Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

Magonjwa Ya Moyo Na Presha Sasa Basi...




MARA NYINGI MAZOEA NDIO YANAYOTUFANYA TUJIKUTE TUNAINGIA KWENYE GHARAMA ZISIZO ZA LAZIMA.




NYAKATI HIZI MAGONJWA KAMA YA MOYO / HIGH BLOOD PRESSURE YAMESHIKA KASI NA KUWA TISHIO NA YAMEINGIA HADI KWA WATOTO, UNABAKI KUJIULIZA HIVI MTOTO MDOGO KAMA HUYU HUU UGONJWA KAUPATA WAPI, MWISHO WA SIKU UNAANZA KUMTAFUTA MCHAWI NI NANI... Kiukweli ni lazima tujali ni vyakula vya aina gani tunatumia, Je! Ni vyakula asilia au vimejazwa makemikali ambayo ndio chanzo cha matatizo haya yote?




HABARI NJEMA KWAKO LEO.


Kampuni ya ''Halista Enterprises'' wanasema - MAGONJWA SASA BASI, Ni baada ya kuanza kuzalisha mafuta Halisi ya Alizeti inayolimwa hapa hapa Tanzania.




WASILIANA NAO KWA NAMBA ZILIZOKO KWENYE STICKER YA TANGAZO.
 TANGAZA KUPITIA:   MJ Media - making business known.

AL-QAEDA YAHUSISHWA NA SHAMBULIO LA WESTGATE SHOPPING MALL


 
SHAMBULIO la kigaidi lililofanywa nchini Kenya Jumamosi iliyopita na watu waliodhaniwa kuwa wafuasi wa Al- Shabab, sasa limeelezwa kutekelezwa na mtandao mpana zaidi wa kigaidi wa kundi la Al-Qaeda.


Baadhi ya wachambuzi na wachunguzi wa masuala ya kiusalama na kimataifa, wameyataja mambo matatu ambayo yanathibitisha pasipo shaka kwamba waliotekeleza tukio hilo la kuvamia, kuteka nyara na kuua watu wapatao 68 katika Kituo cha Biashara cha Westgate, ni wa aina ya kundi ambalo kinadharia na kimatendo linafanana na lile la kigaidi duniani la Al-Qaeda. Mambo yanayotajwa na wachambuzi na wachunguzi hao ni pamoja na mbinu, teknolojia na aina ya watu waliotumika kutekeleza shambulio hilo.

Katika uchambuzi wao, wameeleza kuwa mbinu iliyotumiwa na magaidi hayo kuvamia pasipo kujulikana mara moja na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchini Kenya, lakini pia aina ya silaha walizokuwa nazo, inaonyesha kuwa kundi hilo limeamua kutumia kivuli cha Al-Shabab kufikisha ujumbe kwa dunia kwamba lipo licha ya uongozi wake kubadilika.

Kwamba mbali na mbinu pamoja na teknolojia, pia aina ya watu waliohusika kutekeleza shambulio hilo ambao wamebainika kutoka katika mataifa mbalimbali duniani, ndio ambao wamewafanya wachambuzi na wachunguzi hao waanze kupata shaka kwamba huenda kuna kundi kubwa zaidi lililotekeleza shambulio hilo, ambalo limejivika taswira ya Al-Shabab.

Watu wanaotajwa kuvamia kituo hicho cha biashara na kutekeleza unyama wa kutisha, wanaelezwa kutoka katika mataifa ya Somalia, Uingereza, Marekani na Syria.

Taarifa hizi zinathibitishwa na kauli iliyotolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed ambaye katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera, alisema kuwa Al-Shabab hawakuwa peke yao katika shambulio hilo.

Mohamed aliiambia Al - Jazeera kuwa al-Qaeda ndio waliokuwa nyuma ya tukio hilo na si Al-Shabab.

“Al-Shabab hawafanyi peke yao, hili shambulio ni sehemu ya kampeni ya ugaidi wa kimataifa,” alisema Mohamed.
Waziri huyo alisema zaidi ya magaidi 20 wakiwemo wanawake, walikuwa nyuma ya shambulio hilo na kwamba watu hao wametoka katika mataifa tofauti tofauti duniani.

“Al-Shabab wanataka kujionyesha kwenye ngazi ya kimataifa, hasa baada ya kubadili uongozi na wanataka kuionyesha dunia kwamba wana nguvu bado, hivyo kuwekwa kwenye kundi la kulifikiria,” alisema.

Katika mahojiano yake mengine na kituo cha cha PBS cha nchini Marekani, Waziri Mohamed alisema washambuliaji kama wawili au watatu wamebainika kuwa ni raia wa Marekani na Mwingereza mmoja.

Ni kutokana na taarifa hizo, baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa shambulio hilo la kigaidi lina ajenda zaidi ya Kenya.
Zipo hisia kwamba shambulio hilo halikuwa na lengo la kuiumiza Kenya pekee, kutokana na hatua yake ya kupeleka majeshi yake kwenda kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabab nchini Somalia, bali pia kumuumiza Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye kwa asili anatoka nchini humo.

Obama ambaye nchi yake imekuwa ikiongoza mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi ikiwamo lile la Al-Qaeda, ambapo hivi karibuni ilifanikiwa kumuua kiongozi wake, Osama bin Laden, baba yake ni raia wa Kenya.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa, kitendo cha magaidi kuamua kukishambulia kituo hicho cha biashara cha Westgate, kinatokana pia na ukweli kuwa watu wengi wanaopenda kutembelea hapo ni raia kutoka mataifa ya Magharibi wakiwemo Wamarekani, hivyo ulikuwa ni mkakati wa kumuumiza Obama kwa njia hiyo.

Katika hotuba yake aliyoitoa siku ya Jumatatu, Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, alilielezea kundi la Al-Shabab kuwa ni tishio jipya kwa dunia.



Source: Fahamutz



NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU ISHIRINI NA NNE 24,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.

TANGAZO LA UFADHILI KWA WASANII CHIPUKIZI WA FILAMU NA MUZIKI

1.     Wewe  ni  msanii  chipukizi  wa  filamu au  maigizo ?
2.     Wewe  ni  mwandishi  chipukizi  wa  filamu  ?
3.     Wewe  ni  mtayarishaji  chipukizi  wa  filamu ?
4.     Wewe  ni  muimbaji / mwanamuziki  chipukizi 
 Unataka  kukamilisha  ndoto  zako  lakini  haujui  pa  kuanzia ?  Kama  jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako.
Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  inapenda  kuwatangazia  wananchi  wote  kuwa  sasa,  tumeanza  kutoa  ufadhili  na  udhamini  kwa   wasanii  chipukizi  wa  filamu, waandishi  chipukizi  wa  filamu, watayarishaji ( Producers )  chipukizi  wa   filamu   pamoja  na  waimbaji(wanamuziki ) chipukizi   wenye  sifa  zifuatazo :
1.      Awe  na  kipaji  cha  kuigiza  AU
2.     Awe  na  kipaji  cha  uandishi  wa  filamu   AU
3.     Awe  na  nia  thabiti  ya  kuwa  mtayarishaji  wa  filamu  AU
4.     Awe  na  kipaji  cha  uimbaji.
5.     Awe  raia  wa  Tanzania  na  mkaazi  wa  jijini  Dar  Es  salaam.
6.     Awe  na  umri  wa  kuanzia  miaka  14   hadi   55.
     
     UTARATIBU   WA  KUTUMA  MAOMBI  
Tuma  maombi  yako  kupitia  barua  pepe  yetu  ambayo  ni  : rafikielimutanzania@gmail.com   . Maombi  yaelekezwe  kwa
Mkurugenzi  Mtendaji,RafikiElimu  Foundation, S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.
   AU 
Unaweza  kuleta  maombi  yako  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu. Ofisi  zetu  zipo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU. 
Kufika  katika  ofisi zetu,  panda  daladala  za  UBUNGO- CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  30  SEPTEMBA  2013.
Kwa  maelezo  zaidi   wasiliana  nasi  kwa  simu  0782405936  au  0756606085   

NAWASHUKURU WASOMAJI WANGU, SASA TUMEFIKIA WASOMAJI ZAIDI YA ELFU ISHIRINI 20,000. ENDELEA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE.

SARAH MVUNGI ATAMBULISHA ALBUM YAKE NDANI YA EXCLUSIVE YA _ GEIP.

Muinjilisti SARAH MVUNGI ambaye pia ni MC na muimbaji wa nyimbo za Injili atambulisha Album yake ya tatu inayoenda kwa jina la ''HAKUNA AJUAYE KESHO YAKO'' Baada ya kutamba na album yake ya pili yenye jina ''NIACHENI NIMFUATE YESU'' Sarah Mvungi amesema album zote zipo sokoni na zinasambazwa na UMOJA AUDIO VISUAL.

Sarah Mvungi alikuwa na haya ya kusema baada ya mwandishi wetu wa Blog hii kuzungumza naye ndani ya ''RIVER SIDE HALL'' kupitia project yetu ya ''GOSPEL EXCLUSIVE INTERVIEW PLATFORM chini ya udhamini mkubwa wa Kampuni ya ''HALISTA ENTERPRISES'' watengenezaji na wauzaji wa mafuta halisi ya kupikia ya Alizeti. Kampuni hii pia ndiyo Inayomiliki Blog hii., click hapa uweze KU-LIKE Fun Page Yetu.

Msikilize Sarah Mvungi LIVE hapa.

KAMA ULIKOSA TAMASHA LA RUNGU LA YESU, PICHA HIZI HAPA

Unto Jesus every knee shall bow and tongue confess that He's Lord!

Tamashalililokuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa hatimaye lafanyika kwa kishindo.
Tamasha lilikusanya idadi kubwa sana ya waimbaji wa Gospel Hip Hop na mashabiki kibaooooo!

Twende pamoja.

















Tuwie radhi kwa muonekano wa picha usio mzuri.

Usikose kuangalia video ya Interview kati ya Blog hii na Rungu la Yesu, Allen Chisunga (pastor Peter), Baltazar Paul pamoja na G. (a.k.a. kutana naye) kupitia Page yetu ya: http://www.facebook.com/exclusive.interview kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya HALISTA ENTERPRISES. 
Note: Usisahau ku-LIKE hiyo page yetu.

Barikiwa: 0659 700 002.


HABARI NJEMA KWA WAKAZI NA WOTE WAISHIO MKOANI IRINGA.

Unto Jesus every knee shall bow and tongue confess that He's Lord!


IT'S ALL ABOUT OVERCOMERS FM RADIO ''ON AIR NOW''!


Kituo cha radio ya Kikristo mkoani Iringa kinachojulikana kwa jina la ''Overcomers Fm Radio'' iliyo chini ya huduma ya Overcomers Power Centre inayomilikiwa na Mtumishi wa Mungu Nabii, Dr. BOAZ SOLLO, sasa matangazo yake yamerudi hewani baada ya kutokea tatizo la kiufundi lililopelekea kutosikika kwa matangazo yake hewani kwa takribani majuma mawili hivi.

Meneja masoko (marketing manager) FREDY MWAKYENDENGE wa radio hiyo alipozungumza na mwandishi/mmiliki wa Blog hii pendwa nchini na nje ya nchi alisema:
''Kwa niaba ya Uongozi wa kituo hiki cha radio nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa wasikilizaji wote wa overcomers fm radio kwa kutokupatikana hewani kwa muda usiozidi majumaa mawili kutokana na matatizo ya kiufundi lakini sasa hivi hali imekuwa shwari na wasikilizaji waendelee kubarikiwa na vipindi vya radio yao pendwa vyenye kuelimisha, kuburudisha pamoja na kuwatoa watu kutoka katika vifungo mbali mbali vya adui shetani. Napenda kuwatangazia kwamba leo 22/7/2013 tumerudi hewani kwa mara nyingine tena''. Mwisho wa kumnukuu.

Aidha bwana Mwakyendenge alitumia nafasi hii kumshukuru mtumishi wa Mungu Nabii na Dr Boaz Sollo wa huduma ya OVERCOMERS POWER CENTRE anayefanyia ibada zake katika ukumbi wa shule ya Sekondari Togwa mkoani Iringa ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ovecomers fm radio kwa jitihada alizozifanya katika kuhakikisha wananchi wa Iringa na maeneo ya jirani wanaendelea kubarikiwa na radio yao pendwa ya Overcomers.

BLOG HII INAWATAKIA USIKILIZI MWEMA WA 98.6 FM

AMEN!


UZINDUZI WA ALBAM YA ''AMANI YA BWANA'' YA RUNGU LA YESU KWA UDHAMINI MKUBWA WA KAMPUNI YA HALISTA ENTERPRISES.


UZINDUZI HUU UNAKUJIA KWA UDHAMINI MKUUUBWAAA KABISA WA KAMPUNI YA HALISTA ENTERPRISES WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI WA MAFUTA HALISI YA KUPIKIA YA ALIZETI KUTOKA SINGIDA.
NUNUA MAFUTA HALISI YASIYOCHAKACHULIWA.

MAFUTA HAYA YATAKUWEPO SIKU YA UZINDUZI NA YATAUZWA KWA BEI NZURI KABISA ( REASONABLE PRICE ), USIKOSE KUJA NA PESA UJIPATIE MAFUTA HALISI YA ALIZETI katika ujazo wa Lita 1 Na Lita 5.

Mkurugenzi wa kampuni ya Halista Enterprises atakuwepo na atazungumza!

Ukitaka kujua bei za Mafuta tembelea http://halisitz.blogspot.com/ AU Tupigie 0659 700 002



Juu