Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

Mchungaji Nickson Kallinga (MAN OF WISDOM) ambaye pia ni m'beba maono wa MACEDONIA FOUNDATION, hatimaye awekwa wakfu kuwa Askofu mkuu msaidizi wa Kanisa La River Of Life Tz baada ya uongozi wa juu wa kanisa hilo kumchagua miezi michache iliyopita!
Ibada hii ilifanyika tar. 10 Nov. 2012

Ibada ya kuwekwa wakfu ilifanyika kanisani kwake BETHEL RIVER OF LIFE CHURCH lililopo TOANGOMA, wilaya ya Temeke.
Hati ya uteuzi ilisomwa mbele ya umati mkubwa wa watu na watumishi mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo ya kipekee kabisa.

Askofu Nickson Kallinga aliweka nadhiri ya utumishi, Maaskofu wamuwekea mikono; Askofu mkuu wa kanisa la River Of Life Tanzania LAZARO MOSHI ampaka mafuta. Pia alimkabidhi Biblia pamoja na katiba ya kanisa la River Of Life Tz.

Haya ni baadhi ya maneno aliyoyasema Askofu Mkuu Lazaro Moshi katika hotuba yake:
Katika utumishi wangu (Lazaro Moshi) wa miaka 18 kitu kikubwa ambacho kinatuchosha watumishi ni kuongoza watu wasiotii. Alisema watu wasiotii wamejaa lawama, manung'uniko, alimtolea mfano mtumishi wa Mungu, Musa ambaye aliwaongoza wana wa Israeli jangwani, hali wakiwa na manung'uniko mengi. Mwisho wa kunukuu.

Blog hii inasema nini juu ya Askofu Nickson Kallinga?
Kwanza kabisa amenilea kiroho(He's my mentor for sure), na hivi nilivyo ni sehemu ya kujitoa kwake kunisaidia kuukulia wokovu mara baada ya kumgeukia Yesu.

Mnamo mwaka 2002 alini-support kupitia MACEDONIA FOUNDATION kusoma masomo ya uanafunzi DISCIPLESHIP TRAINING SCHOOL inayoongozwa na shirika la YOUTH WITH A MISSION (YWAM) TZ. Baadae tukatumika pamoja na YWAM, DSM.

Maisha ya Nickson yamekuwa na changamoto nyingi ambazo ndizo zilizomletea utukufu huu. Alikuwa mfanyakazi wa TRA nafasi nzuri kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, Holili Border, Moshi.
Baada ya Mungu kusema naye kwa kina na kumthibitishia kuwa ni yeye amemuita kuitenda kazi yake aliamua kuacha kazi TRA japo ilileta matatizo kwa ndugu zake hata kumhesabu kuwa amechanganyikiwa.
Hatimaye haya tunayoyaona leo ni matunda na matokeo ya KUTII kwake, ALIITII SAUTI YA MUNGU. Kumbuka sio kwamba ametoka TRA na kuwa askofu, la hasha si chini ya miaka kumi iliyopita. Na baada ya kuacha kazi hakurudi na kitu chochote nyumbani bali aligawa vitu vyote huko huko, akarudi mwenyewe mikono mitupu bali moyoni alibeba KUSUDI ambalo ndilo limemuweka hapa alipo leo.

Yapo mengi lakini hayo ni machache katika yale mengi yanayohusu historia ya askofu Nickson Kallinga.








Askofu Nickson Kallinga.









Askofu mkuu Lazaro Moshi wa pili toka kulia.












Nickson Kallinga akitafakari jambo.






















Ombeni Kibatala mmoja wa wanachama wa MACEDONIA FOUNDATION, naye hakukosa kwenye tukio.







Mdee Junior The Dream Big wa pili kutoka kulia.












Bishop Kallinga.












Eneo la tukio.












Bishop Kallinga akiingia eneo la tukio.












    Joshua Kaduma(kushoto) mch. T.A.G Mbezi.












Familia ya bishop Kallinga (mke na watoto wake, Deborah kushoto na Doricas kulia).





































Askofu mkuu Lazaro Moshi akiwa na mkewe.












Bishop Kallinga na mkewe.












Mmoja wa ndugu zake askofu Kallinga akitokwa na machozi ya furaha, aliyedharauliwa leo kainuliwa. Jina la Bwana liinuliwe hakika.










Bishop Kallinga akiweka nadhiri ya utumishi.












Mch. Jeremiah Kiwinda, kiongozi wa kitaifa Youth With A Mission Tz ( YWAM ) akisema neno juu ya Kallinga.










Beate Kiwinda, mke wa Jeremiah Kiwinda ( YWAM).











Jeremiah Kiwinda na mkewe Beate.












Dah, yan kama uliikosa hii kitu pole sana.
Kitu ndafu.











Bishop Kallinga avikwa joho la kwa utumishi.

























Akikabidhiwa katiba ya Kanisa.












Baadhi ya watu niliowahi kufanya nao kazi YWAM (Nixon Sadala, Dr. Debora Carpenter, Kessiah).

























Mungu aibariki kazi aliyoianza ndani ya mtumishi wake Nickson Kallinga.

Long Live Bethel River Of Life Church as well as Macedonia Foundation.

By The Dream Big Blog
Cont. 0659 700 002.
         0756 145 417
email: mdeebn@gmail.com





































«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:


Juu