Kwa sababu hii nalikuandikia ujumbe huu wa mwaka 2013 upate kujitambua wewe binafsi na kile unachomiliki. Na huu ndio ujumbe wa Bwana kwako.
UNA NIIN MKONONI MWAKO?
Kutoka 4:1-10, 20
...BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo....
...Na Musa akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.
Baada ya Musa kumlilia sana Mungu, Mungu alimwambia una nini mkononi mwako?
Kuna mambo kadha wa kadha tunayoweza kujifunza kutoka kwa Musa.
i> Fimbo ilikuwa inamaanisha nini kwa Musa
ii> Fimbo inamaanisha nini katika maisha yetu leo.
Fimbo ya Musa ilikuwa ni zaidi ya fimbo. Iliwakilisha maisha (personality) na utambulisho (identity) yake. Fimbo ilimtambulisha Musa kuwa alikuwa anamiliki kitu gani, Lakini Mungu anamwambia itupe fimbo chini (Surrender) yaani Mungu alikuwa anamwambia Musa kwa lugha ya fumbo ayaachilie maisha yake kwa Mungu (na hii ni kuthibitisha kuwa fimbo iliwakilisha maisha ya Musa), na alipofanya hivyo Mungu aliyabadilisha maisha yake.
Mpango wa Mungu na maisha yetu unaweza kucheleweshwa lakini hauwezi kuondolewa/kupotezwa. Kilicho cha Mungu > Hakuna ambacho Mungu anaweza kupoteza katika maisha ya mtu...''Rejea miaka 40 ya Musa Jangwani akichunga.
Chochote alicho nacho mtu yeyote kiwe chanya au hasi hakiwezi kuwa na maana kama hajakikabidhi kwa Mungu.
Upande wa pili wa maisha ya Musa, fimbo iliwakilisha matatizo aliyopitia (life back ground); inamkumbusha matatizo aliyowahi kupitia. Kwenye maisha usifike mahali ukajiona si kitu, usitazame mazingira unayopitia kwa sababu mazingira yanabadilika, bali mtazame Mungu kwa sababu yeye habadiliki.
Fimbo iliwakilisha uwezo uliokuwa ndani ya Musa ambao haujatumika bado ( Unused Potential).
Usijiangalie na kujitafsiri kama watu wakuangaliavyo na kukutafsiri.
Mstari wa 20. Musa anatoka ukimbizini baada ya kusalimisha vitu vyake kwa Mungu. Kumbe tunapokuwa tumekumbatia vitu vyetu/haki zetu wenyewe tunakuwa tunaishi ukimbizini mahali pasipo na uhuru wa kweli, ni sawa na kuishi utumwani katika nchi yako mwenyewe.
Musa akaichukua ile fimbo ya Mungu mikononi mwake. Hapa tunaona kuwa kabla ya hapo ile fimbo iliitwa fimbo ya Musa; Lakini baada ya kusalimishwa kwa Mungu ile fimbo ilibadilishwa jina ikaitwa FIMBO YA MUNGU hadi leo.
Vivyo hivyo tutakapoyasalimisha maisha yetu/kazi zetu/biashara zetu/watoto wetu/familia zetu/afya zetu na kila kitu kinachohusiana na maisha yetu ndipo vitakapobadilishwa majina kutoka kuwa vitu vyetu na kuwa VITU VYA MUNGU. Paulo mtume anadhihirisha hili pale anaposema; ''Si mimi niishiye bali Kristo ndani yangu'' inaonesha jinsi ambavyo alikuwa ameyasalimisha maisha yake kwa Kristo Yesu (Total Surrender).
Ni mpaka tumeachilia kile tulicho nacho ndipo Mungu atadhihirisha utukufu wake na kukipa uhai. Fimbo ilifanywa kuwa HAI. Hatutafuti kitu kipya ili Mungu atende bali kile kile cha siku zote, na unapokikabidhi haimaanishi Mungu atakunyang'anya la hasha; ndio maana Musa aliendelea kuitumia ile FIMBO.
SWALI NAKUULIZA:
Una nini mkononi mwako ambacho hujakisalimisha kwa Mungu?
Jihoji, halafu salimisha leo kipate kupewa uhai wa Ki-Mungu sasa, na 2013 utakuwa mwaka wako wa kuhuishwa katika kila eneo la maisha yako. Kubali sasa Mungu aanze na wewe, na wewe uanze na Mungu.
Nakutakia kila la kheri katika mwaka huu, maisha yako na kila kinachohusiana na maisha yako kikageuzwe kuwa HAI tena katika Jina La Yesu Kristo wa Nazareth Aliye Hai.
Salamu zangu mimi Mdee, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Halleluyah!
Mawasiliano:
+255659 700 002
+255756 145 417
mdeejunior@gmail.com
@mdee_junior (twitter)
mdee.junior (skype)
Dream Big As You Grow Big.
No comments:
Post a Comment