Kama kawaida ya blog hii, jumapili hii ilikuwa ndani ya kanisa la Ebenezer IPHC Tabata Segerea ambapo mtumishi wa Mungu Rev. Meinralr Anthony Mtitu aliuwasha moto na watu wengi waliponywa kwa namna ya ajabu na pekee sana! Ibada ilipoisha watu hawakutaka kuondoka.
Rev. Meinrald Anthony Mtitu katika fundisho lake alifundisha na kuhubiri zaidi juu ya mambo manne kuhusu tabia za Imani.
MAMBO MANNE KUHUSU IMANI:
Mwanzo 6:9--
Kielelezo ni Nuhu.
1* Imani inamtumaini Mungu hata pale ambapo hapaleti maana yeyote, pale ambapo mazingira yanakataa lakini imani bado inatumaini wakati mtu mwingine akiangalia anaona huku ni kuchanganyikiwa.
Imani inatumaini mahali ambapo katika akili (reasoning) huoni maana - mahali ambapo hesabu zinakataa, formula zinakataa, principle zinagoma, Lakini imani bado inatumaini.
Pale ambapo mazingira yanakataa, ushahidi (facts) unakataa, lakini imani inasema ndio - na hii ndio tabia ya imani.
Kwa imani Nuhu akajenga safina.
Ikumbukwe kuwaNuhu hakuwahi kuona safina hapo kabla, lakini Mungu anamuambia utajenga safina. Pia Nuhu hajawahi kusomea kazi ya kutengeneza safina wala hakuwa engineer.
Hivyo imani inaamini wakati kila kitu hakileti maana. Bali italeta maana utakapotii na kuchukua hatua.
2* Imani haisubiri kuona, kugusa, kuhisi, kunusa au kusikia.
Nuhu alikuwa hajawahi kuona mvua lakini aliamini, maana tangu kuumbwa ulimwengu mvua ya kwanza kunyesha ilikuwa ni wakati wa gharika.
Nuhu alimuamini Mungu kwa kutarajia kuona kile Mungu alichokusudia kufanya.
Nuhu hakujua gharika itakuwaje, lakini alimwamini Mungu.
3* Imani inasubiri haikati tamaa.
Imani ni uwezo wa kusubiri ahadi ya Mungu juu ya neno fulani alilosema bila kukata tamaa.
Ibrahimu anaitwa baba wa imani kwa sababu alisubiri zaidi ya miaka 20 kupata mtoto.
Nuhu alisubiri miaka 120 ndipo mvua ikanyesha.
4* Imani inatii kile Mungu alichosema au kuagiza bila kujali kitakuwa kigumu kiasi gani, au kitakuwa na changamoto kiasi gani. Ndio maana inajengwa kwenye msingi wa neno la Mungu. Neno hili laweza kuwa la jumla (Logos) au maalumu ( Rhema ).
MUNGU AKUBARIKI.
Ukiwa na maoni niandikie upande wa kulia wa blog hii kuna mahali pameandikwa ''WASILIANA NAMI HAPA'' Au mahali pameandikwa ''Client Testimony''
Mawasiliano mengine:
0659 700 002
mdeejunior@gmail.com
No comments:
Post a Comment