Ile Shule maarufu ya kubadilisha fikra ijulikanayo kwa jina la ''CHIMBO - SCHOOL OF THOUGHT'' Inayofanyika kila siku za Jumapili jioni kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 1:00 Usiku ambapo inakusanya watu/vijana zaidi ya 100 wanaohudhuria kila siku za Jumapili.
Ni hakika ukiwa na maono kama ya Tai, utatamani kila siku upige hatua moja mbele. Ndivyo ilivyokuwa kwa CHIMBO - SCHOOL OF THOUGHT kwa kuwa imelenga kubadilisha fikra za Watanzania na kuwa na mkakati madhubuti wa kuwafikia Watanzania wote kwa idadi yake, MC na Mtangazaji Harris Kapiga (Founder) akishirikiana na jopo zima la CHIMBO - Directors wameanzisha Radio Program ambayo itaanza Jumamosi Hii ya tarehe 07/09/2013 katika kituo cha radio cha Praise Power 99.3 FM kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 11:00 Jioni.
Watangazaji watakuwa ni: Peter Msilu akishirikiana na Sarah K, ambao pia ni miongoni mwa CHIMBO - Directors.
NB: Ile program ya kila Jumapili NCHI YA AHADI inaendelea.
IFUATAYO NI JINGLE YA KIPINDI CHA REDIO CHA CHIMBO, NDANI YA PRAISE POWER RADIO 99.3 FM. Ikiambatana na baadhi ya picha za CHIMBO DIRECTORS waliovalia sare za kijani, pamoja na wadau/washiriki wa CHIMBO.
NI MATUMAINI YANGU KUWA, wewe kama mfuatiliaji wangu mzuri wa Blog Hii Utaendelea kubarikiwa sana kwa sababu nitakuwa nakuletea kila kinachojiri pale CHIMBO Nchi Ya Ahadi.
Nakukaribisha pia CHIMBO Nchi Ya Ahadi, Sinza (zamani kamanyola)tujifunze pamoja, Blog Hii Pia Inakuwepo pale kila siku za Jumapili ambapo utapata fursa ya kuonana nami pia nikiwa kama mmoja wa Directors Wa CHIMBO.
MUNGU AKUBARIKI
No comments:
Post a Comment