Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

   
Baada ya kutoka kwenye engagement siku ya jana, blog hii ilielekea moja kwa moja kwenye huduma ya Nchi Ya Ahadi inayoongozwa na Mch. Mpakwa Mafuta, HARRIS KAPIGA. Ambapo seminar isiyokuwa ya kawaida (yenye kubadilisha maisha na mtazamo wa mtu binafsi, personal life changing) ilifanyika kanisani hapo.

   Fundisho kuu lilikuwa ni ''NIDHAMU BINAFSI'' a.k.a SELF DISCIPLINE.
Wazungumzaji wa semina hii walikuwa ni; JAMES MWANG'AMBA (THE CHAMPION), TIMOTHY KYARA na ABELLA BATEYUNGA (MZALENDO).


HIKI NDICHO ALICHOZUNGUMZA JAMES MWANG'AMBA.



James Mwang'amba kabla ya chochote alianza kwa kusema hivi; ''USIPOKATA TAMAA UTASHINDA, USHINDI NI LAZIMA'' Baada ya kusema hivyo ndipo akaingia kwenye mada yenyewe! Twende pamoja naye sasa.





NIDHAMU:

Nidhamu ni uwezo wa kufanya mambo / vitu fulani pasipo kufuata hisia (kinyume na ulivyozoea). Baada ya kutoa tafsiri hiyo fupi iliyobeba shehena ya maarifa na uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu binafsi, James alizungumzia na kufafanua maeneo nane (8) ambayo yanahitaji nadhamu kali.

UNATAKIWA UWE NA NIDHAMU KALI KATIKA MAENEO NANE (8).

1. Eneo la kujiwekea malengo binafsi kila mwaka.

* Kujiwekea fursa/possibilities; mfano. mwaka huu nitafanya a, b, c... ukiendelea zaidi utatoka kwenye mwaka itakuwa malengo ya mwezi hatimaye kila siku.
* Mtu mwenye malengo anajua kule anakoenda, mtu asiye na malengo hawezi kwenda na hajui anakokwenda.
* Malengo yanakupa uwezo wa kudhibiti mabadiliko ya maisha katika dunia.
* Malengo yatakupa FOCUS.
* Siri moja ya mafanikio duniani ni kuwa na FOCUS.
* Malengo yatakufanya uwe namba moja (1), Mafanikio yanakuja kwa kufanya yale uliyojiwekea kuyafanya.

2. Nidhamu ya kufikiri vizuri / clear thinking.

* Ni uwezo wa kufikiri vizuri bila bughudha.
Hapa ananukuu msemo mmoja usemao; Those who cannot go within cannot go without.
* Mali ni uwezo wa mtu kufikiri vizuri / uwezo wa kutumia akili vizuri/zaidi.
Nukuu chanya: 'TATIZO SIO UDONGO TULIO NAO BALI UBONGO TULIO NAO'
* Njia rahisi ya kufikiria vizuri ni kuuzoeza ubongo kufikiri.

3. Nidhamu ya kutunza muda / time management.

- Tatizo tulilo nalo ni kutokutunza muda.
* Maisha ya mtu yeyote yanawakilishwa na kitu kidogo kinachoitwa muda, ukipoteza muda unapoteza maisha yako.
* Kimsingi maisha yako ni muda wako, na muda wako ni maisha yako. Jaribu kujitathmini je! kila baada ya dakika 15 umefanya nini. Usijipe mwanya, usikubali kuchelewa.

4. Nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii / deligent / hard working.

* Hakuna sehemu nzuri ya kufanikiwa kama Tanzania kwa sababu watu wengi ni wavivu, watu wengi sio wabunifu (wana-copy na ku-paste).
* Ukifanya kazi kwa masaa ya kawaida utakuwa na maisha ya kawaida, ukifanya kazi kwa masaa yasiyo ya kawaida utakuwa na maisha ya juu zaidi / yasiyo ya kawaida.
* Kama unapenda starehe, fanya kazi kwa nguvu zaidi kuliko mtu yeyote yule.

5. Nidhamu ya kujitunza kiafya.

6. Nidhamu ya kuweka akiba na kuwekeza.

* Kama huwezi kujiwekea akiba mara kwa mara basi uwezo wa ukubwa haupo ndani yako.
* Kuwekeza ni suala la kuwa na miradi.
* Kuwekeza ni kutumia baadhi ya vitu / kitu ulicho nacho kutengeneza mkondo mwingine wa fedha.
* Ukitaka kuwa maskini tumia fedha zote ulizo nazo na ziada kidogo, fedha ambayo huipangilii itaondoka.

7. Nidhamu ya ujasiri / ushujaa / courage.

* Kila mtu duniani anaogopa kitu fulani, Lakini watu ambao wanapanda juu ni wale wanaoishinda hofu / woga. Kuna hofu ya kweli na isiyo ya kweli.
* Jaribu kuzishinda hofu zako, usipozishinda maisha yako yatabaki pale pale.
* Ujasiri unakufanya uwe na uwezo wa kumiliki mambo makubwa / biashara kubwa.

8. Nidhamu ya kujifunza endelevu / continuous learning.

* Kama kuna udhaifu Tanzania ni udhaifu wa kutopenda kujifunza.
* Mtu yeyote ambaye hana tabia ya kusoma ni sawa na mtu ambaye hajui kusoma.
* Nidhamu ya kujifunza ni Elimu binafsi.

Hivyo ndivyo James Mwang'amba alivyohitimisha; kumbuka haya niliyokueleza ni dondoo fupi tu ya kile alichozungumza. Kupata yote kwa ukamilifu wake unaombwa ufike Nchi Ya Ahadi, Sinza Kamanyola; DSM ni mbele kidogo ya KING's PALACE HOTEL.

TIMOTHY KYARA NAYE ALIACHILIA NONDO ZA UKWELI SANJARI NA DADA ABELLA BATEYUNGA (MZALENDO)


Mch. Timothy Kyara. Alizungumza vitu vingi sana vya msingi kuhusu ''JINSI YA KUJENGA NIDHAMU''.
Katika jinsi ya kujenga nidhamu, Timothy alizungumza mambo makuu matatu ya msingi.





1. Ni lazima ujue / ufahamu unataka kufanya nini.
2. Nini kitatokea kama sitafikia lengo
3. Angalia dalili.
Kupata kwa ukamilifu wake usikose jumapili ijayo tar. 27.







Mzalendo, Abella naye aliachilia nondo za kupona mtu.

Akasema, NIDHAMU NI UHURU.

Alizungumza kwa marefu na mapana ' JINSI YA KUTENGENEZA NIDHAMU YA ROHO '

Ukitaka kujua mengi zaidi, Karibu Nchi Ya Ahadi, Sinza.














Pia tarehe 26 ya mwezi huu ndani ya Nchi Ya Ahadi kutakuwa na mafunzo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa kama vile mkaa wa makaratasi, sabuni za miche n.k.
NB: Mafunzo haya yatatolewa bureeeeeee! Ni kuanzia saa nne za asubuhi; USIKOSE.





Ndani ya Nchi Ya Ahadi utaweza kujipatia kitabu kizuri sana kilichobadilisha maisha ya watu wengi duniani na kuwa matajiri. Njoo na kiasi kidogo cha TSH. 10,000/= upate nakala yako ''MTU TAJIRI BABELI''





Endelea kutembelea blog hii, pia utapata ratiba nzima ya Ibada zinazofanyika NCHI YA AHADI.

Long Live Nchi Ya Ahadi Ministry!

KUMBUKA: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 


HJ




Hakikisha unaacha Comment au maoni yako hapo chini baada ya kumaliza kusoma! Maoni yako yana thamani kwetu na kwa yeyote anayepitia blog hii.

Barikiwa.

Also visit my-zone-solution finder, click here


Mawasiliano:

+255 659 700 002 / 756 145 417

mdeejunior@gmail.com


mdee.junior (skype)


@mdee_junior (twitter)



Dream Big As You Grow Big.

























«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:


Juu