Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO






Benson Mahenya: Mmiliki wa Kampuni ya BM PUBLISHERS wachapishaji wa Gazeti La ''Afya Tabibu''











Alianza kwa kusema hivi: 

Ipo kauli isemayo kuwa ''Furaha ya mtu hujitengenezea mwenyewe'' hivyo kufikiri, kuona na kufanya ulichozaliwa nacho ni furaha kubwa sana. Inawezekana tafakuri na fikra zako umetumia muda mwingi na mlango huo uuonao bado ni mlango ambao huoni mpenyo wa kupita lakini ukiuamini na kuchukua hatua kuingia ndani hakika ipo milango mingine saba wazi inakusubiri. Daima elewa kuwa kungoja kwako kunaufanya mlango huo wa kupitia kufungwa. Ili uweze kufika sehemu fulani lazima ukutane na mtu sahihi kwani msaada wako utapatikana pale utakapochukua hatua ya kuanza. Daima mabadiliko huja baada ya kuanza.

Dondoo Muhimu.
kuanza...
kila kitu kilianza...
dunia imekuwako kwa kuanza...
mimi na wewe tuna mwanzo...

Hakika mwanzo tufe ni mvutano.

 MTAZAMO WA BIASHARA TANZANIA.

Mtazamo ni kitendo cha kulielewa jambo na kuuona mwelekeo wake katika ufahamu wa taarifa zake. Pia tunaweza kusema kuwa ni ujenzi wa mawazo juu ya jambo, tukio ama kitu halisi kilichopo au kilichopo katika ulimwengu bwete (kifikra). Hivyo mawazo yako au mtazamo wako juu ya jambo fulani daima haulingani na mtu mwingine.
Amua maisha yako mwenyewe pasipo kusubiri mtu akuamulie. 
Kwa mfano mimi mwenyewe (Benson Mahenya) nilipotaka kujiajiri nilipata vipingamizi sana na kipingamizi kikuu kilikuwa ni familia yangu ikizingatiwa ni kijana wa kwanza kati ya watoto kumi na sita yenye baba mmoja lakini mama tofauti tofauti. Hivyo mshahara wangu wa kwanza na mingine nilikuwa naituma nyumbani kusaidia ndugu zangu nikifikiri kuwa itakuwa suluhisho la matatizo yaliyowakabili ndugu zangu, lakini kumbe ndivyo nilivyozidi kuchelewa kufikisha ndoto zangu. Lakini nilipotambua kuwa yanipasa nijikwamue kwanza mimi kisha wao (ndugu). Niliwekeza katika ndoto zangu hakika sasa nimewaajiri ndugu zangu.

Kwa mtazamo wa kibiashara nchini ni vema kuweza kujua msingi wa mtazamo ambao ni Biashara. Pasipo kujua msingi wa biashara ni vigumu pia kuelewa fursa zake katika kuzifanyia kazi.

Awali ya yote tujue dhana fafanuzi ya neno biashara.
Zipo fasiri nyingi juu ya neno biashara zikiwemo;
Biashara ni kitendo cha kuuza na kununua bidhaa na huduma kulenga faida. Hii ina maana kuwa biashara yoyote lazima ilete faida ama ilenge kuleta faida. 
Unapojihusisha na biashara weka msingi mzuri wenye tija na manufaa utakaokuingizia faida.

Ujasiriamali kwa sasa ndilo neno lenye kusikika masikioni mwa watu wengi sana kwa sasa.
* Ujasiriamali ni shughuli endelevu kupata faida.
* Fasiri nyingine ni kwamba, ni kuona fursa na kuitumia.
* Ni kuona fursa, kuifuata kwa ujasiri na kuitekeleza.
Kuonekana ni neno lisilosikika tena bali ni vitu viwili vyenye mwingiliano mmoja _ UJASIRIAMALI.

VITU VYA MSINGI KATIKA KUFANYA UJASIRIAMALI NA BIASHARA.

Yajue malengo yako:
Katika ujasiriamali na biashara kwa ujumla ni vema kutambua malengo yako. Pasipo kutambua malengo ni kikwazo cha mafanikio na kusonga mbele kwa biashara.
Malengo huwekwa na mhusika mwenyewe wa biashara ama mjasiriamali. Ukiwa mjasiriamali malengo yako ni lazima yatazame kufanikisha kupatikana pesa.

Katika suala la biashara na ujasiriamali pesa ni suala muhimu kwani laweza kusimama na kuchangia kwa sehemu kubwa.
Kuhusiana na suala la pesa ni vyema ukajua malengo yako na kutaka uzifanyie nini. Katika kulenga pesa elewa utazitumia kwa ajili gani na matumizi yapi yatafanyika kukupeleka mbele au kusonga na kupiga hatua zaidi.

Unapolenga pesa katika kuzihitaji usiiangalie pesa bali kufikia malengo yako. Mfano kusomesha watoto, kupanua mradi wako.
Ukiwa mfanyabiashara mwenye mtazamo wa kusonga mbele hakikisha biashara yako inakupa faida. Boresha biashara yako upate faida kubwa. Ubunifu wenye ubora utakupa faida yenye manufaa katika biashara yako. Jenga tabia ya kufanya marekebisho yenye kuboresha biashara yako ili uwe na soko la uhakika.

Faida yaweza kuwa kubwa au kuwa nzuri kukufanikisha haraka na muda mwingine yaweza kuwa ndogo ikakufanikisha pia. Biashara yenye faida wakati mwingine yaweza kuanza pasipo faida ila itategemea uendeshwaji wake ikatoa faida na kujengeka vyema.

Mfano:
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 siku moja katika sherehe za maonesho ya saba saba mkoani Dar es salaam, katika ufunguzi wa maonesho hayo kulikuwa na mabanda ya ujasiriamali mbalimbali likiwemo na banda la ndugu Reginald Mengi ambalo lilikuwa ni banda lililotembelewa na rais wa awamu ya kwanza hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo mwalimu alikutana na biashara ya maji ambayo yalikuwa yanauzwa hakika alishangazwa mno, unajua kwa nini? Wakati ule maji ya kunywa katika chupa hayakuwa na soko Tanzania kama wakati huu. Hivyo, hata faida yake haikuwa kubwa lakini hakukata tamaa hadi leo hii anaendelea.

Hivyo katika biashara suala la faida yawezekana kabisa biashara yako unapata faida ndogo usihofu maana yawezekana kabisa kesho Taifa litakutegemea kupitia hiyo biashara yako. Kataa kabisa kukata tamaa bali bidii iwe ndio msingi wa mambo yako. Ni vyema ukaitazama biashara yako kwa mtazamo wa kijasiriamali.

UJASIRIAMALI NI NINI?  Suala la biashara kupata faida ni muhimu kulitazama katika muonekano wa ujasiriamali.

Katika suala la faida si bei kubwa ndio itakupa faida bali biashara yenye mzunguko ndio itakuingizia faida.
Watu wengi wameanzisha biashara nyingi sana na nzuri lakini kukosa walengwa wa faida imesababisha biashara zao kutoendelea.
Katika mtazamo huu wa faida haikatazwi kuuza vitu vya bei ya juu bali lenga vyema faida itakayokupa mzunguko wa biashara yako.

   Kwa upande wa huduma pia, faida itazamwe vyema kwa mfano:
   Kuna huduma nyingi sana zina faida sana lakini jinsi ya kulenga kupata faida huduma hizo zimesababisha kuzorota na kutoendelea kabisa. Mfano... ''Kuna vituo fulani vya afya katika tafiti ambazo niliwahi kufanya eneo fulani kila hatua mgonjwa anayopita kutibiwa anatozwa hela. Kuandikisha majina unalipia fomu, kuonana na daktari unalipia hela, kuchukua vipimo unalipia hela, tena ni maeneo ya watu wa hali ya chini kabisa wakiwa ni wakulima pekee. Hii ilipelekea wateja kukosekana kwani faida ililengwa zaidi.
Kwa ushauri wangu (Benson Mahenya) faida ni vema iwepo lakini itakayokuza biashara. Mara nyingi unapoanza biashara anza na gharama yenye kulenga faida kidogo. Ikijulikana gharama yaweza kupanda kidogo.

Suala la faida katika biashara ni vema litazamwe vyema kwani laweza kukuza biashara ama kuiangusha. Ni vema faida ikapewa kipaumbele cha kuboreshea mazingira ya biashara ili iweze kukua.

ZINGATIA HAYA JUU YA PESA ZAKO.
> Katika suala la pesa na malengo yako, jitahidi kuiheshimu pesa ya biashara au jaribu kuitofautisha kabisa 
   na pesa ya matumizi hasa starehe.
> Usiingie mkopo hela ya biashara kununua vipodozi, kustarehe na kufanyia anasa.
   Tafuta chanzo kingine cha pesa kufanyia hivyo si biashara kwani mkopo utakugharimu.
> Pesa ya biashara iwe ndio msingi wa hatua nyingine ya kukutangaza kwenye soko. Jinsi utakavyoiheshimu,
   itakuheshimu na kukupa heshima, wengine hudai pesa yaweza kukukalisha na yeyote na kusikilizwa na
   yeyote.

> Pesa ni sabuni ya roho, yaweza kuleta kicheko japo simanzi imewazunguka wengi.
> Jitahidi kutunza/kuwekeza zaidi kuliko kutumia. Matumizi yako yasizidi kipato chako.
> Usidharau pesa ndogo kwani ndio iletayo pesa kubwa na nyingi.
> Punguza matumizi yasiyo ya lazima kwenye mzunguko wako, mfano:

* Sio kila kitu cha kununua na kula
* Zima taa ukimaliza shughuli zako nyumbani
* Zima vifaa vyote vinavyotumia umeme ofisini kwako.
* Usiendeshe gari unaongea na simu kwani waweza pata ajali ikakupa matumizi mengine.
* Zingatia usalama barabarani kuepuka kupigwa faini, mfano kuendesha gari kwa kasi, kuendesha kwa
   uzembe na kuchelewa kuamka.
* Punguza safari za kusalimia kila mtu kwani waweza pata matumizi usiyotarajia, mfano: kuchangia
   chakula kwa kuwanunulia rafiki zake mpenzi wako kwa kutokupanga (kuhonga ili kuficha aibu)
> Pesa yako ya biashara isikufanye ukaidharau ndoa yako hasa kwa wana ndoa waliofanikiwa kwa 
   kuanzia hali duni. Mmoja akifanikiwa iwe ni biashara sio kumnyanyasa mwingine. Waweza sababisha
   talaka itakayowatesa watoto.

*************************************************************************

Tuwasiliane kwa:
0659 700 002
halisitz@gmail.com


MWISHO: 
Kama ambavyo Blog hii imekuwa ikikuletea mafundisho yenye kubadilisha ufahamu/akili na maisha kwa ujumla; Unaweza kui-support Blog hii kwa kununua mafuta halisi ya alizeti yenyo ubora wa juu, Lengo ni kufanikisha Blog hii Iendelee kukuletea mafundisho mazuri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa ambao nimekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha msomaji wangu anapata kitu kitakachoweza kumtoa hatua moja kwenda hatua nyingine!
   Ili kujipatia Mafuta haya waweza kuwasiliana nasi kwa  0659 700 002 na Mungu atakubariki.
Asanteni sana wadau wangu! 




  


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:


Juu