Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO


KATIKA MAHUSIANO:

 Huna haja ya kuvaa roho ya mbogo na faru kwa wakati mmoja pale ambapo mpenzi wako wa kiume amesahau siku yako ya kuzaliwa "birthday" au ameikumbuka ila hakuipa umuhimu ulioutarajia wewe. Wewe jiulize mbona mara nyingine yeye anasahau birthday yake mwenyewe? Usilitazame suala hili kama tatizo na kulitolea hukumu kwamba kule kusahau maana yake haupendwi, unadharauliwa, la hasha! Mara nyingine hata yeye aliyesahau hajielewi kwa nini alisahau, tena anaumia nakujichukia kwa nini kasahau. Ni tofauti za kijinsia baina yake na wewe ndizo zinazopelekea zaidi kuibuka kwa suala hili. Wote wawili hamna budi kusaidiana kwa upendo katika kushughulikia issue hii, na msiiruhusu iwaharibie furaha ya siku yenu. "Dont make mountains out of small hills".

Katika mahusiano ni bora tukafahamu kwamba maranyingi tunawasiliana kwa alama "codes", alama hizi huletwa na mambo mengi ikiwemo tofauti zetu za kijinsia. Pale mmoja anaposhindwa kuzisoma codes za mwenzake mikwaruzano huibuka. Nakupa mfano; wapenzi hawa wawili wanajiandaa asubuhi kuondoka kwenda kuanza siku makazini, mwanamke anasema "sina cha kuvaa" moyoni mwake anamaanisha "sina chochote kipya cha kuvaa, vyote vya zamani, nimevichoka". Mwanaume naye anasema "sina cha kuvaa" yeye akimaanisha "hakuna nguo safi iliyoandaliwa ya kuvaa". Sentensi ile ile imetafsiriwa kwa maana tofauti kutokana na kusemwa na jinsia mbili tofauti. Hii inakuonyesha jinsi ambavyo katika mahusiano kila mmoja anaangalia jambo kutokana na mahitaji na mtazamo wake, na mara nyingine kumwona mwenzake anavyotazama sio sahih na hivyo kutofautiana kuwa kwingi, jifunze kuzisoma "codes" za mwenzako. "When you know the right button to press, you will get the right response" fanya tofauti uone rangi yake

Mara kwa mara misuguano inapotokea katika mahusiano unakuta kuna mazingira ya mpenzi mmoja kuangalia zaidi mahitaji au uhitaji wake na kusahau kuupa kipaumbele uhitaji wa mpenzi mwenzake. Inakuwa kabisa kama vile wote mnahitaji hewa sawa ili kupumua lakini kila siku unaona mwenzako anaiminya mirija yako ya kupumulia wakati yeye anaongeza uwezekano wake wa kupumua vizuri. Kamwe hatuishi hivi kwenye mahusiano. Jifunze na ubadilike.

Sio tu uamue kumpenda pale atakapoonyesha mazingira ya kukuheshimu na sio tu uamue kumheshimu pale atakapoonyesha mazingira ya kukupenda. Ukweli ni kwamba haunabudi kumheshimu hata kama mazingira ya kukupenda ni madogo na yeye hana budi kukupenda hata kama mazingira ya kumheshimu yanaonekana kuwa finyu. LOVE and RESPECT ‘equation’ huanzia hapa. Kama kila mmoja kwenye mahusiano akijua jukumu na “call” yake katika mahusiano hayo, baadhi ya mikwaruzano na majibizano yatabaki kuwa historia.

Chris Mauki.

Inaendelea...
Usikose Part 3.
0659 700 002
0653 100 100 




NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU 26,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:


Juu