwa hakuna jambo jipya.
Mazingira yatuzungukayo ndio tunatakiwa kubuni, ili kujitengenezea jina binafsi la biashara lazima uweze kuwa m'bunifu mwenye ubunifu wenye tija.
Ubunifu huboresha wazo ulilonalo. Tambua ubunifu ni kuwa na nidhamu, kuwa mbunifu katika mazingira , maeneo mbalimbali uliopo ili uweze kujitengenezea alama binafsi ya kibiashara. Hivyo daima keti kitako ili uweze kufikiri namna ambavyo utakuwa tofauti na wengine katika mradi wako, kazi au biashara yako.

9. KUWA MUWAJIBIKAJI (be responsible)

Siku zote wanaofanikiwa ni wale wanaowajibika katika shughuli mbalimbali tuzifanyazo. Kumbuka kuwa uwajibikaji ni nguzo ya kibiashara.
Uwajibikaji humfanya mtu kuwa mkweli. Jijengee msingi wa kukiri pale uendapo ndivyo sivyo kwani ni moja ya uwajibikaji.

10. WAAMBIE WATU WAKO KUWA MOYO WAKO UKO WAPI.

Jenga tabia ya kushirikiana na watu tofauti tofauti waliofanikiwa zaidi. Kuwaambia watu wazo lako ni vyema sana kuwashirikisha watu unao waamini na ni waaminifu, yapo mawazo mazuri utakayoyapata toka kwao. Hivyo ili uweze kujitengenezea alama binafsi ya kibiashara ni lazima ujenge tabia ya kuwashirikisha watu wengine mawazo au wazo ulilonalo.

BADO LIPO TUMAINI, Hii ndio kauli mbiu tunayoenda nayo.


Juu