Chat Now

HABARI MPYA

FUNDISHO LA MSINGI

PICHA NA MATUKIO

CAPACITY BUILDING CLASS

MAHUSIANO

NUKUU YA LEO

THREE - FOUNDATIONAL PRINCIPLES TO DEVELOP A PROFITABLE BUSINESS.

Hello brethren in Christ Jesus,
Would like to share with you briefly the three foundational principles to develop a profitable business.






1. Acceptability.
  God given a right to increase at what you (I) do. Increase is a power of God's plan. The plan of God is to increase.
God is not the God of decrease but the God of increase. His plan for me and you is that we increase in our business/professional life.

   It is the sin to stay at the bottom.
   It is not evil to begin small but it is evil to remain small.

2. Willing To Change.
  You must be willing to change in order for you to experience change.
Not where you are but who you are because who you are changes where you are; you can be a success in the desert, in the wilderness, in any dry place, you can prosper anywhere you are if you know who you are.
  It is not your locality but it's your Identity.
Identity in CHRIST changes your locality in life. What man needs is a discovery. Positive discovery brings positive recovery.

  Jesus was involved in business; His powerful statement - '' I must be about my father's business'', means-His business was to fulfill the assignment of His Father and that was to bring hope, liberation and lifting to humanity.
  So whenever you involve in anything that brings about profit in our life and help to bring service to humanity that is a BUSINESS.

Proverbs 14:23
  In all labor there is profit, but idol talk leads on little poverty.
-The men wasn't designed to work for nothing.
-Everything you do - is the sign to progress. If you involved in life and what you are doing is not profitable it is an indicator that you are involved in the wrong thing.
-You are not born to be failure on what you do; you were designed for profit.

3. Apostolic Anointing.
  Church Changing.
* We don't gonna church to have a good time, to feel good bounds/bumps, to fall down.
* We come to church - to be changed, to be adjusted, to be corrected, to be up-graded, to be re-defined.
* We come to church to live at better humans; thus why we're here.
* We're not here to be blessed - we're here to change (in the church).

Blessings.
- Big revelation; you're blessed, you shall be blessed on coming and going, in the field, in the city- you're blessed.
- So you're not here to be blessed - you're already blessed.

About A Church.
 A church is not a building - a building doesn't make a church, but we're a church ( Ephesians 4:16).

Grace.
 Is a divine impact, a divine resource upon the heart that will eventually depending on the way you live.
Is a divine resource, it's a spiritually Energy we're given according to the measure of the gift of CHRIST.

Hallellujah, Glory to the Most High God!
May you have a good time to meditate on it and become what God designed you to be in Jesus Mighty Name, Amen.

Contact us:
+255 659 700 002
+255 756 145 417
mdeejunior@gmail.com (email)
mdee.junior (skype)
@mdee_junior (twitter)


DREAM BIG AS YOU GROW BIG.

KONA YA WATUMISHI: Kutoka kurasa za facebook na groups mbalimbali.

   Hiki ndicho alichofundisha mtumishi wa Mungu Gasper Madumla kupitia page yake ya NENO LA MTUMISHI. Blog hii imeona vema kukushirikisha nawe upate kile Mungu anataka upokee siku ya leo na ndio kusudi la blog hii. Karibu twende pamoja.

   Pia mtumishi wa Mungu Upendo Benson, na Mary Muna katika kurasa zao za facebook wamezungumza kitu ambacho kitakusaidia kutafakari. Upendo Benson ametoa dondoo (highlight) fupi juu ya mahusiano, ni kazi yako kupanua akili na ufahamu wako juu ya kile ambacho ametoa kama highlight.
KARIBU.


Mtumishi Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiweee……

 NENO:SIMAMA IMARA UKAUONE WOKOVU WA BWANA.
Ninanakusalimu mpendwa katika jina la Yesu Kristo aliye hai,nikimuomba Bwana Mungu afungue moyo wako ili upate kupokea hiki ninachokuletea siku ya leo,maana ujumbe huu umekusudiwa kwako wewe mpendwa usomaye ujumbe huu, na wala si mwingine aliyekusudiwa bali ni wewe.
Ninakuhakikishia kabisa endapo utafanikiwa kusoma mpaka mwisho,Mungu atakufanyia jambo,nawe utapenya kupitia somo hili,litakuwa Baraka sana kwa kila atakayesoma.

Wokovu wa Bwana haupatikani kwa njia nyepesi. Maaana hata maandiko yanatuambia kwamba -yeye takayevumilia hata mwisho ndio atakaye okoka. 

Swala la kuokoka ni jambo la muda mfupi sana yaani ni dakika tu pale utakapokuwa umeongozwa sala ya toba na kumaliza,ila kuna maisha mengine baada ya hapo,hayo maisha ni WOKOVU. 

Na tunaokoka ili tufanye kazi ya Mungu,na sio kwenda mbinguni tu,maana ingekuwa swala ni kwenda mbinguni tu,basi watu wote waliokoka wangekuwa wamekufa tangu siku ile walipookoka,BALI WAPO HAI ILI WAYAFANYE MAPENZI YA BABA NA MWISHO NDIO WAFIKE MBINGUNI. Halleluyaaa..

• Maisha ya wokovu ni mchakato wa maisha ya utauwa
• Utauwa ni maisha ya kumlingana na Mungu,yaani maisha ya UTAKATIFU
• Na kumbuka bila huo utakatifu hakuna atakaye muona Mungu,( Waebrania 12 :14 )
Kumbe ! Yatupasa tuwe watakatifu kwanza ili tuweze kumuona Mungu, Watu wengi utawasikia “ Jamani nimemuona Mungu kwa njia tofauti tofauti, Hali wao si WATAKATIFU,maisha yao yamejaa dhambi tupu,HAPO HAKUNA MUNGU LABDA KUNA mungu . Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mungu na mungu,

^ Mungu = Baba wa Mbinguni aliye hai,Jehova, MUNGU MWENYE NGUVU
^ mungu = miungu ya wapagani,anaweza labda kuwa ngombe,n.k HANA UTUKUFU

Wewe mpendwa endapo utasimama imara kuutafuta uso wa Mungu, Hakika utauona wokovu wa Mungu, na hapo utakuwa ni wa tofauti na pale ulivyokuwa kabla.

Tunasoma KUTOKA 12 : 1-2

“ Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 
Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. ”

Hawa wana wa Israel walikuwa utumwani muda wa miaka 430 (Kutoka 12 : 40 ) ila Mungu alikuwa ana haja nao,Haja ya Mungu ilikuwa anataka ajitwalie utukufu kupitia wao waende kumuabudu Mungu aliye hai,

Kumbuka Mungu akiwa na haja na wewe ni lazima atakupata tu,na atakupandisha juu pindi utakapo tii sauti yake kwa BIDII 

Tunasoma Luka 19 : 29-31

“ Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi, 
akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa. 
Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji. ”

Huyu Punda alikuwa kifungoni yaani alikuwa amefungwa katika NIRA ambayo kwa hiyo alikuwa hana uwezo wa kufanya chochote kile atakacho kufanya isipokuwa ni kufanya yele atakayo bwana wake aliyemfunga.

Halleluuyaaa…

Punda wa sasa anawaeza kuwa wewe,ikiwa umefungwa yaani hauwezi kufanya chochote kile utakacho na kufanikiwa BASI UPO KIFUNGONI shetani yeye ufunga watu,

Sasa tazama pale Yesu anasema “ 31” na alipofunguliwa huyu punda tunaona anatandikiwa nguo zao njiani naye huyo punda anapita kwa heshima kubwa kabisa ambayo hapo mwanzo alikuwa hawezi kuipata kabisaa,kwa sababu alikuwa AMEFUNGWA 

Tena huyo punda baada ya kufunguliwa na Yesu,Bwana Yesu Kristo akampanda,akaka juu yake huyo punda na watu woteee wakapaza sauti zao kwa kelele za shangwe 

Maana tena walikuwa hawamuoni punda bali wanamuona Yesu wa nazareti aliye hai akitembea juu ya punda,MAANA YEYOTE YULE ALIYEMBEBA YESU,SI YEYE ATAKAE ONEKANA BALI NI YESU NDIE ATAKAYEONEKANA BADALA YAKE, 

NA MTU HUYU NI YULE ALIYESIMAMA IMARA KATIKA MAISHA YA UTAUWA ,NA WATU WATAKUPA KIBALI NA HESHIMA KUU, SABABU SI WEWE BALI NI YESU JUU YAKO.

Ooooh,HALLELUYAAAAAA,
Mtu mmoja aseme AMEN,

Najisikia nikuhubirie zaidi,THANKS JESUS 
Kwa kukufanya wewe kuendelea kusoma ujumbe huu,hakika Bwana Yesu ana haja na wewe,maana wewe ni kama huyo mwanapunda ambaye Yesu alikuwa ana haja naye.

Sasa turudi katika andiko la kwanza
KUTOKA 12 : 1-2

Hawa wana wa Israel baada ya kuishi miaka mingi namna hiyo tunaona Mungu anawaambia kwamba mwezi huu utakuwa ni ni mwezi wa kwanza wa miaka kwao,

hii inamaanisha siku ile ndio ilikuwa haswaaa ni siku ya kuokoka kwao, maana hata miezi ilibadilika,miaka pia ilibadilika, KWA SABABU HII “ YAKALE YAMEPITA YAMEKUWA MAPYA” Yaani mtu yeyote mwenye dhambi akija kwa Yesu Kristo mtu huyo anafanyika mpya na Bwana Mungu azikumbuki tena dhambi zake.

• Ukisimama imara utauona wokovu wako
JAMANI MAMBO MENGINE HUJALOGWAAA!
BALI TU ,MUNGU ANATAKA UMTUMIKIE ILI NA YEYE AKUPIGANIE.

Tunasoma Kutoka 14 : 13
“ Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. ”

Ninakuambia hivi ;
Kwa yale makwazo yanayokufanya ushindwe kupokea ahadi za Mungu,leo ndio mwisho wake na hutayaona tena endapo utamaanisha kulichukua somo hili na kulifanyia kazi
Maana njia ni moja tu ,nayo ni YESU KRISTO PEKEE yeye ndio njia na kweli.

Tazama mstari huo,Mungu anasema “ USIWAOGOPE HAO WAMISRI ”
• Magonjwa uliyonayo ni wamisri
• Kufungwa Kutokuolewa/kuoa ni wamisri
• Kudumaa kiroho ni wamisri tu
• Ugumu wa maisha ni wamisri tu N.K

HAYO YOTE USIYAOGOPE WEWE SIMAMA NA YESU KRISTO UKIMTUMIKIA KWA FURAHA ZOTE,MAANA HAO WAMISRI HAUTAWAONA TENA KATIKA JINA LA YESU KRISTO,POKEA…..

Ni ombi langu kwako kuwa,Wakati uombapo usiwe unapenda kuomba mambo ya maisha yanayoharibika,na yenye kupita mfano kuomba kila wakati MUME,MKE,KUJENGA,KUPATA KAZI,KUNUNUA GARI,KUPANDISHWA KAZI NA MAMBO KAMA HAYO, 

Bali wewe taka sana mambo ya rohoni naye yote utazidishiwa omba MUNGU AKUFUNGUE MACHO YA ROHONI,.AKUPE NJAA YA KUMTAFUTA,NA YOTE YA ROHONI,NA HAPO NDIPO UTAWEZA KUSIMAMA IMARA UKAUONE WOKOVU WAKO.




  • Kipengele kinachoitwa kupenda hakina professor wala Dr wala mwalimu wala mtaalam wala police wala rais wala waziri... ukishapenda tu wewe baaasi.... ikifika pa kutendwa utatendwa tu, pa kufanywa zoba utakua zoba tu, pa kudanganywa utadanganywa tu, pa kulizwa utalizwa tu, pa kusalitiwa utasalitiwa tu.. kwenye kipengele hiki cheo hakina kazi na ujanja wako unawekwa kapuni.



    Give all of you to Jesus...and He will make what you think is nothing...into something. What you keep from Jesus-keeps you in confinement...what you give to Jesus-is what defines you. Give Him what you have so He can define you! (John 1:3).



Mungu awabariki kwa kufuatilia blog hii.
Tunakaribisha maoni kuhusu blog hii.

Wasiliana nasi kwa:

+255 659 700 002
+255 756 145 417
mdeejunior@gmail.com (email)
@mdee_junior (twitter)
mdee.junior (skype)

DREAM BIG AS YOU GROW BIG.

KIOO CHA BLOG: SAFARI YA HANA KUELEKEA MAJIBU.

   Nakusalimu kwa Jina la Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Amina.

   Katika kioo cha blog hii, leo tunatazama siri ya kuelekea majibu yadumuyo. Mtumishi wa Mungu Hana katika kitabu cha 1Sam ndiye KIOO chetu cha leo. Kumbuka kuwa Mungu alimfunga tumbo asizae, lakini ilikuwa ni kwa ajili ya Utukufu wake mwenyewe (MUNGU), hatimaye Bwana akamuona na kumpa uzao baada ya kumlilia sana! Hana alienda mbali zaidi ya ukawaida wa Wakristo wengi wa sasa (beyond normality).

   Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana ni kwa nini tunaomba sana au tunaombewa sana lakini hatuoni matokea halisi na mabadiliko katika maisha yetu? na yakiwepo matokea kwa nini yanakuwa ni ya muda mfupi tu? Tatizo liko wapi? Je! mimi ninayeomba/kuombewa ndo nina tatizo? na je tatizo liko wapi? je! nalitambua tatizo? Majibu ya maswali haya ndio mpenyo na ufunguo wa majibu ya maombi tuombayo/uombayo.

   Wakristo wengi kama sio wote tumekuwa na tabia sugu ya uvivu na kuridhika (complacent) kwa matokeo hafifu tuyaonayo. Hatupendi kuomba, tunasubiria kuombewa; na tukiomba twaomba emotionally/kihisia sio kwa target/kulenga, hii inatufanya tuwe tegemezi.

   Hebu kwa pamoja kupitia KIOO cha blog tumtazame Hana, yumkini anayo majibu.

1Samuel 1:1-20.
   Wakristo wengi tumekuwa na tabia ya kutegemea maombi ya kuombewa na watumishi wa Mungu. Na hii ni kwa sababu tumeishia tu kutambua hitaji tulilo nalo  na sio uhitaji wa hitaji (requirements of the need).
Mfano; unahitaji Mungu akupe mume/mke, na hilo ndio hitaji lako; lakini ufanye nini ili upate hitaji lako kwa wakati na majira sahihi kutoka kwa Bwana, huo ndio uhitaji wa hitaji lako. Hapa ndipo kuna tatizo, kutambua uhitaji wa hitaji na mwisho wa siku tunaanza kupeperushwa na upepo wa huduma za maombezi(sipingani na huduma za maombezi) la hasha! Nataka Mkristo afike mahali aweze kusimama yeye kama yeye na Mungu wake kwa sababu watumishi wanaotuombea wana nafasi yao, Mungu naye ana nafasi yake na sisi tuna nafasi zetu ili Mungu atende(we must play our part). Tusiwabebeshe watumishi wa Mungu nafasi zetu/wajibu wetu kwa Mungu wetu, nasi tutapona.
Nataka nikuambie, usipotambua nafasi yako, na uhitaji wa hitaji lako utawekewa mikono, miguu na mwisho wa siku utafanyiwa maombi yanayoambatana na kupigwa makofi lakini hutaona badiliko lolote kwa maisha yako. Tatizo ulilo nalo lisikufanye uwe yatima wakati unaye Baba anayekujali, badilika sasa na badilisha mfumo wako wa maombi.

Mstari wa 4-5
   Eli anaonesha kumpenda sana Hana hata kumpa sehemu mara mbili kwa ajili ya dhabihu. Eli hakutambua uzito/uhitaji wa hitaji la Hana mkewe.

Mstari wa 8.  Tunaona Eli akimfariji Hana kwa maneno mazuri sana akisema; Je! mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? Ni kweli ametumia lugha nzuri inayoonesha kujali/kupenda na kuthamini akimaanisha kuwa nakupenda hata kama huna mtoto, pamoja na lugha zote na matendo yote yaliyoonesha Eli kumpenda Hana vile alivyo bado haikuweza kugusa tatizo la Hana. Ukweli ulibaki pale pale kuwa Hana bado hana uwezo wa kuzaa.

   Mwisho wa siku Hana anafunguka, moyo wake ulijaa huzuni, macho yake yalijaa machozi hata asiweze kula, alikuwa na uchungu rohoni mwake. Faraja kutoka kwa Eli, kuhani haikumsaidia kitu, ilikuwa ni faraja ya muda tena inawezekana Eli, kuhani alithubutu hata kumwekea mikono na kuomba pamoja naye lakini bado jibu halikutokea/lilifichwa.
Hatimaye Hana akatambua kuwa hakuna majibu kwa mwanadamu wala kwa mumewe, wala kwa fedha, mali na utajiri wao.

   Hana hakutaka tena kulialia mbele za watu wala hakutaka faraja ya mwanadamu, ndipo alipoamua kuinuka akamwacha Eli kuhani na kuingia hekaluni peke yake mahali ambapo mchungaji hakuwepo wala mtume, wala nabii, wala kwaya, wala praise and worship team haikuwepo bali alikutana na UWEPO wa mzee wa siku Mungu Jehovah ndilo Jina lake. Mstari wa 9-10. Biblia inasema kuwa Hana alimuomba Bwana huku akilia sana.
Hebu tujifunze kumtafuta Mungu na uwepo wake mana ndiko kuliko na majibu yetu. Hana akaeleza uhitaji wake mbele za BWANA.

   Inawezekana unapita katika nyakati ambazo kila akutazamaye anakuona duni, si kitu, haufai, unadharauliwa; Lakini usife moyo huo sio mwisho wa maisha yako. Tambua uhitaji wa hitaji lako, ingia nyuani mwa Bwana, mimina roho yako mbele zake, Hakika utatoka hapo ulipo na hutakuwa kama ulivyo leo.Kataa upepo wa kukimbilia maombezi kila mahali unaposikia kuna maombezi, jifunze kufanya sehemu yako kwanza. Hana akamjibu Eli, kuhani ''Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kittu'' haya ni maneno ya kuchoshwa na hali aliyokuwa anapitia.
 
   Baada ya maombi mazito ya ufunuo, Hana alitoka hekaluni (uweponi mwa Mungu) akiwa na furaha tele na amani wala uso wake haukukunjamana tena maana aliingia hekaluni akiwa na roho ya uchungu huku akilia sana na uso wake ulikunjamana sana tena hakuweza kula chakula, lakini hali yake ilibadilika baada ya kukutana na Rehema za Bwana hekaluni. Furaha ikarejea na amani akaweza kula chakula maana kabla ya hapo chakula kilikuwa hakishuki! Mstari wa 18.
Uwepo wa Mungu hubadilisha maisha ya mtu rohoni na mwilini na kumfanya kuwa mtu mpya tena humuondolea aibu.
   Hitaji la hana lilikuwa ni kupata mtoto tena mtoto mume; na uhitaji wa hitaji lake ulikuwa ni kutafuta na kukaa uweponi mwa BWANA na kumimina roho yake/hitaji lake , kuwasilisha haja yake kwa Bwana na sio kwa wanadamu ambao leo wapo kesho hawapo, leo wanakuchekea kesho wanakung'ong'a na kukusemea mabaya.


HITIMISHO:
Majibu ya Hana yalitokana na yeye kutambua nafasi yake na kuingia katika utendaji kiuhalisia.

Je! tatizo ulilo nalo limekufanya uonekane duni, usiyefaa, si kitu si lolote, hata jamii inayokuzunguka imekukatia tamaa na kukudharau; au ndoa ya iko hatarini (ICU) kwa sababu huzai hata mume amekuwa na nyumba ndogo.

TAMBUA NAFASI YAKO, SIMAMA NA MUNGU, kama alivyomtokea Hana atakutokea na wewe leo kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth Mwana wa Mungu Aliye Hai.


   Bwana Yesu, kwa utukufu wa jina lako takatifu na kwa Damu yako ya thamani; nakusihi/naomba roho ya ufufuo kwa ndugu yangu huyu ambaye anafuatilia KIOO cha blog hii, kutana na uhitaji wa hitaji lake kwa jina lako Yesu. Kila mara anyoshapo mikono yake kuelekea hekaluni mwako/madhabahuni pako naomba umsikie na kumtendea muujiza zaidi ya vile ulivyotenda kwa mtumishi wako shujaa HANA. Na kila aitiapo msaada wako Eeh BWANA ukashuke na kumsaidia, zaidi sana macho ya moyo wake yatiwe nuru yapate kuona maajabu yatokayo katika sheria yako ambayo ni Neno lako, pia ukampe neema ya kutambua uhitaji wa hitaji lake pale apitiapo nyakati ngumu au mazingira yeyote yale na akawe mwanafunzi mwaminifu katika hali zote anazozipitia au atakazozipitia katika maisha yake. Mpe neema ya kipekee kuvuka ng'ambo ya bahari/ng'ambo ya ufahamu alio nao sasa apate kukujua zaidi na kukufuata wewe peke yako. Mpe kuitambua nafasi yake na kile anapaswa kuwajibika kwacho.
   Kwa Jina La Yesu Kristo, nimeomba na kuamini kuwa ndugu yangu huyu amepokea na ya kuwa hakika hutamwacha hata nukta moja. AMINA!



















Kwa Msaada zaidi au Maoni wasiliana:

+255659 700 002
+255756145 417
mdeejunior@gmail.com
@mdee_junior (twitter)
mdee.junior (skype)

DREAM BIG AS YOU GROW BIG!





 





2013 ACHILIA KILA KITU KWA BWANA; 'SURRENDER YOUR PERSONALITY AND IDENTITY TO GOD'


   Mdee, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya Imani ya wateule wa Mungu (yaani wasomaji wa Blog hii), na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa; katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu; kwa msomaji wangu, mteule hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.

   Kwa sababu hii nalikuandikia ujumbe huu wa mwaka 2013 upate kujitambua wewe binafsi na kile unachomiliki. Na huu ndio ujumbe wa Bwana kwako.

UNA NIIN MKONONI MWAKO?

Kutoka 4:1-10, 20
...BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo....
...Na Musa akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.

   Baada ya Musa kumlilia sana Mungu, Mungu alimwambia una nini mkononi mwako?
Kuna mambo kadha wa kadha tunayoweza kujifunza kutoka kwa Musa.
i> Fimbo ilikuwa inamaanisha nini kwa Musa
ii> Fimbo inamaanisha nini katika maisha yetu leo.

  Fimbo ya Musa ilikuwa ni zaidi ya fimbo. Iliwakilisha maisha (personality) na utambulisho (identity) yake. Fimbo ilimtambulisha Musa kuwa alikuwa anamiliki kitu gani, Lakini Mungu anamwambia itupe fimbo chini (Surrender) yaani Mungu alikuwa anamwambia Musa kwa lugha ya fumbo ayaachilie maisha yake kwa Mungu (na hii ni kuthibitisha kuwa fimbo iliwakilisha maisha ya Musa), na alipofanya hivyo Mungu aliyabadilisha maisha yake.

   Mpango wa Mungu na maisha yetu unaweza kucheleweshwa lakini hauwezi kuondolewa/kupotezwa. Kilicho cha Mungu > Hakuna ambacho Mungu anaweza kupoteza katika maisha ya mtu...''Rejea miaka 40 ya Musa Jangwani akichunga.
Chochote alicho nacho mtu yeyote kiwe chanya au hasi hakiwezi kuwa na maana kama hajakikabidhi kwa Mungu.

   Upande wa pili wa maisha ya Musa, fimbo iliwakilisha matatizo aliyopitia (life back ground); inamkumbusha matatizo aliyowahi kupitia. Kwenye maisha usifike mahali ukajiona si kitu, usitazame mazingira unayopitia kwa sababu mazingira yanabadilika, bali mtazame Mungu kwa sababu yeye habadiliki.
   Fimbo iliwakilisha uwezo uliokuwa ndani ya Musa ambao haujatumika bado ( Unused Potential).
Usijiangalie na kujitafsiri kama watu wakuangaliavyo na kukutafsiri.

Mstari wa 20. Musa anatoka ukimbizini baada ya kusalimisha vitu vyake kwa Mungu. Kumbe tunapokuwa tumekumbatia vitu vyetu/haki zetu wenyewe tunakuwa tunaishi ukimbizini mahali pasipo na uhuru wa kweli, ni  sawa na kuishi utumwani katika nchi yako mwenyewe.

Musa akaichukua ile fimbo ya Mungu mikononi mwake. Hapa tunaona kuwa kabla ya hapo ile fimbo iliitwa fimbo ya Musa; Lakini baada ya kusalimishwa kwa Mungu ile fimbo ilibadilishwa jina ikaitwa FIMBO YA MUNGU hadi leo.
Vivyo hivyo tutakapoyasalimisha maisha yetu/kazi zetu/biashara zetu/watoto wetu/familia zetu/afya zetu na kila kitu kinachohusiana na maisha yetu ndipo vitakapobadilishwa majina kutoka kuwa vitu vyetu na kuwa VITU VYA MUNGU. Paulo mtume anadhihirisha hili pale anaposema; ''Si mimi niishiye bali Kristo ndani yangu'' inaonesha jinsi ambavyo alikuwa ameyasalimisha maisha yake kwa Kristo Yesu (Total Surrender).

   Ni mpaka tumeachilia kile tulicho nacho ndipo Mungu atadhihirisha utukufu wake na kukipa uhai. Fimbo ilifanywa kuwa HAI. Hatutafuti kitu kipya ili Mungu atende bali kile kile cha siku zote, na unapokikabidhi haimaanishi Mungu atakunyang'anya la hasha; ndio maana Musa aliendelea kuitumia ile FIMBO.

SWALI NAKUULIZA:

Una nini mkononi mwako ambacho hujakisalimisha kwa Mungu?
Jihoji, halafu salimisha leo kipate kupewa uhai wa Ki-Mungu sasa, na 2013 utakuwa mwaka wako wa kuhuishwa katika kila eneo la maisha yako. Kubali sasa Mungu aanze na wewe, na wewe uanze na Mungu.

Nakutakia kila la kheri katika mwaka huu, maisha yako na kila kinachohusiana na maisha yako kikageuzwe kuwa HAI tena katika Jina La Yesu Kristo wa Nazareth Aliye Hai.

   Salamu zangu mimi Mdee, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Halleluyah!


Mawasiliano:

+255659 700 002
+255756 145 417
mdeejunior@gmail.com
@mdee_junior (twitter)
mdee.junior (skype)

Dream Big As You Grow Big.



Juu