Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

   Hiki ndicho alichofundisha mtumishi wa Mungu Gasper Madumla kupitia page yake ya NENO LA MTUMISHI. Blog hii imeona vema kukushirikisha nawe upate kile Mungu anataka upokee siku ya leo na ndio kusudi la blog hii. Karibu twende pamoja.

   Pia mtumishi wa Mungu Upendo Benson, na Mary Muna katika kurasa zao za facebook wamezungumza kitu ambacho kitakusaidia kutafakari. Upendo Benson ametoa dondoo (highlight) fupi juu ya mahusiano, ni kazi yako kupanua akili na ufahamu wako juu ya kile ambacho ametoa kama highlight.
KARIBU.


Mtumishi Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiweee……

 NENO:SIMAMA IMARA UKAUONE WOKOVU WA BWANA.
Ninanakusalimu mpendwa katika jina la Yesu Kristo aliye hai,nikimuomba Bwana Mungu afungue moyo wako ili upate kupokea hiki ninachokuletea siku ya leo,maana ujumbe huu umekusudiwa kwako wewe mpendwa usomaye ujumbe huu, na wala si mwingine aliyekusudiwa bali ni wewe.
Ninakuhakikishia kabisa endapo utafanikiwa kusoma mpaka mwisho,Mungu atakufanyia jambo,nawe utapenya kupitia somo hili,litakuwa Baraka sana kwa kila atakayesoma.

Wokovu wa Bwana haupatikani kwa njia nyepesi. Maaana hata maandiko yanatuambia kwamba -yeye takayevumilia hata mwisho ndio atakaye okoka. 

Swala la kuokoka ni jambo la muda mfupi sana yaani ni dakika tu pale utakapokuwa umeongozwa sala ya toba na kumaliza,ila kuna maisha mengine baada ya hapo,hayo maisha ni WOKOVU. 

Na tunaokoka ili tufanye kazi ya Mungu,na sio kwenda mbinguni tu,maana ingekuwa swala ni kwenda mbinguni tu,basi watu wote waliokoka wangekuwa wamekufa tangu siku ile walipookoka,BALI WAPO HAI ILI WAYAFANYE MAPENZI YA BABA NA MWISHO NDIO WAFIKE MBINGUNI. Halleluyaaa..

• Maisha ya wokovu ni mchakato wa maisha ya utauwa
• Utauwa ni maisha ya kumlingana na Mungu,yaani maisha ya UTAKATIFU
• Na kumbuka bila huo utakatifu hakuna atakaye muona Mungu,( Waebrania 12 :14 )
Kumbe ! Yatupasa tuwe watakatifu kwanza ili tuweze kumuona Mungu, Watu wengi utawasikia “ Jamani nimemuona Mungu kwa njia tofauti tofauti, Hali wao si WATAKATIFU,maisha yao yamejaa dhambi tupu,HAPO HAKUNA MUNGU LABDA KUNA mungu . Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mungu na mungu,

^ Mungu = Baba wa Mbinguni aliye hai,Jehova, MUNGU MWENYE NGUVU
^ mungu = miungu ya wapagani,anaweza labda kuwa ngombe,n.k HANA UTUKUFU

Wewe mpendwa endapo utasimama imara kuutafuta uso wa Mungu, Hakika utauona wokovu wa Mungu, na hapo utakuwa ni wa tofauti na pale ulivyokuwa kabla.

Tunasoma KUTOKA 12 : 1-2

“ Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 
Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. ”

Hawa wana wa Israel walikuwa utumwani muda wa miaka 430 (Kutoka 12 : 40 ) ila Mungu alikuwa ana haja nao,Haja ya Mungu ilikuwa anataka ajitwalie utukufu kupitia wao waende kumuabudu Mungu aliye hai,

Kumbuka Mungu akiwa na haja na wewe ni lazima atakupata tu,na atakupandisha juu pindi utakapo tii sauti yake kwa BIDII 

Tunasoma Luka 19 : 29-31

“ Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi, 
akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa. 
Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji. ”

Huyu Punda alikuwa kifungoni yaani alikuwa amefungwa katika NIRA ambayo kwa hiyo alikuwa hana uwezo wa kufanya chochote kile atakacho kufanya isipokuwa ni kufanya yele atakayo bwana wake aliyemfunga.

Halleluuyaaa…

Punda wa sasa anawaeza kuwa wewe,ikiwa umefungwa yaani hauwezi kufanya chochote kile utakacho na kufanikiwa BASI UPO KIFUNGONI shetani yeye ufunga watu,

Sasa tazama pale Yesu anasema “ 31” na alipofunguliwa huyu punda tunaona anatandikiwa nguo zao njiani naye huyo punda anapita kwa heshima kubwa kabisa ambayo hapo mwanzo alikuwa hawezi kuipata kabisaa,kwa sababu alikuwa AMEFUNGWA 

Tena huyo punda baada ya kufunguliwa na Yesu,Bwana Yesu Kristo akampanda,akaka juu yake huyo punda na watu woteee wakapaza sauti zao kwa kelele za shangwe 

Maana tena walikuwa hawamuoni punda bali wanamuona Yesu wa nazareti aliye hai akitembea juu ya punda,MAANA YEYOTE YULE ALIYEMBEBA YESU,SI YEYE ATAKAE ONEKANA BALI NI YESU NDIE ATAKAYEONEKANA BADALA YAKE, 

NA MTU HUYU NI YULE ALIYESIMAMA IMARA KATIKA MAISHA YA UTAUWA ,NA WATU WATAKUPA KIBALI NA HESHIMA KUU, SABABU SI WEWE BALI NI YESU JUU YAKO.

Ooooh,HALLELUYAAAAAA,
Mtu mmoja aseme AMEN,

Najisikia nikuhubirie zaidi,THANKS JESUS 
Kwa kukufanya wewe kuendelea kusoma ujumbe huu,hakika Bwana Yesu ana haja na wewe,maana wewe ni kama huyo mwanapunda ambaye Yesu alikuwa ana haja naye.

Sasa turudi katika andiko la kwanza
KUTOKA 12 : 1-2

Hawa wana wa Israel baada ya kuishi miaka mingi namna hiyo tunaona Mungu anawaambia kwamba mwezi huu utakuwa ni ni mwezi wa kwanza wa miaka kwao,

hii inamaanisha siku ile ndio ilikuwa haswaaa ni siku ya kuokoka kwao, maana hata miezi ilibadilika,miaka pia ilibadilika, KWA SABABU HII “ YAKALE YAMEPITA YAMEKUWA MAPYA” Yaani mtu yeyote mwenye dhambi akija kwa Yesu Kristo mtu huyo anafanyika mpya na Bwana Mungu azikumbuki tena dhambi zake.

• Ukisimama imara utauona wokovu wako
JAMANI MAMBO MENGINE HUJALOGWAAA!
BALI TU ,MUNGU ANATAKA UMTUMIKIE ILI NA YEYE AKUPIGANIE.

Tunasoma Kutoka 14 : 13
“ Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. ”

Ninakuambia hivi ;
Kwa yale makwazo yanayokufanya ushindwe kupokea ahadi za Mungu,leo ndio mwisho wake na hutayaona tena endapo utamaanisha kulichukua somo hili na kulifanyia kazi
Maana njia ni moja tu ,nayo ni YESU KRISTO PEKEE yeye ndio njia na kweli.

Tazama mstari huo,Mungu anasema “ USIWAOGOPE HAO WAMISRI ”
• Magonjwa uliyonayo ni wamisri
• Kufungwa Kutokuolewa/kuoa ni wamisri
• Kudumaa kiroho ni wamisri tu
• Ugumu wa maisha ni wamisri tu N.K

HAYO YOTE USIYAOGOPE WEWE SIMAMA NA YESU KRISTO UKIMTUMIKIA KWA FURAHA ZOTE,MAANA HAO WAMISRI HAUTAWAONA TENA KATIKA JINA LA YESU KRISTO,POKEA…..

Ni ombi langu kwako kuwa,Wakati uombapo usiwe unapenda kuomba mambo ya maisha yanayoharibika,na yenye kupita mfano kuomba kila wakati MUME,MKE,KUJENGA,KUPATA KAZI,KUNUNUA GARI,KUPANDISHWA KAZI NA MAMBO KAMA HAYO, 

Bali wewe taka sana mambo ya rohoni naye yote utazidishiwa omba MUNGU AKUFUNGUE MACHO YA ROHONI,.AKUPE NJAA YA KUMTAFUTA,NA YOTE YA ROHONI,NA HAPO NDIPO UTAWEZA KUSIMAMA IMARA UKAUONE WOKOVU WAKO.




  • Kipengele kinachoitwa kupenda hakina professor wala Dr wala mwalimu wala mtaalam wala police wala rais wala waziri... ukishapenda tu wewe baaasi.... ikifika pa kutendwa utatendwa tu, pa kufanywa zoba utakua zoba tu, pa kudanganywa utadanganywa tu, pa kulizwa utalizwa tu, pa kusalitiwa utasalitiwa tu.. kwenye kipengele hiki cheo hakina kazi na ujanja wako unawekwa kapuni.



    Give all of you to Jesus...and He will make what you think is nothing...into something. What you keep from Jesus-keeps you in confinement...what you give to Jesus-is what defines you. Give Him what you have so He can define you! (John 1:3).



Mungu awabariki kwa kufuatilia blog hii.
Tunakaribisha maoni kuhusu blog hii.

Wasiliana nasi kwa:

+255 659 700 002
+255 756 145 417
mdeejunior@gmail.com (email)
@mdee_junior (twitter)
mdee.junior (skype)

DREAM BIG AS YOU GROW BIG.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

4 comments:

Mdee Junior said...
This comment has been removed by the author.
SESI said...

Mungu awabariki sana kwa kundi hili.

Mdee Junior said...

Je! Bwana amekuhudumia kupitia jumbe za watumishi hawa? Acha ujumbe wako hapa, au maoni!

Mdee Junior said...

Sesi, Mungu akubariki!
Maombi yako ni ya muhimu sana kwetu!


Juu