Unto Jesus every knee shall bow and tongue confess that He's Lord!
IT'S ALL ABOUT OVERCOMERS FM RADIO ''ON AIR NOW''!
IT'S ALL ABOUT OVERCOMERS FM RADIO ''ON AIR NOW''!
Kituo cha radio ya Kikristo mkoani Iringa kinachojulikana kwa jina la ''Overcomers Fm Radio'' iliyo chini ya huduma ya Overcomers Power Centre inayomilikiwa na Mtumishi wa Mungu Nabii, Dr. BOAZ SOLLO, sasa matangazo yake yamerudi hewani baada ya kutokea tatizo la kiufundi lililopelekea kutosikika kwa matangazo yake hewani kwa takribani majuma mawili hivi.
Meneja masoko (marketing manager) FREDY MWAKYENDENGE wa radio hiyo alipozungumza na mwandishi/mmiliki wa Blog hii pendwa nchini na nje ya nchi alisema:
''Kwa niaba ya Uongozi wa kituo hiki cha radio nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa wasikilizaji wote wa overcomers fm radio kwa
kutokupatikana hewani kwa muda usiozidi majumaa mawili kutokana na
matatizo ya kiufundi lakini sasa hivi hali imekuwa shwari na
wasikilizaji waendelee kubarikiwa na vipindi vya radio yao pendwa vyenye kuelimisha, kuburudisha pamoja na kuwatoa watu kutoka katika vifungo mbali mbali vya adui shetani. Napenda kuwatangazia kwamba leo
22/7/2013 tumerudi hewani kwa mara nyingine tena''. Mwisho wa kumnukuu.
Aidha bwana Mwakyendenge alitumia nafasi hii kumshukuru mtumishi wa Mungu Nabii na Dr Boaz Sollo wa huduma ya OVERCOMERS POWER CENTRE anayefanyia
ibada zake katika ukumbi wa shule ya Sekondari Togwa mkoani Iringa
ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ovecomers fm radio kwa jitihada alizozifanya
katika kuhakikisha wananchi wa Iringa na maeneo ya jirani wanaendelea
kubarikiwa na radio yao pendwa ya Overcomers.
BLOG HII INAWATAKIA USIKILIZI MWEMA WA 98.6 FM
AMEN!
No comments:
Post a Comment