Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO


Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mh. Fredrick Sumaye siku ya Jumapili ya tarehe 11/8/2013 alikuwa mzungumzaji ndani ya CHIMBO - School Of Thought iliyo chini ya Harris Kapiga ambaye ni Mchungaji, MC na Mtangazaji wa CLOUDS TV na CLOUDS FM Radio ya jijini Dar es Salaam.

Chimbo-School Of Thought hufanyika kila siku za Jumapili kuanzia saa 9:00 Alasiri Hadi saa 1:00 Usiku, Mahali ni Sinza Nchi Ya Ahadi (zamani kamanyola).
Mh. Sumaye alizungumza na umati mkubwa wa vijana waliohudhuria siku hiyo juu ya jinsi na namna ya kuitunza amani ya Tanzania kwa ajili yetu na kizazi kijacho baada yetu.

HIKI NDICHO ALICHOSEMA MH. SUMAYE.

Mh. Fredrick Sumaye alifunguka kwa kuonyesha uzalendo wake na mapenzi yake kwa nchi ya Tanzania ambapo hakuzungumzia chama chochote cha siasa pamoja na kuwa yeye ni mwanachama wa chama fulani kikubwa hapa nchini.

Mh. Sumaye alisema:
Amani ya Tanzania inaletwa na itatunzwa na sisi wenyewe, unajua tunaitumia siasa vibaya. Lazima sisi kama viongozi wa siasa tunatakiwa tuwe makini sana kama kweli tunataka amani iendelee kuwepo. Na umakini wetu lazima haki ionekane inatendeka ipasavyo.
Lazima vyama vya siasa viwe makini, wote tufuate sheria, tume ya uchaguzi iwe muelekezi mkuu wa taratibu za uchaguzi na tusitumie vijana kuvuruga au kuwapambanisha.

Aidha aliendelea kusema kuwa:
Zipo dalili mbalimbali za vyama vya siasa kuanzisha majeshi na hilo ni jambo la hatari litakalovuruga amani yetu kama sio kuipoteza kabisa - alisisitiza.

Katika hotuba yake, Mh. Sumaye alionekana kuongea kwa hisia sana na kuwasihi umati mkubwa wa vijana waliojitokeza kuwa makini maana wao ndio wanaotumika kwa sababu wana nguvu na rahisi kuchochewa. ''Lakini mkiwa makini hamtatumika kuchochea vurugu/fujo''-alisema kwa msisitizo.
Endapo mtakubali kutumika na kuchochea fujo/vurugu mtambue kwa hakika kuwa hizo fujo na vurugu mtakuwa nazo ninyi kwa muda mrefu kuliko mtu mwingine yeyote akimaanisha kizazi hiki na kile kijacho baada ya hiki.

Kwa hiyo kama tunataka kurithisha amani hii kwa wenzetu wanaokuja huko baada ya sisi na baada na ninyi (vijana) na vizazi vingine ni lazima tufuate taratibu nzuri za siasa.

*****************************************************************************

Click hapa uweze ku-LIKE Ukurasa wetu wa CHIMBO-SCHOOL OF THOUGHT

Jumapili hii ya Tarehe 18/8/2013 Mh. Jerry Slaa atazungumza ndani ya Chimbo-School Of Thought
mada atakayozungumza ni ''JINSI GANI UNAWEZA KUIISHI NDOTO YAKO'' How to Live your Dream.






MH. SUMAYE AKIWA AMEPIGA PICHA YA PAMOJA NA CHIMBO DIRECTORS

Wasiliana na Blog hii:
0659 700 002
0653 100 100
halisitz@gmail.com

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:


Juu