Blog hii imefanikiwa kuhudhuria moja ya motivational seminars iliyofanywa na Ndugu RUGE MUTAHABWA ambaye ni mkurugenzi mkuu mtendaji wa Clouds Tv na Clouds Fm,
Ndugu yangu msomaji na mfuatiliaji wa blog hii, ni moyo wangu wa dhati kwako kukuletea vitu vipya kila siku ili kuhakikisha kuwa unapata kitu cha kuanza nacho mkononi mwako kama channel / mfereji wa kupata msaada wa Mungu, kama ilivyokuwa kwa mtumishi wa Mungu Mussa (Moses), Mungu aliitumia fimbo aliyokuwa nayo mkononi mwake. Je! wajua una nini mkononi mwako? Fuatana nami hapa. Kumbuka kuandika maoni yako.
Tatizo kubwa kwa sasa kwenye jamii yetu inayotuzunguka ni namna ya kujikwamua katika umasikini. Kwa kiwango kikubwa jamii yetu imekwama pale ilipo na kushindwa kusonga mbele ama kupiga hatua zaidi. Kwa maneno mengine ni kwamba; Kila mtu ana ndoto ya mafanikio lakini atawezaje kufikia ndoto yake ilihali ukata (umasikini) umempiga mweleka?
Tatizo sio kwamba watu hawafikirii kufanikiwa bali atawezaje kufanikiwa bila fedha?
'Ugunduzi (innovation) kwa upande wangu ni neno fasaha kuliko watu wengi kutumia neno ubunifu (creativity). Kwa upande wangu mimi, Ruge, ubunifu hauna thamani (Value) kwani wengi wabunifu wamekufa bila thamani. Kwa mfano vijana na watu wengi ni wabunifu wa mawazo lakini ugunduzi umekosekana kuwapa thamani'. Hivyo, tunapofanya ugunduzi lazima pawepo na ubunifu na uthamani wa kitu tunachokifanyia ugunduzi katika jamii.
Sipingi jamii inavyodhani na kuamini kuwa ubunifu upo lakini ugunduzi ndio hupelekea kuwepo thamani na kuweza kupata mafanikio, kila tukigunduacho kilishakuwepo awali ila kinachofanya kiwe na thamani ni ugunduzi pale tunapokibadilisha kutoka kutokuwa na thamani mpaka kuwa na thamani. Vitu vilishakuwepo tayari bali kinachofanyika sasa ni kuvibadilisha katika ugunduzi na kukipa thamani.
Kwa watu waliofanikiwa kwa sasa ni kwa vile vilivyopo wakagundua kuvibadilisha kuvipa thamani.
Mifano ya watu waliofanikiwa kwa ugunduzi ni kama ifuatavyo:
Nchini Tanzania kwanza ni msemaji wa mada hii amabye ni mimi (Ruge), awali nilipogundua redio ya burudani (Clouds Fm), redio nyingi na kubwa zilishakuwepo isipokuwa nilichofanya ni kuipa thamani kwa kugundua kuwa redio zilizokuwepo hazikuwa za kiburudani, Hivyo redio ikaegemea kiburudani kuwaburudisha zaidi Watanzania.
Pili, Bakhresa kutengeneza nazi ya kwenye pakiti na pia maandazi na chapati kugundua mahitaji madogo madogo ya nyumbani ambayo tayari yalishakuwepo na akayapa thamani.
NCHI ZA NJE.
Mtaalamu aliyegundua runinga bapa (flat screen) alibadilisha thamani kutoka runinga za mgongo na kugundua bapa. Kilichopelekea kugundua bapa ni kwa zile za awali kuwa na mgongo ambazo feni ndizo zilisababisha, hivyo akagundua kurekebisha na kubadili thamani kwa kuziuza kwa bei ya juu sana.
Hivyo kwa upande wangu RUGE MUTAHABWA dhana ninayotembea nayo daima ni kugundua ndiko kunaleta mafanikio zaidi kuliko au pengine si ubunifu kabisa. Hivyo basi tuungane kwa hoja ya kuelewa kwamba ugunduzi ndio uletao mafanikio kuliko ubunifu.
Tatizo kubwa katika kugundua ni kukosa muda wa kufikiria. Katika mafanikio ya kiugunduzi niliyofikia kuna siri ambayo nataka nawe upate kuipata nayo ni:
''Kwa upande wangu mimi Ruge, mfano nyumbani kwangu au nikiwa njiani kwenye safari zangu kuna wakati nazima simu, redio, wakati mwingine huwa napaki gari kando na kukaa katika mazingira ya kufikiri. Hapa ni kukaa kimya kusikia sauti ya ndani. Ndipo mawazo ya vitu nilivyofanikiwa huvipata.
Kwa sehemu kubwa ya mafanikio kukosekana kwa watu wengi ni kukosa muda wa kufikiria.

VYANZO VYA UGUNDUZI.
1> Mazingira yanayotuzunguka.
Katika kufanikiwa nimegundua kuwa mazingira yaliyonizunguka ndio kilikuwa kitu cha kwanza.
Mfano wakati napata wazo la kuanzisha redio tayari redio zilishakuwepo kabisa.
Nilichogundua ni kwamba redio ya burudani na masuala yote ya burudani hayakuwepo.
Hivyo nilitumia fursa hiyo kuanzisha redio ya burudani ndipo CLOUDS FM ikaanza na sasa CLOUDS TV
nayo iko hewani. Mfano mgunduzi wa mgodi wa madini ya dhahabu wa Kimberlywa Afrika Kusini
alinunua shamba kutoka kwa mkulima mmoja wa kizungu ambaye alikuwa akifanya shughuli zake ilihali
alikuwa akitamani kupata dhahabu na kwa kuwa alikuwa mkulima hakuwa na mawazo ya ugunduzi baadae
aliamua kuliuza shamba hilo ili aende nchi nyingine kutafuta dhahabu, hivyo aliyelinunua shamba lile mmoja
wa wafanyakazi wake aliokota jiwe na mawe mengine. Mwisho mmiliki wa shamba lilealipofika
alistaajabu kuona dhahabu wakati wale wafanyakazi wake nao hawakujua aina ile ya mawe. Hivyo mzungu
yule alichokifanya ni ugunduzi akabadilisha kupata thamani. Ugunduzi ni kutafuta kilicho bora na kukifanya
kiwe bora zaidi. Tafuta fursa kwa kile ulicho nacho kisha kitumie kupata fursa kubwa ya thamani.
2> Kufahamu thamani.
Sehemu kubwa ya watu ni kutojua thamani yao na kuweza kujua thamani ya hitaji hilo. Hapa ni kujua tatizo lililopo, kusoma mazingira na kisha kugundua. Katika ugunduzi anza na ulicho nacho na kisha kichukulie hatua. Achana na mazoea katika ugunduzi kwani mazoea hudumaza ugunduzi.
Mfano mzuri ni gazeti la Mwananchi, limebadili muonekano wake lakini magazeti mengine tangu Uhuru sura ipo vile vile mpaka sasa tuko kwenye sayansi na teknolojia. Vipo vitu vingi iwapo utafanya maamuzi.
NINI KINATUKWAZA KUGUNDUA.
* Historia ya familia, ndugu zetu wamesababisha kuondoa ugunduzi. Familia nyingi zimelazimisha watu wengi kutogundua bali kukidhi matakwa yao na watu wa karibu yao. Ili uweze kufikia kiwango cha ugunduzi basi hauna budi kujitoa mhanga hata kama utachekwa kwani hata utakapoacha watakucheka tu.
* Uoga.
Watu wengi huwa na uoga wa kufahamu. Elewa kuwa hakuna aliyewahi kufanya bila ya kujaribu. Dunia ni kama bahari itachukua rangi ya mawingu kwa kuwa mawingu ndiyo yako juu nawe pia lenga na angalia mbali.
* Ukosefu wa ufahamu wa kusoma na kujua kile kinachoendelea.
Hivyo kubali unachokifanya.Kubali kujua kile kinachoendelea.
* Ongeza thamani ya kile ukifanyacho.
Weka watu na kuweka thamani ya ukifanyacho. Kitu kingine ni kuwa wavumilivu wa umasikini. Pia usikubali kuuza umiliki wa haki katika kazi.
* Kuachwa nyuma kwenye teknolojia.
Watu wengi teknolojia imetuacha nyuma na hatuendani nayo sambamba.
* Watu unaokaa nao.
Ishi na watu wenye uchu na maendeleo. Wenye kukupa hamasa, kusukumana ili kupata maendeleo. Tambua kuwa wapo watu watakao kukatisha tamaa na kukuonyesha dhahiri vigezo kwamba hutaweza kufanikiwa, wakati mwingine ni kweli lakini tambua kuwa mafanikio yapo nyuma ya ukweli. Pia jambo la muhimu elewa kuwa wakati mwingine bahati mbaya huweza kutoa mawazo mazuri. Hivyo wanao fanikiwa ni wale wanaorahisisha mambo yale yale yaliyopo kisha kuyagundua.
MAMBO YA MSINGI YA KUYAZINGATIA KATIKA KUGUNDUA.
@ Amua kitu cha kuanza.
Katika kutaka kufanya utekelezaji amua kitu cha kuanza nacho. Jitahidi kuweka vipaumbele vyako wewe tu na sio vya mtu mwingine.
@ Lengo lako la mwisho ni lipi?
Katika kufanya jambo lazima ujue lengo lako la mwisho. Hivyo ili uweze kufanya ugunduzi elewa wazo lako la mwisho katika ugunduzi wako. Pia tambua kuwa mwisho wako lazima uwe na kitu cha upekee. Hakikisha kuwa kila unapofanya ugunduzi wako lazima uweze kubainisha upekee wako.
@ Tengeneza mahitaji katika ugunduzi.
Ugunduzi wakati mwingine lazima utengeneze mahitaji. Watu lazima wahitaji na wewe ugundue mahitaji yao. Lakini wakati mwingine tengeneza mahitaji watu wayatake.
Mfano, katika redio kwasasa inabidi pawepo vipindi ambavyo watu watahitaji. Vipindi vingi vimekuwepo tu bila kutengeneza ugunduzi ambapo watu wanahitaji. Ugunduzi huleta uthamani zaidi kuliko ubunifu ingawa mara nyingi huweza kutumika pamoja kwani huleta usambamba.
Hakika jivuno la pekee kwa Taifa ni watu bora ambao elimu bora matunda bora.
Endelea kufuatilia blog hii kwa mambo mazuri zaidi yatakayofungua ufahamu na fikra zako ili kutoka katika maisha/hatua moja hata nyingine.
Blog hii pamoja na wasomaji wote tutabarikiwa endapo utaweka maoni / comment yako hapa chini au hapo juu upande wa kulia kwa kutu-follow kwenye twitter na kuandika maoni yako hapo.
Usikose juma lijalo blog hii itakutana na mtaalamu wa saikolojia na mahusiano, Dr. Aunt Sadaka.
Usikose juma lijalo blog hii itakutana na mtaalamu wa saikolojia na mahusiano, Dr. Aunt Sadaka.
Ubarikiwe.
Dream Big As You Grow Big.
No comments:
Post a Comment